Zanzibar: Askari wa JKU auawa, mkuu wa kituo cha polisi ashambuliwa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,810
Unguja. Askari wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU), Ramadhan Juma Hassan (24) ameuawa, huku mwenzake akijeruhiwa na kundi la watu wasiojulikana walipokuwa kwenye lindo katika sheli ya mafuta.

Akizungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu, leo Februari 6, 2024, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Hamisi Mwampelwa amesema tukio hilo limetokea saa 7:00 usiku wa kuamkia leo katika sheli ya mafuta Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.

Kwa mujibu wa Mwampela, kundi hilo la wahalifu linalodhaniwa kuwa zaidi ya watu 10 likiwa na silaha za jadi, lilivamia kisha likamnyang’anya silaha askari huyo kabla ya kutekeleza mauaji hayo na kumjeruhi mwenzake ambaye bado hajafahamika jina.

“Tukio ni la kweli limetokea katika sheli ya Tunguu, baada ya watu hao kuvamia waliwanyang’anya askari silaha, wakamuua na mwingine kumjeruhi. Baada ya kutekeleza uhalifu huo silaha hiyo walitelekeza hapo hapo kituoni,” amesema.

Mbali na kuua na kujeruhi, watu hao pia wanadaiwa kuiba fedha taslimu Sh10 milioni.

Wakati huo huo, kijana anayedaiwa kuwa mgonjwa mwenye matatizo ya akili anadaiwa kumshambulia na kumjeruhi Mkuu wa Kituo cha Polisi Mwanakwerekwe, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Fadhili Mdimbwe.

Licha ya kukataa kuzungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharib, Richard Mchonvu amekiri kutokea kwa tukio hilo, huku akiwalalamikia wananchi walioshuhudia, lakini hawakutoa msaada wowote.

“Kwanza tukio hilo ni la muda mrefu, siwezi kulizungumzia. Wananchi wanakuwa wanalalamika masuala ya uhalifu, lakini wanashangilia yanayotokea,” amesema Kamanda Mchonvu

Katika kipande kidogo cha picha jongefu (video), kinamuonyesha askari huyo akishambuliwa, huku wananchi wakishuhudia bila kutoa msaada.

Chanzo cha habari ambacho hakikutaka kutajwa jina kimeeleza kijana huyo anadaiwa ni mgonjwa mwenye matatizo ya akili mwenye cheti na tukio hilo linadaiwa kutokea Januari 27, 2024.

“Huyo mkuu wa kituo anaendelea na matibabu Dar es Salaam na alikaa ICU kwa siku nne, kwa sasa afya yake inaimarika siku hadi siku,” amesema.
 
Mimi najiuliza, huyo askari kabisa, tena mkubwa kituoni mwenye mafunzo, amepewaje kichapo heavy na mwehu hadi kupelekwa ICU?
Basi ni sawa kwa wale mapongo kulambwa stiki na wamasai
 
Probably askari aliyeshambuliwa ni kutoka Bara na Kichaa alikuwa Mzanzibar. Kwa unafiki wa wale Viumbe walikuwa wanatamani sana askari husika auliwe. Pole sana Afande, ugua pole
 
Sheli ni nini?

Sheli = gas station/petrol station.
Ni sawa na pikipiki kuiita Honda, au Paracetamol kuiita Panadol.

Brand name ya kwanza inaweza kubeba jina la bidhaa fulani, ni jambo la kawaida katika hatua za ukuaji wa lugha.
 
Back
Top Bottom