Zambia yalalamikiwa kwa kujimilikisha kazi ya kubeba Mizigo Bandari ya Dar es Salaam

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,715
13,467
Salaam Wakuu,

Chama cha Wamiliki Malori Tanzania(TATOA) Wameiomba Serikali kuingilia kati Sheria iliyotungwa Zambia ya kusimamia Uingiaji na utokaji wa Mizigo Nchini Zambia.

Sheria hiyo inataka Mizigo yote inayoingia Zambia, 50% ibebwe na Wazambia Wazawa, 30% ibebwe na TAZARA na 20% ibebwe na Watu wengine.

Akiongea na Wanahabari, leo 24June 2021 Mkoani Dar Es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Truck Owners Association( TATOA) TATOA ndugu ELIAS Lukumay amesema kitendo hicho ni kinyume na muongozo wa SADC ambao unaelezea kuwe na biashara Huria, na inataka tushindane kwa ubora na bei si Sheria kandamizi.

Lukumay amesema, hili tatizo lisipofanyiwa kazi, Malengo ya Tanzania ya Kupitisha Mizigo Bandari ya Dar Es Sakaam ya kufikia Tani Milioni 30 kwa Mwaka haitafikiwa. Sasa hivi Tanzania inapitisha Mzigo tani Milioni 17 kwa Mwaka.

Amesema Tanzania inaboresha Miundombinu ya bandari na barabara. Lakini hatua hii ya Zambia itafanya Watanzania Wasinufaike na Bandari ya Dar Es Salaam. Pia Wasafirishaji wa Tanzania wamekopa kwenye Mabenki Mbalimbali, hivyo hii Sheria kama itatekelezwa Zambia, itapelekea Kampuni nyingi za Tanzania kufilisika.

Wamemuomba rais Samia awasaidie kuondoa hii kero kwani Watanzania hawataruhusiwa Magari yao Kupeleka Mizigo Zambia

Amechukua nafasi hiyo ya kuongea na Wanahabari kumpongeza kwa jinsi alivyoongeza Ufanisi wa Utendaji Bandarini. Foleni ya Malori imeisha, Utendaji umekuwa mzuri.
IMG-20210624-WA0009.jpg

Kutoka kushoto: Mallamia Elitunu Katibu Mtendaji Chama cha Mawakala wa Forodha TAFFA, Makamu Mwwnyekiti wa TATOA ndugu ELIAS Lukumay,Hussein Wandwi Mtendaji Mkuu Chama cha Wasafirishaji( TAT)
 
Hii inaweza kujibiwa na reciprocal action, hiyo mizigo ikivuka mpaka kuja tz ichukuliwe na wa tz ktk ratio hiyo hiyo ya wazawa, tazara, na wengineyo
 
hii inaweza kujibiwa na reciprocal action, hiyo mizigo ikivuka mpaka kuja tz ichukuliwe na wa tz ktk ratio hiyo hiyo ya wazawa, tazara, na wengineyo
Zambia ina-import kuliko inavyo-export! ... nchi zote jirani na Zambia zinatakiwa kushirikishwa; vinginevyo watajidai kutumia bandari sijui za SA, Mozambique, sijui wapi!
 
Zambia ina-import kuliko inavyo-export! ... nchi zote jirani na Zambia zinatakiwa kushirikishwa; vinginevyo watajidai kutumia bandari sijui za SA, Mozambique, sijui wapi!

Huko kote mbwembwe tu. Bandari yao iliyo pua na mdomo ni Dar.
 
Kinachotupatia competitive edge mpaka wazambia wafanye hivi ni nini?
 
Na wakiacha kutumia bandari yenu ?,au unafikiri Tanzania Tu ndio ina bandari ?
Umeliweka vizuri na wengi hawajui hili. Rais Frederick Chiluba mwaka 1992- 2012 ndiye aliyefanya biashara ya TAZARA i-drop baada ya kuelekeza mizigo iwe inapita bandari ya Durban. Dar -Lusaka ni pafupi kwa km 300 tu ukilinganisha na Durban- Lusaka.

