Live Updates ya majibu ya kura kati ya Trump na Kamala
Rasmi Fox News yatangaza kuwa Donald Trump ameshinda Urais wa Marekani dhidi ya Kamala Harris
Kulingana na kituo cha habari NBC, Donald Trump ameshinda jimbo la Pennyslavania, jimbo ambalo kwenye chaguzi nyingi huamua nani atakuwa Rais wa marekani
================================================================
Taarifa kutoka The Associated Press (AP) kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Marekani zimeanza kuonesha Rais wa zamani, Donald #Trump anaongoza kwa idadi ya Kura ambazo hutumika kuamua mshindi wa Urais (Electoral Votes)
-
Takwimu za awali za Mtandao wa The Associated Press (AP) zinaonesha Trump ana Kura 247 huku Makamu wa Rais, Kamala Harris akiwa na Kura 210, ambapo yeyote kati yao ili awe Mshindi atahitaji kupata Kura 270
-
Aidha, Kura za Wananchi hadi kufikia Saa 1 Asubuhi (EAT), zinaonesha Kamala amepata Kura 61,291,377 (47.4%) na Trump akiongoza tena kwa Kura 66, 074,641 (51.1%), huku Matokeo kamili yakitarajiwa kujulikana kabla ya Saa 3 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki
November 5, 2024 mtanange utapigwa ndani ya USA, hadi sasa dalili zote zinaonyesha itakuwa kati ya Donald Trump (Huyu ashapitishwa na chama chake) na Kamala Harris (Huyu bado hajapitishwa na chama chake)
Binafsi japo nipo Tanzania ila nnahisi mipango yangu ya kuanzisha biashara ndani ya ardhi ya USA inaweza athiriwa endapo kutakuwa na policy changes ikitokea Trump ameshinda.
Hivyo ntaendelea fuatilia kwa karibu mtanange huu hadi mshindi ametangazwa. Ungana nami hapa tupate kujuzana zaidi kuhusu uchaguzi huu.
Pia unaweza piga kura hapo nani unahisi atashinda kwenye uchaguzi huu.