Yanga inatarajiwa kuondoka kesho kwa ndege kwenda mkoani Kagera wakipitia Mwanza kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera.
Yanga inaondoka ikiwa inawaacha jijini Dar es Salaam wachezaji vijana walio katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana na wakongwe wawili, Thabani Kamusoko na Donald Ngoma.
Wazimbabwe hao wawili wote ni majeruhi na watabaki jijini Dar es Salaam kuendelea kupata matibabu.
Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amesema basi la Yanga limetangulia likiwa na viongozi wakati wachezaji wataondoka kesho.
Salehe Jembe