Yaliyotokea Kariakoo ni ukumbusho kuwa Amani hulevya Ujinga

stormryder

JF-Expert Member
Mar 23, 2013
3,610
5,512
Mimi ni mshabiki namba moja wa Israel, ila nimeguswa na tukio la kuanguka kwa Jengo Kariakoo, Jitihada tuliyoweka katika uokozi ni aibu kwetu hasa sisi Watanzania tunaomini sio Nyani.

Gaza kwao kuanguka kwa majengo ni kila siku tena kwa mabomu na sio uzembe, lakini Watu wake na mifumo yao ya uokozi imepunguza Idadi ya vifo hadi 40, 000 pekee, Kama sisi Jengo moja tumetumia siku 2 na bado hatujamaliza, basi kwenye Majanga makubwa ya Vita au asili tunaweza kupoteza watu zaidi ya laki moja kwa wiki,

Ifike hatua tuiwajibishe serikali ya CCM kwa kuiweka pembeni tuanze upya, ni aibu kuona viongozi wa Serikali wanaenda eneo la maafa na magari ya zaidi ya billioni 3 alafu wanashindwa kuwa na vifaa vya uokozi visivyozidi billion 1.
 
IMG_0256.jpeg
 
Hivi makomandoo wetu hawaezi kupenya penya kama miners taratibu kwa kutambaa na vifaa vidogo vidogo kama vya wachimbaji wadogo wadogo wa madini..... Taratibu sana kupenya kama nyoka.....
Sijui lakini... Nawaza TU. SI kwa ubaya
 
Makomando wa Nini wakati mna Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Yaani ni katika kusaidiana... Maana na mkubwa wa kazi JW SI Yuko hapo... Washirikiane. Maana naona na wao SI watakuwa na mafunzo ya hali ya juu kwenye mambo kama hayo???? Let say hapo ndani kuwe na high value asset SI wangei-retrive TU??? Yaani unachokonoa unapenya.... Taratiibu
 
Kukaa sana kwa amani tunalewa sio polisi, uhamiaji, JW au wapi tuko vizuri. Tatizo ni kukaa na imani kwamba jeshi ni kwa ajili ya vita tu, zana (sio silaha) za kijeshi zina dual use ukiwa nazo zitatumika sana kwa civilians kuliko mara moja kwa miaka kadhaa usubiri vita.

Jana nimeona mabasi ya JWTZ yamejaza wanajeshi wakashuka mikono mitupu, sanasana walichosaidia ni kusogeza watu pembeni ili magari ya wagonjwa na viongozi wapite. Jambo ambalo mgambo anaweza.

Nchi zenye majeshi yenye bajeti, zilizokaa chonjo unakuta military ina search and rescue helicopters kadhaa za nchi kavu na majini, ikitokea mafuriko au meli kuzama wanajeshi wanawahi. Kule Bukoba ajari ya ndege tungeona Navy wanatumia ujuzi wao kama wangekuwa na small base Bukoba au Mwanza, badala yake wavaa yeboyebo kina Majaliwa ndio walionekana.
Hizohizo helicopters zinatumika kuzima moto mkubwa ukiwaka mjini, au milimani kama Kilimanjaro kule moto huwaka mara nyingi.

Hapa kwenye hili jengo tungeona Engineering Brigade ambayo imefundishwa vitu kama kutengeneza airstrip ya haraka wakati wa vita, kurekebisha barabara na madaraja kama Bailey bridge, kuwa na floating piers kusafirisha mizigo ya dharura kwenye mito, kujenga base kwa haraka, kufanya demolition au kuokoa kama strategic factories, buildings zimeharibiwa na adui.

Ingekuwa hivyo tungeona jeshi wanafika na zana zao wanafanya kazi kwa haraka na kwa ufanisi zaidi maana discipline ya kuwa haraka wanakuwa nayo, mafunzo ya gharama kubwa wanayo, vifaa vya uwezo zaidi wanavyo.
Sasa bongo bajeti kama hiyo haitengwi.
 
Hivi makomandoo wetu hawaezi kupenya penya kama miners taratibu kwa kutambaa na vifaa vidogo vidogo kama vya wachimbaji wadogo wadogo wa madini..... Taratibu sana kupenya kama nyoka.....
Sijui lakini... Nawaza TU. SI kwa ubaya
Duh!...hii kali..
 
