Yesu Kristo aliuawa kwa sababu za kisiasa zaidi kuliko za kidini

King Octavian

JF-Expert Member
Oct 1, 2011
403
351
Si lengo wala dhamira yangu kupinga wala kupindisha Imani ya mtu yeyote, bali ni wajibu wangu kama binadamu mwenye akili na upeo wa kudadisi, kuchanganua na kuyaelewa mambo mbalimbali katika namna tofauti tofauti.

Biblia ni kitabu kama vilivyo vitabu vingine vyenye maarifa, tamaduni na vinavyoelezea hisia za jamii za watu wake, isipokua Biblia ni kitabu maarufu kuliko kitabu chochote kilichowahi kuandikwa katika taaluma ya uandishi hapa Duniani.

Uchambuzi wangu utajikita zaidi katika kuelezea kifo cha Yesu Kristo ambaye historia kupitia vitabu mbalimbali vinavyounda kitabu kikuu cha biblia inatueleza kuwa ndiye chanzo cha Dini ya kikisto au kwa lugha ya kigeni dini hiyo inajulikana kama CHRISTIAN yenye tafsiri ya Wafuasi wa Yesu Kristo.

Historia kutoka katika vitabu vya MATHAYO na LUKA inatuambia kua Yesu Kristo alikua MYAHUDI na alizaliwa sehemu ijulikanayo kama BETHLEHEM katika jimbo la JUDEA. Wakati huo sehem kubwa ya Dunia ilikua inatawaliwa na kumilikiwa na UTAWALA WA FALME YA KIRUMI (ROMAN EMPIRE).

Warumi au Waroma walitawala Kwa muda mrefu sana karibu sehem yote ya dunia chini ya wafalme mbalimbali waliofahamika kama KAISARI (CAESAR).

Katika kila jimbo la utawala wa kirumi, likiwemo jimbo alimozaliwa Yesu la JUDEA aliwekwa mtawala na msimamizi mkuu wa serikali ya kirumi, aliyefahamika kwa cheo cha GAVANA. Kipindi cha Yesu Kristo, Gavana wa JUDEA alijulikana kwa jina la PONTIAS PILATE (PONSIO PILATO)', na alikua chini ya Mfalme wa Roma aliyejulikana kama (TIBERIUS CAESAR).

Kazi kubwa ya kwanza ya Gavana wa Roma katika jimbo ilikua ni kulilinda jimbo na utawala wa kiroma kwa nguvu za kijeshi, na ndio maana kila gavana alipewa wanajeshi wasiopungua 3000 kwa kazi hiyo. Kama mwakilishi wa utawala wa kiroma kazi yake nyingine ilikua ni kuhakikisha anakusanya KODI pamoja na kutoa hukumu(mahakama) katika makosa mbalimbali kwa mujibu wa sheria za kiroma.

utawala wa kiroma pia uliwatumia wenyeji wa maeneo wanayoyashikilia katika utawala, hasa katika utawala wa ngazi za chini au serikali za mitaa, waliyatumia makabila mbalimbali, au viongozi wa Dini inayotawala sehemu hiyo. Mfano katika jimbo la Judea na Jerusalem lilikuwepo baraza la Makuhani au Walimu na Viongozi wa dini, baraza hilo lilijulikana kama SANHEDRIN Kwa lugha ya kiyahudi.

SANHEDRIN ni nini?
Historia inatuambia kuwa Waislael waliamriwa na Mungu kuanzisha mahakama ya majaji na mahakimu ambao walipewa mamlaka ya kuwahukumu waisrael wanapokwenda kinyume na matakwa ya Mungu wao kwa mujibu wa sheria walizopewa na Mungu wao. Majaji hao wote walikua ni wale Viongozi wa Dini pamoja na Walimu wa Dini.

Kiongozi mkuu wa kidini (KUHANI MKUU) au kiongozi wa baraza la SANHEDRIN katika jimbo la Judea aliitwa CAIPHAS (KAYAFA). Viongozi wote hawa wa kiyahudi kama historia inavyotuambia walikua chini ya utawala wa Kiroma na walifanya shughuli zao kwa umakini na uwoga pasipo kuitilafiana na watawala wao WARUMI. Na moja ya jukumu lao ilikua ni kuhakikisha haitokei vurugu ya aina yoyote miongoni mwa WAYAHUDI wala mtu anayepingana na utawala wa kirumi, ama sivyo PILATO aliwatishia kuwa atalifunga hekalu lao la kuabudia.

Utawala wa warumi ulikuwa ni wa kibabe na kimabavu sana kiasi kwamba watu walikua wameuchoka na walikua wakisubir siku moja atokee mtu awaokoe katika utawala huo, kwani walichoka kulipa kodi, kuuliwa hovyo na pia kutumikishwa kwa kazi ngumu na utawala huo warumi, kifupi ni kwamba walichoka kutawaliwa.

