Zan_Exit iwe agenda ya upinzani Zanzibar

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,418
9,209
Baada ya CCM kupiga chini katiba ya wananchi hamna namna zaidi ya Mamlaka kamili. Zanzibar has nothing to lose but chains of oppression.
 
A
Baada ya CCM kupiga chini katiba ya wananchi hamna namna zaidi ya Mamlaka kamili. Zanzibar has nothing to lose but chains of oppression.

Acha uchochezi wewe kwann hupendi tuendelee na muungano wetu haaaaa una tatizo gani au inawezekana wewe sio Mtanzania na umetumwa na wapinga muungano tafadhali sana sana mkuu na jamiiforum tafadhali itoeni hiyo mada ifutwe pleaseee please please jamiiforum Admn angalizo haya maeneo yasiwe ndio chokochoko za kuhatarisha amani futa hiyo tafadhali
 
Uhuru wa kuwasilisha maoni katika mitandao ya kijamii usitumike vibaya tafadhali, Najua jamiiforum ipo Tanzania na uanzishwaji wake unakubalika kisheria sasa kama inafikia hatua ya kuangalia hizo post aisee lazima jamiiforum wajitathimini sana na uzalendo toa hiyo mada tafadhali
 
Muungano ukivunjika, sidhani kama Unguja na Pemba patakalika. Itakuwa ni msala mwingine kama wa Rwanda na Burundi. Acha tu muungano uendelee kwa faida ya Wazanzibari.
 
Kwa waliosoma physical geography, Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika iliyomegeka miaka milioni nyingi nyuma, kufuatia kitu kinachoitwa
Continental Drift Hypothesis - Tectonophysics - Great Rift Valley ...

Na hapa mnaweza kushuhudia jinsi Zanzibar ilivyomegeka!.


Hivyo Zanzibar ni hiyo ni sehemu yetu halali!. Hao Waarabu walipokuja Zanzibar waliwakuta wenyeji chini ya Mwinyi Mkuu. Hivyo hakuna cha mamlaka kamili, wala kujitenga!. Zanzibar ni sehemu ya JMT na itaendelea kuwa hivi!.

Pasco
 
Hawa jamaa wa chadema unafikiri ni kweli wameminywa demekorasia? Tatizo hawana hoja ndio maana kila kaneno wanakarukia. Walimfukuza think tank wao, Dr. Slaa sasa hawana siasa za issues bali kurukia rukia kila kaneno
 
Nchi inaongozwa na katiba na uanzishaji wa vyama upo chini ya katiba. Kijana unatakiwa uwe makini na thread unazozianzisha. Uhuru wako uwe na mipaka.
 
Ukimalizana Na Zan_Exit itakuja Na Pem_Exit Na hapo ndio patamu maana tutaanza Na wazan_Exit wasionekane Bongo
 

Wacha ijadiliwe ni hoja nzuri...
 
Wa znz wanayo sababu na haki ya kufanya hivyo..kuungana sio kuwekeana mamluki wa kuwatawala. Upande wa pili umekua ukiwa ekea mamluki kwa nguvu....tafakari ingekua hilo linafanywa upande wa pili ....jaribu kufikiri wewe upo upande wa znz
 

Pasco mimi nadhani Pwani yote , ni ya Znz , na ilikua hivyo kabla ya miKa 1000 nyuma , Mjerumani ndio aliondoa sehemu hio kuwa ya znz
 

we jamaa acha uongo, eti miaka milion nyingi nyuma, hiv tanganyika ina miaka hata 1000? hiyo tanganyika ya miaka milioni nyingi nyuma unaweza kutuletea ramani na mipaka yake hapa?!
 
Muungano sawa lakini unapogeuka manyanyaso wa nini huo, sasa angalia wengine wamefikia hatua hawataki hata ujadiriwe; kwanini ? Mnaficha nini? Muungano usiwe kichaka cha maovu, ni mangapi wazanzibar wanayalilia lakini hayatekelezwi ? Na kwa nini? Kila siku ni kero za muungano kero gani hizo zisizoisha.
 
Muungano sawa lakini unapogeuka manyanyaso wa nini huo, sasa angalia wengine wamefikia hatua hawataki hata ujadiriwe; kwanini ? Mnaficha nini? Muungano usiwe kichaka cha maovu, ni mangapi wazanzibar wanayalilia lakini hayatekelezwi ? Na kwa nini? Kila siku ni kero za muungano, ni kero gani hizo zisizoisha???
 
basi dunia nzima ni nchi moja.. maana jiografia inasema there was only a single landmas PANGAEA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…