- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Salaam Wakuu,
Nimekutana na Taarifa kutokea Twitter ya Privadinho ikikanusha taarifa zinazoelezea sakata la Yanga kufungiwa kusajili sababu ya kushindwa kulipa deni ya Bechem United. Tazama hapa chini.
Nimekutana na Taarifa kutokea Twitter ya Privadinho ikikanusha taarifa zinazoelezea sakata la Yanga kufungiwa kusajili sababu ya kushindwa kulipa deni ya Bechem United. Tazama hapa chini.
- Tunachokijua
- Yanga ni kifupi cha Young Africans Sports Club, ambacho ni klabu maarufu ya soka kutoka Tanzania. Klabu hii ilianzishwa mwaka 1935 na ina makao yake makuu jijini Dar es Salaam. Yanga ni moja ya klabu kongwe na yenye mafanikio makubwa katika historia ya soka Tanzania, ikiwa na mashabiki wengi na rekodi nzuri kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa.
Wanachama na mashabiki wa klabu hii mara nyingi hujulikana kama Wanajangwani au Wananchi, na rangi zao za jadi ni kijani na njano.
Mnamo Desemba 5, 2024 Waandishi wa habari za michezo wa Tanzania na nje Mataifa mengine wametoa Taarifa iliyoambatana na barua ikieleza kuwa Shirikisho la soka Duniani (FIFA) wameifungia Klabu ya Yanga sababu kushindwa kulipa madai waliyoamriwa ambayo FIFA iliiamuru Yanga kuilipa Klabu ya Bechem United, baadhi ya taarifa hizo ni hizi hapa, hapa na hapa (kwa kuzitaja chache).
Siku moja baada ya kutokea kwa taarifa hiyo (Desemba 6, 2024) mmoja wa Maafisa habari wa Klabu ya Yanga kitengo cha Dijitali anayejulikana zaidi wa jina la Privadinho kupitia ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa X aliibuka na kukanusha Taarifa hiyo kwa madai kuwa ni propaganda. Kanuho hilo la Privadinho limehifadhiwa hapa. Sehemu ya kanusho hilo Privadinho aliandika:
Ndugu propaganda za Yanga kufungiwa ni utoto kama utoto mwingine. Hii ni zaidi ya mara tatu mna copy taarifa huyu Bumunda Micky. Upi uhalisia wa madai hayo?
JamiiCheck imepitia kurasa rasmi za FIFA na kubaini kuwa Taarifa ya Shirikisho hilo kuifungia Klabu ya Yanga madai yao kutokea Klabu ya Bechem United ni ya kweli.
Upitiaji wa JamiiCheck katika ukurasa huo umekutana na Barua iliyowekwa siku ya Desemba 5, 2024 ambapo FIFA ilieleza Kuifungia klabu ya Yanga kufanya usajili wa Wachezaji wapya mpaka watakapokamilisha kulipa deni la dola 80,000 (Tsh Milioni 216) wanalodaiwa na Klabu ya Bechem United kama ada ya usajili wa mchezaji Augustine Okrah.
Kwanini Yanga wamepata kesi hiyo?
Mnamo Agosti 20, 2024 Shirikisho la soka duniani (FIFA) lilitoa siku 40 za kuitaka klabu ya Yanga kuilipa kiasi cha USD 80,000 (Takriban Tsh Milioni 216) klabu ya Bechem United ya nchini Ghana kama pesa ya malipo iliyosalia katika uhamisho wa Augustine Okrah kutoka Bechem United kwenda Yanga. (Taarifa ya kesi hiyo mehifadhiwa hapa)
Hivyo, kesi hii imekuja baada ya Yanga kushindwa kutekeleza agizo hilo hilo la Agosti 20, 2024