Yesu Kristo alipoingia Jerusalem, alifanya matukio ambayo yaliwashtua watawala wa mji huo hasa MAFARISAYO au Makuhani, na kuona kua ujio wake unatishia utawala wao na vilevile waliogopa kwamba Yesu Kristo anaweza kuwa chanzo cha vurugu zilizokatazwa na PONSIO PILATO.

Moja ya tukio alilolifanya Yesu lilikua lile la kuvamia hekalu na kuanza kumwaga mwaga bidhaa pamoja na fedha za wafanyabiashara waliokuwemo humo, kitendo hicho kiliamsha shangwe na vigelegele miongoni mwa wayahudi wakimuona kama mkombozi wao katika utumwa huo wa kiroma. Pia Yesu aliongea maneno yaliyoamsha maswali, maneno yaliyoashiria Mapinduzi ya kiutawala. Yesu alisema; mathayo 24:2.

"Sawa, mnaweza kuyatazama haya yote! Kweli nawaambieni, hakuna hata jiwe moja litakalosalia hapa juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa."

Wafarisayo hao waliona kua huo ni mpango wa kuangusha utawala wao na hivyo wakakubaliana kua Yesu lazima adhibitiwe haraka iwezekanavyo. Na ndio maana hata CIAPHAS (KAYAFA) aliamuru kuwa Yesu akamatwe na ahukumiwe haraka usiku kwa usiku, tena usiku wa manane jambo lililovunja sheria za kiyahudi (JEWISH LAWS) zilizoelekeza hukumu zote kutolewa mchana kweupe tena mbele ya umati wa watu.

Yesu alipokamtwa mwanzoni alituhumiwa kwa kosa la Kupotosha imani ya Dini na Mungu wao kwa maana nyingine alikua ANAKUFURU (BLASPHEMY) kitendo cha Yesu kujitangaza kua.yeye ni mwana wa Mungu na Tayari Maandiko yote waliyoyasubir wayahudi hao kayatimiza ilionekana kua KUFURU kwao, hivyo viongozi hao wa dini waliona wamuadabishe yesu.

Lakini kutokana na kwamba wao hawana mamlaka ya kutoa hukumu bali mwenye mamlaka hayo alikua ni PONTIAS PILATE, iliwaradhimu wampeleke Yesu kwa Pilato. Lakini wazee hao wa baraza la SANHEDRIN walipofika kwa Pilato Walizibadirisha tuhuma na wakamtuhumu Yesu kwamba anachochea mapinduzi ya serikali ya kirumi kwa kuwakataza watu wasilipe kodi kwa KAIZARI na vile vile anajiita MFALME, Jambo ambalo kwa mujibu wa sheria za Roma ilikua ni Uhaini (TREASON). Hii ni kwa mujibu wa kitabu cha LUKA.

Yesu alimshawishi ZACCHAEUS (ZAKAYO MTOZA USHURU)wa mji wa YERICHO ambae alikua Mkuu wa Watoza ushuru, aache kazi ya kutoza ushuru na amfuate, Yericho, ni mji uliokua ndani ya eneo la ukusanyaji kodi la Pilato. (Luka 19:2-19)

KWA NINI PONTIAS PILATE (PONSIO PILATO) ALIMUHUKUMU YESU JAPO HAKUMKUTA NA KOSA KWA MUJIBU WA SHERIA ZA KIROMA?

Historia inatuambia kua Pilato alipingana na maelezo ya makuhani na kuyaona kuwa hayana uzito wa adhabu wanayopendekeza Yesu apewe. Alitaka kulithibitisha hilo kwa kumuuliza Yesu maswali ambayo lengo lake ni kuona kama kweli Yesu ni Tishio kwa utawala wa Kirumi. Pilato alimuuliza Yesu,

"Wewe ni mfalme wa Wayahudi?" Yesu akamjibu hayo umetamka wewe.
Pilato aliwarudia makuhani na kuwawmbia

Simuoni mtu huyu kua na tuhuma. Makuhani wakamjibu, lakini amevunja sheria, pilato akawaambia, amevunja sheria zenu sio sheria za kaisari.

Pilato alitoa hukumu ya yesu kuteswa mpaka kufa kwa woga wa kutokea vurugu zitakazompelekea kushindwa kutawala, kwani Aliwaza kua kama hatatoa hukumu hiyo kwa Yesu CAIPHAS atampa lawama zote endapo yatatokea machafuko na vurugu ndani ya jimbo lake la utawala. Vile vile aliogopa kuwajibishwa na KAIZARI endapo vurugu zingetokea, angeonekana ameshindwa kutawala.

