A
Anonymous
Guest
Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu, siku za hivi karibuni imeendelea kuibuka tabia ya baadhi ya Watu ambao ujitambulisha kama waamini wa dini mbalimbali wameufanya kama utaratibu rasmi kuingia kwenye magari daladala au mabasi abiria kuuza mafuta wanayodai kwamba ni tiba au dawa mbalimbali ambazo udai kwamba walengwa wakizitumia wanapona magonjwa waliyonayo ikiwemo kisukari na tezi dume.
Huku Zanzibar kuna watu wanaojitambulisha kuwa ni 'Shehk' ni mara nyingi nakutana nao kwenye daladala wanauza vitu hivyo kwenye magari huku wakitumia ushawishi wa kiimani kufanya Watu wanunue dawa hizo, ambapo.
Licha ya kwamba suala hilo linaleta usumbufu kwa abiria lakini linaleta mashaka juu ya usalama kwa wanonunua mafuta au dawa hizo ambazo sidhani kama wana vibali rasmi kwa kuwa wengi wao kupitia maelezo ambayo wamekuwa wakiyatoa juu ya matumizi ya dawa hizo yanaleta mashaka.
Hata hivyo licha ya kudai hawafanyi biashara badala yake wanatoa huduma ya vitu hivyo inayoenda sambamba na dua au maombi lakini inaonesha wazi dhamira yao ni kupora pesa za watu kupitia mgongo wa dini.
Tanzania Bara huko hili suala nakutana nalo sana kwenye magari yanayotoka Mikoa ya Kaskazini kuja Dar es Salaam hususani kipande cha kutokea Tanga, yanafanyika yale yale wanayofanya huku Zanzibar kwa kujifanya wanatoa huduma ya dawa na maombi kwa abiria waliopo kwenye gari lakini ushawishi wao mkubwa ni kupiga hela.
Ombi langu kwa Serikali naomba ifuatilie kwa ukaribu suala hili limeendelea kuwa kero kwa wengi, pia mamlaka zifuatilie juu ya usalama na ubora wa dawa zinazouzwa na watu hao kwa kutumia kivuli cha dini.
Lakini pia ni muhimu ili kuondoa mkanganyiko ni vyema Viongozi wa Dini mbalimbali wakatoa kauli za kujitenga na Watu hao waotumia mgongo wa dini bila kuzingatia taratibu stahiki.