Zaidi ya Nusu ya Watanzania Watakuwa Wanaishi Mijini Ifikapo Mwaka 2050

May 14, 2024
80
63
Tanzania inaungana na Umoja wa Mataifa katika utekelezaji wa lengo la 11 la Maendeleo Endelevu kwa kuhakikisha Maendeleo ya Makazi na Jamii zinakuwa salama, jumuishi, stahimilivu na endelevu huku ikikadiriwa zaidi ya nusu ya watu wake watakuwa wanaishi mijini ifikapo mwaka 2050.


Akiwasilisha taarifa ya Tanzania katika kikao cha 12 cha Kongamano la Miji Duniani (WUF) linalofanyika katika jiji la Cairo nchini Misri kuanzia Novemba 4 hadi 8, 2024 kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo, Bi. Lucy Kabyemera amesema Tanzania inafahamu changamoto ya ongezeko la watu mijini na ukuaji wa miji unaoendelea kwa kasi kubwa barani Afrika.

Amesema, Tanzania kama nchi nyingine zinazoendelea, inakumbwa na ongezeko la watu mijini kwa kiwango kikubwa, ambapo ongezeko hilo linakadiriwa kuwa asilimia 4.8 kwa mwaka huku asilimia 35 ya watu milioni 61.7 wakiishi katika maeneo ya mijini.

“Mabadiliko haya yameathiri kwa kiasi kikubwa njia za maisha, kazi, usafiri na mawasiliano. Hali hii inaleta changamoto katika mgawanyo na upatikanaji wa rasilimali, kuanzia makazi, usafiri, huduma za afya, elimu na fursa za ajira ambazo zote zinategemea mahali watu wanapoishi” amesema Naibu Katibu Mkuu Kabyemera.

Katika kukabiliana na hali hiyo, Tanzania imejizatiti katika kufanya mageuzi katika sekta ya makazi hatua inayosaidia kupunguza mifumo ya uzalishaji wa hewa ukaa, mifumo ya usimamizi wa mafuriko, kubuni miji yenye kupunguza matumizi ya nishati na ukijani na kutumia teknolojia na huduma za nishati safi ili kukabiliana na ongezeko hilo la miji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuwa kinara katika kukabiliana na hali hiyo kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuhakikisha nishati inapatikana na kuwa endelevu kwa wote.

Nishati safi ya kupikia ni suala la dharura na ni kipaumbele kwa Tanzania, ndiyo maana Tanzania imezindua Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia wa Mwaka 2024-2034 ili kukabiliana na kasi ya ukuaji wa miji na kuongezeka kwa mahitaji ya nishati inayotumika katika miji mbalimbali nchini kwa maendeleo endelevu kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Kongamano la Miji Duniani huitishwa na Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-Habitat) kila baada ya miaka miwili (2) kama kongamano kuu la kimataifa kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa changamoto za miji na kuweka mikakati ya pamoja kuboresha miji. Jukwaa hilo limeanzishwa zaidi ya miaka 20 mjini Nairobi, Kenya mwaka wa 2002 na kuhudhuria na wawakilishi wa Serikali za kitaifa, kikanda na serikali za mitaa, wasomi, wafanyabiashara, viongozi katika jamii, wapangaji miji na wawakilishi wa mashirika ya kiraia. Kwa mwaka huu ni mara ya pili Jukwaa hili linafanyika katika Bara la Afrika likiwa na kauli mbiu isemayo mambo yote yanaanzia nyumbani.
 
Wahamie mjini kwa miundombinu ipi? Mwaka 2050 ni miaka 25 kutaka sasa, jiji la dar lenye watu 3.5 mpaka leo halina maji safi na salama maeneo mengi, ndo usema ndani ya miaka 25 litaweza kilea tuseme watu 15m......
 
Back
Top Bottom