Yesu alihukumia Kifo (Death Penalty).
Ukichunguza uchambuzi katika maelezo hayo utaona kuwa kulikua na mvutano wa kisiasa katika uongozi wa nani anakubalika zaidi na nani anataka kumpindua nani. Makuhani pamoja na Wazee wa baraza walitishwa kuwa Yesu kaja kuharibu utawala wao na labda walikua wanapata maslahi zaidi kutoka katika utawala wa kirumi hivyo ujio wa Yesu ulikuja kutiachanga katika kitumbua chao.

Upande wa Pilato japo alidai kua hausiki na mauaji ya Yesu kwa kunawa mikono kwa maji kuashiria kua Umwagaji Damu wa Yesu hausiki nao, alisema

"Sina hatia na damu ya mtu huyu, jambo hili ni juu yenu ""

lakini tamaa ya Madaraka ilimsukuma kutoa hukumu hiyo, uwezekano wa yeye kupinga tuhumu na kuamuru Yesu aachiwe huru ulikua mkubwa na ulikua ndani ya uwezo wake kwa sababu Gavana wa kirume kwa kipindi chao alikua yeye ndiye sheria na yeye ndiye mahakama muamuzi wa mwisho. Lakini alihisi kama angefanya hivyo ingekua mwisho wa utawala wake.

Asanteni kwa Kusoma maandishi haya.
(sept.2016)
 
Naomba ufafanuzi kwa mujibu wa hii stori
1 Warumi walikuwa na dini gani kabla ya kuja Yesu?
2 Wayahudi dini waliokuwa wakiifata ililetwa na nabii yupi?
3 Ikiwa Yesu alikwenda kumwaga pesa ya sadaka kwenye HEKALU na WAYAHUDI waliingiwa na wasiwasi wa utawala wa dini yao kwanini isiwe shutuma ya dini na iwe siasa?
4 Mahakama ilio mhukumu Yesu ilikuwa ya dini ya (Wayahudi) au ya siasa(Kirumi)
 

Najibu kutokana na ninavo jua mimi na nilivo soma

1. Warumi walikuwa waki sali miungu mbali mbali, kama mungu jua, mungu neptune, na jamii nyingi za ulaya ziligawanyika katika kuamini miungu
2. Wayahudi mpaka leo wana mfahamu nabii MUSA tuu, na Yesu kwao alikuwa ni mtoto wa fundi serelemala aliye dai kuwa yeye ni Mungu, ki fupi kwao wana amini Messiah bado hajaja na wanatumia zaidi vitabu vya taurat.
4. Ilikuwa ni ya warumi, hata adhabu ya Msalaba ni adhabu iliyo tumiwa na warumi zaidi na si wayahudi.

*Marekebisho yana ruhusiwa
 
Hii nilishawahi kusikia zaidi nikasema nitapata wapi vitabu au nakala za mambo haya ya kale.
Kitu kimoja,mambo yanayotokea siku hizi za leo hayatofautiani sana na mambo ya miaka 2000 iliyopita.
Its the same human being we talking about.
 
Marekebisho katika swali no. 3 maelezo hayajasema Yesu alimwaga pesa za sadaka
 
Pilato alipomuuliza Yesu kuwa 'je wew ndiye mfalme wa wayahudi? ' Yesu alijibu ndio mim ndiye "
 
Ahsante mkuu kwa majibu yako. lakini umenifanya nikuulize tena hii namba 2 na 4.
1 Ikiwa Wayahudi wanamjua Mussa tu mbona kwenye vitabu vya dini vinasema manabii wengi ni Wayahudi?
2 Unasema wametumia adhabu ya msalaba kutokana hio ndio adhabu ya Kirumi, kwahio msalaba ni alama ya Kirumi na sio ya kikristo? ikiwa ndio kwanini sasa iwe alama kuu inayotumika kwenye dini ya kikristo?
 

Anhaa, sikumaanisha hawa manabii hawa watambui, kuna watu kama kina Abraham, Isaya, kina Samweli, wana watambua lakini pia wanahistoria wana dai hili neno lilikuwa lina tumika 'loosely' kwa watu wengine pia ambao ni manabii wadogo wadogo ambao inadhania wanafika hata 60 wanao julikana tuu.
Lakini Moses anatambulika kwa kuwa ndio nabii wa kwanza kabisa kupata kuwepo, na ndiye mwandishi wa Sheria zoote za kiyahudi yaani torati, kwa hiyo hawa wengne wana tambulika ila hawapewi sifa kama za moses.

Msalaba hutumika kuonesha mateso ya Yesu na kuwakumbusha wa kristo kuwa aliteswa kwa ajili yao, halafu pia

Warumi ni taifa au kabila(race) lakini ukristo ni dini (religion) hivo hakukuwa na shida kutumia alama hiyo alama.

Nime jibu kwa haraka lakini ntafuatilia zaidi maswali yako.

*likiwepo la ziada ntatoa maelezo, japo si expert wa haya mambo ndugu
* nilipokosea ntakubali kusahihishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…