Zanzibar: CUF wamegoma kweli, CCM mbele kwa mbele!

which means waswahili, waarabu na wa asia hawana demokrasia? au si utamaduni wao?

Washiriki ama wasishiriki, ushindi ni lazima kwa CCM. Wakati wa kudekezana umeshapita. Demokrasia hii tumeiga kwa wazungu
 
Sasa hata kama CUF wangeshiriki uchaguzi huu wa marudio na kudhibiti bao la mkono, bado Jecha angeufuta tena tu..! Waachiwe CCM washiriki wenyewe uchaguzi wao..

Kwanza walishasema Zanzibara walimwaga damu kuichukua hivyo hawataitoa kwa makaratasi..
 
Gharama za uchaguzi wa marudio ni bilioni 4.5 acha kudanganya wewe

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
amesema hakuna mbadala wa kumaliza
mkwamo wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar, zaidi
ya kurudiwa kwa uchaguzi na kuhakikisha kuwa
Serikali imekamilisha bajeti ya kufanikisha
uchaguzi huo unaosubiriwa kutangazwa na
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar(ZEC).
Akizungumza na waandishi wa habari, Balozi
Seif amesema hivi sasa, serikali inasubiri tume
ya uchaguzi ya znz kutangaza tarehe ya kurudia
uchaguzi huo ambao gharama zake zinakadiriwa
kufikia shilingi BILIONI 7 kiwango ambacho
kilitumika katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25,
ambao matokeo yake yamefutwa na Mwenyekiti
wa ZEC Alhaj Jecha Salim Jecha kwa sababu
mbalimbali.
CHANZO:Channel 10 News 2/1/2016.
 
SIPATI PICHA KAMA HAWATATUMA MAWAKALA KURA ZAO ATAHESABU NANI???

Hivi mtu ambaye hataki kushiriki uchaguzi, anahitaji kuhesabiwa kura? Hujui kwamba waliomba/walitaka majina ya wagombea wao yaondolewe kwenye orodha, ni tume ya Jecha tu imelazimisha yawepo.
 
Kuna viongoz wa ccm ni wakubwa kwenye kutoa matamko ya kitaifa kuliko wenye dhaman hiyo serikalin...
 
Washiriki ama wasishiriki, ushindi ni lazima kwa CCM. Wakati wa kudekezana umeshapita. Demokrasia hii tumeiga kwa wazungu
Hata uchaguzi tumeiga huko huko basi tuache tu vyote sababu hatuviwezi kabisaa, japo na elimu pia kuwa tumeiga huko huko kwa wazungu lakini haitusaidii kitu, nayo tuifute tu. Sababu wanao fanya hayo mambo ni wale wanaoitwa madokta na maprofesa.
 
La busara ni Jecha kuwapa ushindi kutokana na timu pinzani kutofika uwanjani. Hili la kuendelea na mechi bila kushiriki timu pinzani sio kishekesho tu ni uwandazimu. Fungeni mabao hadi elfu ukweli unabaki pale pale hiyo siyo mechi.
Sometimes timu pinzani isipofika uwanjani mechi inapigwa na "chandimu" timu ya watoto wa mtaani ambao hutumia mpira wa ndimu! Nimeona kina Sibida na Cheyo wamejitokeza, hao ndio chandimu
 
Hivi kuna waangalizi ambao wameshafika maeneo ya uchaguzi mpaka sasa..? Maana nilisikia Waangalizi toka Marekani na Ulaya wameisifu Serikali ya Jamhuri na ile ya Mapinduzi kwa uamuzi wao wa busara wa kufuta uchaguzi wa October na kuuitisha tena March 20, na wamesema watatuma waangalizi wao huku wakiwa na uhakika wa usalama uliotamalaki na utulivu uliopitiliza toka kwa wananchi..
 
Zec waache utoto kuwa na picha shein na box nyingine liwe giza tu maana hagombei na mtu iwe kama zama za mwalimu
 
Mzee VUTA-NIKUVUTE kwa jinsi ninavyo ona hali ya democrasia ya vyama vingi inavyo kwenda Afrika, nashauri kama bado kuna nchi hazijaingia kwenye mfumo huo, basi watakapo amua kuingia katika mfumo wa vyama vingi kile chama kilicho kuwa madarakani muda wote kifutwe wote waanze upya kusajili vyama vipya. Hapo watakua wamevunja mzizi wa vitina. Hata hapa Tanzania ilibidi kufuta CCM, wote tungeanza upya na vyama vipya, haya yote yasinge tokea. Lakini kwa sasaa inabidi CCM ivurugike kama KANU ndio kidogo tutaanza kuona mwanga, lakini hali iliyoko sasa ni giza tupu katika ulimwengu wa democrasia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…