Breaking News!!!
YAMETIMIA! Katika kile kinachoendelea kuthibitika kwamba mechi zinazowakutanisha wapinzani wa soka la Bongo, Simba na Yanga ndizo zinazoamua hatma ya makocha wa vilabu hivyo vikongwe hapa nchini.
Hatimaye klabu ya Yanga leo hii imesitisha mkataba wa ajira na kocha wake George Lwandamina waliyemleta wiki chache zilizopita kutoka nchini Zambia, baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa matokeo ya klabu hiyo katika mechi za hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na na kile kinachoelezwa kwamba kukosa maelewano mazuri na baadhi ya wachezaji nyota wa klabu hiyo.
Hivyo kuanzia leo hii kocha msaidizi Juma Mwambusi ataendelea kuliongoza benchi la ufundi la klabu hiyo chini ya Mkurugenzi wa Ufundi Hans van Pluijm, huku uongozi wa klabu ukifanya jitihada za haraka kusaka kocha mkuu wa klabu hiyo kutoka nje ya nchi atakayeziba nafasi ya Lwandamina aliyetimuliwa leo asubuhi.
Na taarifa zilizotufikia hivi punde kocha kutoka nchini Madagascar ametua asubuhi hii kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, ili kukamilisha mazungumzo na uongozi wa Yanga ya kuingia kandarasi ya kuifundisha klabu hiyo kama kocha mkuu.
Kocha huyo anayefahamika kwa jina la Germana Jennaise ametua akiwa pamoja na wakala wake.