Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,126
- 151,484
Huyu bwana ni mtu ambae hatazami wala hawazi kuwa katika maisha kuna leo na kesho, na pia hawazi kuwa cheo ni dhamana na kwamba madaraka aliyonayo ipo siku atayaacha apende asipende.
Bwana huyu anasahau kuwa kabla yake walikuwepo wengine ambao walikalia kitu hicho kwa zamu kabla ya yeye kupata hiyo nafasi tena kwa zali la mentali!!
Ukimtazama bwana huyu kwa jicho la tatu,utagindua ana viashiria vyote ya kutaka kukali kiti hicho kwa muda mrefu kama ilivyo kwa marafiki zake wakubwa ambao wamekaa katika nafasi hizo kwa miaka mingi(miongo kadhaa).
Hata hivyo,kabla ya kufanikisha hili,ni lazima aonyeshe kuwa yeye ni zaidi ya wenzake waliomtangulia na hivyo kuna kila sababu ya kumuongezea muda( kwa maneno mengine,anatafuta justification ya kubaki hapo alipo).
Asilolifahamu bwana huyu ni kuwa,njia na mbinu anazotumia haziwezi kumsaidia kutimiza azma yake badala yake zinaweza kumfanya aishie njiani kwani anataka kutimiza azima yake kwa kukanyaga na kuvunjavunja kila mtu anaetaka kuwa kikwazo kwake(awe ndani ya chama chake au nje ya chama chake) bila kujua anatengeneza maadui ambao mmoja wa hao maadui ndio anaeweza kuja kuwa mrithi wake siku za baadae kupitia chama chake au vinginevyo.
Kabla sijaendelea zaidi,naomba niseme kuwa,hata watangulizi wake hawawezi kuukubali huu mpango wake kwani kama wao waliondoka wakati walipotakiwa kuondoka,kwanini yeye atake kufanya kinyume chake?Kitachofuata ni watu kuungana kutoka pande zote huku wakitumia njia sahihi na halali kumpumzisha.
Hata hivyo,busara na uvumilivu vikikosekana, tunaweza kuona tunayoyaona kwingineko.
Kwahiyo,hawa watangulizi wake ndio watakuwa sehemu ya kundi la kumpinga ama waziwazi au chini kwa chini na kwa hakika hatafurukuta(atashindana lakini hatashinda).
Matokeo ya hali hii ni huyu bwana kuja kuondoka ofisini kwa aibu(kwa kukataliwa na wenzake ndani ya chama na hata nje ya chama chake) huku akiwa amejeruhiwi wengi na yoyote atakaemrithi atakuwa teyari ana kinyongo nae na hivyo unaweza kuandaliwa mpango wa kumshughulikia na katika kumshughulikia,yafuatayo yanaweza kuja kutokea.
1.Watakuja kumfilisi mali zake kama sio kuzitaifisha
2.Tuhuma zake nyingi zitawekwa hadharani
3.Wateule na wapambe wake wengi watashughulikiwa,n.k.
NB:
Haya niyasemayo yanaweza yasitokee kwa sasa(yakashindwa kutimia kwani yanahitaji muda na maandalizi) na hivyo akafanikisha azima yake hiyo ila upinzani dhidi yake utaongezeka kwani watu hawatapenda na hivyo haya niyasemayo yanaweza pia kuja kutokea akiwa teyari amejiongezea muda wa kukaa ofisini yaani huko mbeleni.
Mwisho,Mzee wangu huyu aelewe tu,waliochagua kukaa kimya huku moyoni hawaridhiki,ndio wanaweza kuwa wabaya kuliko hawa wanaosema ya moyoni.