Zaidi ya watumiaji Billion 2 wa Google Chrome wapo hatarini data zao kukusanywa sana mitandaoni

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,034
20,370
Browser ya kuperuzi ya Google chrome inatumika na zaidi ya watumiaji Bilioni 2 ambao wanaitumia sana. Hivi karibuni kuna kesi inaendelea baada ya tetesi kuonyesha zaidi ya Watumiaji Bilioni 2 wa Google Chrome wapo katika hatari ya data zao kukusanywa sana mitandaoni kutokana na baadhi ya madhaifu ambayo yapo katika browser ya chrome.

Microsoft imeweka mfumo wa kutoa onyo kuhusu Usalama na Uhakika wa Chrome, pale watumiaji wa Windows wakipakua app ya Chrome. Microsoft imeamua kuwa wazi na kupambana kuzuia watumiaji wa Windows kutumia Google Chrome.

Mwaka huu chrome imepata hack nyingi kuliko kipindi chote. Ni kwa sababu bado kuna madhaifu mengi GOOGLE imeacha katika chrome ili kulinda mfumo wake wa matangazo na kukusanya data.

Issue kubwa inayoendelea: Browser nyingi kama vile Mozilla, Safari, Brave na Opera zimeweka mfumo mpya wa kuzuia Websites kusoma cookies za website nyingine, mfumo wa kuzuia trackers, Third-Party tracking, na mfumo wa AI ya kuweka usiri wa mtu anachoperuzi kwa mfumo wa encryption.

GOOGLE peke yake ndio ameacha madhaifu hayo japo browser yake inaongoza kwa kuwa na watumiaji wengi duniani na kila mwaka wanaongezeka, lakini bado hakuna maboresho ya kiusalama.
 
Du na ndo nimemaliza kulidownload kwenye Mx-Linux yangu kumbe kimeo. Ninacholipendea lina heap size kubwa unapodownload file kubwa kutoka kule Mega.


Sent from my cupboard using mug
 
Nadhani hii ni vita tu ya kibiashara kati ya hawa tech giants.. Microsoft wanalenga kuipromote browser yao ya Edge baada ya Microsoft Internet Explorer kufail kwny market.

Sisi wengine tukae kwa kutulia huko hatuna hata app ya calculations ya magazijuto WTFFF

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Du na ndo nimemaliza kulidownload kwenye Mx-Linux yangu kumbe kimeo. Ninacholipendea lina heap size kubwa unapodownload file kubwa kutoka kule Mega.


Sent from my cupboard using mug
Kweli ila mara nyingi hivi vitu vimetengenezwa kulenga watu fulani.
Hivyo kwa target yao watu wengine kama sisi sizani kama tutaathirika Zaidi.
 
Nadhani hii ni vita tu ya kibiashara kati ya hawa tech giants.. Microsoft wanalenga kuipromote browser yao ya Edge baada ya Microsoft Internet Explorer kufail kwny market..
Sisi wengine tukae kwa kutulia huko hatuna hata app ya calculations ya magazijuto WTFFF

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
Kweli sisi si waathirika wa hii kitu hapo ni wao wanapambana katika masoko hivyo ni kuchafuana kwa namna waijuao wao.
 
Kisheria site nyingi inabidi ukiingia ukwambia ikuulize kama utaruhusu cookies na kwa kiasi gani ili your browsing iwe na ufanisi...

All in all huwezi kuweka kitu out there alafu ukadhani upo safe 100% ni vema kufahamu tu anything digitally which is out there can be hacked kwahio ni wewe binafsi kutumia njia tofauti au third party programs kupunguza makali..., pia unaweza ukawa unafanya vitu incognito na sio kushare information zako za siri kwa uwazi sana (Hakuna Siri ya Watu wawili....)

Sasa wewe kama unaweza akaunti yako yenye trillion kadhaa laid bare au financial information nje nje au mnapanga kupindua nchi kwa kutumia email sijui unategemea nini
 
Kisheria site nyingi inabidi ukiingia ukwambia ikuulize kama utaruhusu cookies na kwa kiasi gani ili your browsing iwe na ufanisi.....
Kweli vitu confidential haipaswi kushirikiwa kwa kutumia hizi digital maana si sehemu salama.
 
Muhimu ni kutumia third party password manager.

Kuachana na hizi password manager za browsers.

Atleast password ziwe safe.
 
Chrome wkt mwengine ukiifungua unakuta message za ajabu ajabu mfano za madada wa pornography wanakuhamasisha uclick ..
 
Back
Top Bottom