Yericko Nyerere mshauri Mbowe vyanzo vipya vya mapato mjenge hata choo cha chama, ACT wamewazidi, Dkt Mwigulu sio level yenu

zanku

Member
Jun 9, 2020
70
152
YERICKO NYERERE, KISHAURI CHAMA CHENU KIJENGE HATA OFISI, MAMBO YA NCHI HUYAWEZI

Na Mzabibu Mwitu


Nimeona andiko la Kamanda wa Chadema, Yericko Nyerere akimnanga Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba na Serikali ya CCM kwa ujumla, katika makala hiyo Yericko kama kawaida yake amejaribu kutaka kujionesha kuwa smart kichwani lakini mwishoni kaishia kutoa boko.

Umekuwa mstari wa mbele kujaribu kujibrand kuwa mchambuzi makini na intelligence jambo ambalo hujafikia hata 10%.

Natambua wewe ni mwanamkakati wa propaganda ndani ya chama chenu na umekuwa ukiandika mfulululizo wa maandiko ya kumshambulia Dkt Mwigulu Nchemba juu ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali, haya yote unafanya Ili kutimiza wajibu wako ndani ya chama chenu wala huandiki kwa maslahi ya nchi, acha kujifanya una uchungu, tunaokujua tunajua biashara zako zimedoda, biashara ya bamia na ile ya ukanjanja wako wa ku-copy vitabu vya watu ili uje uwadanganye nyumbu wenzio umeandika wewe zote zina hali mbaya, kazi pekee uliyobaki nayo ni hii ya kuandika propaganda kumfurahisha Freeman Mbowe ambae ndie mwanzilishi wa hii ajenda yenu ya kihuni.

Nirudi kwenye mada, Ulichoandika kwa asilimia hujatumia akili kufikiri, hivi unajua makampuni ya simu yanakata Tshs ngapi kwa kila Mtanzania kwenye kila laini? Umewahi kulalamika? Hivi hivyo vyanzo ulivyotaja una unahisi ndani ya system ya nchi hii havijawahi kuwazwa? Acha kutumia tumbo kufikiri kamanda.

Dkt Mwigulu Nchemba kawaza vyema sana juu ya utozaji huu mpya wa kodi na ndio mfumo mpya Duniani kote, nenda nchi zote zilizoendelea kuanzia South Africa na kwingineko Mitandao ya simu ndio chanzo kipya cha mapato kwa sababu Dunia imeamia huko, huwezi kutoza kodi sehemu ambayo haina mzunguko mkubwa wa fedha, huwezi kuacha makampuni ya simu yajitajirishe ilhali sisi kama nchi tukiendelea kwa mikopo yenye riba kuwa, binafsi naunga mkono tozo kwa asilimia kwa sababu matokeo yake yanaonekana.

Kamanda ebu tumia intelijensia yako kumshauri Mbowe atumie michango ya Join the Chain na malipo ya E-card ya Chadema digital walau kujenga hata kachoo ka shimo hapo makao makuu yenu, hivi chama cha miaka mingi hivyo kinazidiwa na ACT Wazalendo ambao wamejenga ukumbi na ofisi na vikao vyako vinafanyika humo! Nyie kutwa kukodi maukumbi, hivi mnapata wapi moral authority ya kuhoji watu wenye vision wanapofanya positive changes ambayo hata nyie kuthubu tu mmeshindwa? Oneni aibu bhana.

Serikali iendelee kutoza kodi mahali penye mzunguko mkubwa bila kujali kelele za vyura wajinga, hii nchi lazima iendelee mbele lakini bila mapato itakuwa ni kazi bure, tunayo miradi mingi ya kumalizia kama nchi, tunayo madeni ya kulipa, tunao wanafunzi wa kupeleka shule na mambo kedekede hivyo Tozo haziepukiki.

Nchi nyingi Duniani zinazoendelea zimeweka kodi, Tozo na levy mbalimbali kwenye transactions zote za kidigital kwa sababu Dunia imeelekea huko.
Mfani ni huu:

Kenya


Ghana




Hapo juu nimeweka link mbalimbali zikionesha ni namna gani nchi mbalimbali zinatumia population iliyoko kwenye mitandao na kampuni za mawasiliano kutoza kodi, jambo la kulipa kodi siku zote halipendwi hasa kwa vyama vya upinzani kwa sababu vinatambua Serikali ya chama tawala itafanya development na kusababisha kupunguza ukosoaji, nakupa moyo kaka yangu Mwigulu Nchemba Songa mbele, wengi tumekaa kimya kwasababu tunajua uwezo wako wa kutoteteleshwa na kelele za chura, tunajua Nia Yako ni njema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom