Pre GE2025 Zanzibar: Polisi wakanusha taarifa ya Mjumbe wa Kamati Kuu ACT kudaiwa kutekwa na vyombo vya ulinzi, wasema alikamatwa na kuachiwa kwa dhamana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,854
4,866
Wakuu,

Mapema leo Naibu Katibu Mkuu wa ACTWazalendo -Zanzibar Omar Ali Shehe alidai kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Hadija Anuwar alitekwa na watu wasiyojulikana wakati wa uandikishaji katika Daftari la kudumu la Tume ya Uchaguzi Zanzibar -ZEC.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Jeshi la polisi limetoa ufafanuzi wa tukio hilo likisema Khadija alikuwa na dhumuni la kuzorotesha zoezi la uandikishaji daftari la kudumu, ambapo alikamatwa na kuachiwa baadaye kwa dhamana.



Screenshot_20250301_202616_Instagram.jpg
Screenshot_20250301_202627_Instagram.jpg
 
Kwani mwenye uwezo wa kufanya haya ni nani?.
Hivi unaweza kuja na ushujaa tena na gari zozote kisha mkanushe.
Kweli ushuzi na haja kubwa zijawai kuwa na ushirikiano ila zina ushirikiano kwenye ushiriki wa utumbo mkubwa.
 
Barua ya ufafanuzi na kupigia upatu mambo ya kujiandikisha kupiga yanahusiana vipi?

Watu wajiandikishe pia kwa tume hii hii ya CCM isiyo na usawa kwenye uchaguzi?
 
Yani imekanusha kuwa ijamkamata hapohapo imemuachia kwa dhamana.

Aisee yani hapa ndio tunajua akili zetu zipoje
 
Back
Top Bottom