Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga, leo wamewapa raha Watanzania baada ya kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Sagrada Esparanca ya Angola katika mchezo wa kwanza wa raundi ya tatu ya Kombe la Shirikisho wakiwania kucheza hatua ya makundi.
Mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imekuwa mwanzo mzuri kabla ya timu hizo kurudiana Mei 18 ambapo Yanga itakuwa inahitaji sare ili kusonga mbele.
Habari zaidi, soma hapa=> Yanga heshima mbele Afrika, Sagrada yalala mara mbili | Fikra Pevu