Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 329
- 874
ZAMA ZAKO ZIKIPITA KUBALI KUACHIA WENYE ZAMA ZAO WAFURAHIE😊
Mambo uliyotakiwa ufanye ukiwa na miaka 10 ukiyafanya leo una miaka 30 Utaonekana kituko 😊
Na usipokubali umri wako ukaanza kujirudisha nyuma kwa kufanya mambo ya kupingana na umri wako pia utaonekana kituko na kibaya zaidi utakuwa unapoteza muda.
Umri ukikupita huwezi kuurudisha nyumba bali ukubali tu kuwa sasa unatakiwa ufanye mambo ya kuendana na umru husika kwa mfano ukiwa na miaka 45 akili kubwa ifikirie utaishije uzeeni kipindi ambacho utakuwa na nguvu ya kula ila huna nguvu ya kufanya kazi.
Umri ni kama zama tu zikipita ndio basi tena kubali kuhamia kwenye zama nyingine na usianze kuona wivu kwa walio kwenye zama zao.
Kuna ambao umri bado unawaruhusu kufanya mambo fulani na kuna wengine tayari umri umeshakuwa kikwazo ila unaweza kulazimisha tu uonekane kituko na mtu wa ajabu mwenye kupoteza muda .
Kubali tu kuwa sasa wewe wa miaka 40 siyo yule tena wa miaka 20 na ukiweza hilo utafurahia sana maisha 😊
#Mwanasayansi Saul kalivubha
#fikia ndoto zako.