Hivyo basi lazima siku zote tumuangalie mteja asije aka trade-off hiyo distance na kero zetu Watanzania. Akiona gharama za umbali zinahimilika anaweza kuamua vinginevyo
 
Huko kote mbwembwe tu. Bandari yao iliyo pua na mdomo ni Dar.
... kaka muogope Muumba! Zambia ina option ya kutumia bandari za Dar-es-Salaa au Beira, Msumbiji. Lets assume destination ni Lusaka. Tofauti ya umbali Beira - Lusaka compared to Dar-es-Salaam to Lusaka ni 1,095km. Iko hivi; Beira - Lusaka = 852 km while Dar-es-Salaa to Lusaka 1,947 km! See the big difference.

Enzi hizo Dar-es-Salaam ilikuwa favorable kwa sababu za kiusalama RENEMO rebellions, apartheid in SA, etc. Ila kwa sasa sababu hizo hazipo tena; tunatakiwa kupambana ku-win biashara sio lelemama. Mambo ya urafiki wa Mwl. na KK zilipendwa hizo sidhani kama kuna .dot com (ambao ndio wanatawala sasa) atakuelewa. KK mwenyewe keshamfuata Mwl. juzi!
 
Hii inaweza kujibiwa na reciprocal action, hiyo mizigo ikivuka mpaka kuja tz ichukuliwe na wa tz ktk ratio hiyo hiyo ya wazawa, tazara, na wengineyo
Hakuna mizigo mingi ya kutoka zambia kuja Tz, Kulinganisha na inayokwenda, wakisema hivyo mbona zambia watafurahi sana!!
 
... kaka muogope Muumba! Zambia ina option ya kutumia bandari za Dar-es-Salaa au Beira, Msumbiji. Lets assume destination ni Lusaka. Tofauti ya umbali Beira - Lusaka compared to Dar-es-Salaam to Lusaka ni 1,095km. Iko hivi; Beira - Lusaka = 852 km while Dar-es-Salaa to Lusaka 1,947 km! See the big difference.

Enzi hizo Dar-es-Salaam ilikuwa favorable kwa sababu za kiusalama RENEMO rebellions, apartheid in SA, etc. Ila kwa sasa sababu hizo hazipo tena; tunatakiwa kupambana ku-win biashara sio lelemama. Mambo ya urafiki wa Mwl. na KK zilipendwa hizo sidhani kama kuna .dot com (ambao ndio wanatawala sasa) atakuelewa. KK mwenyewe keshamfuata Mwl. juzi!

Zambia ni kubwa, inategemea mzigo utafikia wapi. Kama kaskazini inaweza kutumia Dar, kama ni Kusini Beira. Lkn changamoto ya Beira ni milima. Kama umewahi safiri nchi hizi kwa barabara,utanielewa.
 
Zambia ni kubwa, inategemea mzigo utafikia wapi. Kama kaskazini inaweza kutumia Dar, kama ni Kusini Beira. Lkn changamoto ya Beira ni milima. Kama umewahi safiri nchi hizi kwa barabara,utanielewa.
... ndio maana nikatumia Capital City Lusaka kama destination na, in fact, mizigo mingi ya Zambia destination ni Lusaka ambayo iko far south from Tz border; it is closer to Zimbabwe hence Beira kuliko Dar. Sema disadvantage itabidi wapitie "nchi ya tatu" (Zimbabwe) wakati kwa Dar-es-Salaam hakuna nchi nyingine in-between.
 
tuanze kulia na serikali yetu nayo ianze kuweka sheria kandamizi kwa wageni na sheria rafiki kwa wazawa...
Kabla ya kufika huko Busara ya mazungumzo ifanyike Kwanza,pia kufanya evaluation za faida na hasara za kuchukua hatua hizo,Wadau pia washirikishwe.
 
Back
Top Bottom