ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 59,566
- 70,219
Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Mazrui ametangaza kuwa Hospitali zote Zanzibar zilizojengwa na Serikali ya Rais Dkt. Hussein mwinyi sasa rasmi zitasimamiwa na Sekta binafsi kwenye uendeshaji wake ili kuwe na huduma za kisasa na za Kimataifa.
Akiongea Visiwani Zanzibar leo August 16,2024 Mazrui amesema Wizara ya Afya imeingia makubaliano maalum ya uendeshaji na usimamizi na Sekta binafsi Ikiwemo EHN na TCL na kusisitiza kuwa Wizara ya Afya huo sio ubinafsishaji bali ni kuongeza ufanisi wa Hospitali hizo ikiwemo za Wilaya na za Mikoa ili Wananchi wapate huduma bora katika Visiwa hivyo ambako kwa miaka mingi huduma za Afya za Zanzibar ni bure kwa vipimo vyote huduma kubwa na ndogo.
"Tumebaini Wananchi wengi wanapenda kwenda Hospitali binafsi na wanapoteza fedha nyingi, wengine hawana wanaenda kwa Wafadhili wasaidiwe, kuwaondolea shida hiyo Wananchi sisi tunawalipa Sekta binafsi kwa niaba yao ili wapate huduma matibabu bila ya malipo, Watu wanatibiwa na kupata dawa zote na vipimo bila ya malipo yeyote na Serikali inawalipa Sekta binafsi wanaotoa huduma hizo" #Millard AyoUPDATES
My Take
Afadhari jambo Hilo liketokea Zanzibar ila lingetojea huku Bara Hakuna Kauli au matusi Wadanganyika wangeacha kumshambulia Rais kisa tuu ni wa pande Ile.
Nawapongeza Wazanzibar Kwa kuwaza Nje ya Box Ili kukabiliana na utaoaji Huduma usio rafiki.
Lakini pia hakikisheni Ajira zinasimamiwa na sekta binafsi pia Ili Serikali ibakie kusimamaia viwango vya taaluma na utoaji Huduma.👇👇