Wana jangwani wenzangu timu inatupa raha na kutembea kifua mbele lakini tujiulize kwa ukongwe wa timu yetu tulistahili kupata mafanikio zaidi ya haya.Hakuna mwana yanga asiejua kuwa mafanikio haya ya kucheza kandanda safi yusuf manji ana mchango mkubwa na hatuna budi kumshukuru kwa hili.
Zaidi ya gate collection na pesa ya udhamini wa TBL je club ina vyanzo gani vingine vya mapato kwa mwenye uelewa ningeomba anijuze nina kuwa na shaka na hali hii kwani siku manji akikaa pembeni je hali hii ya furaha itaendelea?khofu yangu ipo hapo na khasa nikitizama majirani zetu hali wanayopitia inanipa shaka.
Najaribu kuwaza kama mikakati madhubuti inakuwepo hata kwa kuuza gazeti la yanga imara walau wanachama na wapenzi wakaeleweshwa kuwa sio unanunua tu khabari bali unakuwa umechangia club muamko huo ukiwepo hata kwa kupata watu laki moja kwa wiki wenye uwezo wa kutoa 500 kununua gazeti kweli chanzo hiki hakifai?
Unaweza kujibu kuwa mbona gazeti lipo miaka mingi?sikatai ile je lipo kimaslahi ya timu au wajanja wachache?maana kwa watu laki takriban kwa mwezi mapato yasingepungua 200m je ndogo hizo?Najihisi vibaya jinsi timu yangu inavyo kuwa na fursa kama hii ya mtaji wa mashabiki kisha I nashindwa kuitumia.Wacha niishie hapa wachangiaji wengine nao wachangie.