Yaani ni katika kusaidiana... Maana na mkubwa wa kazi JW SI Yuko hapo... Washirikiane. Maana naona na wao SI watakuwa na mafunzo ya hali ya juu kwenye mambo kama hayo???? Let say hapo ndani kuwe na high value asset SI wangei-retrive TU??? Yaani unachokonoa unapenya.... Taratiibu
Tanzania Tatizo hawataki Kuambiwa Ukweli ila hakuna Haja ya Jeshi la Zimamoto maana Halina Linachofanya mpaka Sasa hivi..

Halina Vifaa wala halina Nyendo za Kufanya kazi zaidi ya Maji na Vigali vyao vyekundu..

Ila Mimi Naona Walihalalishe Jeshi la Kujenga Taifa Liwe Jeshi rasmi...Waliondoe Kwenye Militia ili ndo Liwe Jeshi la Uokoaji..
Na Lipewe bajeti ya Kutosha
 
Kukaa sana kwa amani tunalewa sio polisi, uhamiaji, JW au wapi tuko vizuri. Tatizo ni kukaa na imani kwamba jeshi ni kwa ajili ya vita tu, zana (sio silaha) za kijeshi zina dual use ukiwa nazo zitatumika sana kwa civilians kuliko mara moja kwa miaka kadhaa usubiri vita.

Jana nimeona mabasi ya JWTZ yamejaza wanajeshi wakashuka mikono mitupu, sanasana walichosaidia ni kusogeza watu pembeni ili magari ya wagonjwa na viongozi wapite. Jambo ambalo mgambo anaweza.

Nchi zenye majeshi yenye bajeti, zilizokaa chonjo unakuta military ina search and rescue helicopters kadhaa za nchi kavu na majini, ikitokea mafuriko au meli kuzama wanajeshi wanawahi. Kule Bukoba ajari ya ndege tungeona Navy wanatumia ujuzi wao kama wangekuwa na small base Bukoba au Mwanza, badala yake wavaa yeboyebo kina Majaliwa ndio walionekana.
Hizohizo helicopters zinatumika kuzima moto mkubwa ukiwaka mjini, au milimani kama Kilimanjaro kule moto huwaka mara nyingi.

Hapa kwenye hili jengo tungeona Engineering Brigade ambayo imefundishwa vitu kama kutengeneza airstrip ya haraka wakati wa vita, kurekebisha barabara na madaraja kama Bailey bridge, kuwa na floating piers kusafirisha mizigo ya dharura kwenye mito, kujenga base kwa haraka, kufanya demolition au kuokoa kama strategic factories, buildings zimeharibiwa na adui.

Ingekuwa hivyo tungeona jeshi wanafika na zana zao wanafanya kazi kwa haraka na kwa ufanisi zaidi maana discipline ya kuwa haraka wanakuwa nayo, mafunzo ya gharama kubwa wanayo, vifaa vya uwezo zaidi wanavyo.
Sasa bongo bajeti kama hiyo haitengwi.

Well said....

Haya mambo uliyotaja ni gharama sana chief...
 
Kwangu mimi naona Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Livunjwe..
Na JKT chini ya Jeshi la wanachi Liwe Jeshi Rasmi na Iondolewe kwenyr Militia..
Baada ya Hapo Bajeti iliyokuwa Ikipelekwa Kwenye zimamoto Ihamishiwe Wizara ya ulinzi..
Na Moja kwa moja JKT iruhusiwe Kurecruit Wanajeshi...

Ukiangalia waliojenga Msovera ni JKT...Ukuta wa Mererani Ni JKT vitu vyote hufanya wao kwanini Sasa Tusivunje tu Hii ZIMAMOTO na Rasmi.Jukumu Liende kwa JKT
 
Tanzania Tatizo hawataki Kuambiwa Ukweli ila hakuna Haja ya Jeshi la Zimamoto maana Halina Linachofanya mpaka Sasa hivi..

Halina Vifaa wala halina Nyendo za Kufanya kazi zaidi ya Maji na Vigali vyao vyekundu..

Ila Mimi Naona Walihalalishe Jeshi la Kujenga Taifa Liwe Jeshi rasmi...Waliondoe Kwenye Militia ili ndo Liwe Jeshi la Uokoaji..
Na Lipewe bajeti ya Kutosha
Well spoken
 
Kukaa sana kwa amani tunalewa sio polisi, uhamiaji, JW au wapi tuko vizuri. Tatizo ni kukaa na imani kwamba jeshi ni kwa ajili ya vita tu, zana (sio silaha) za kijeshi zina dual use ukiwa nazo zitatumika sana kwa civilians kuliko mara moja kwa miaka kadhaa usubiri vita.

Jana nimeona mabasi ya JWTZ yamejaza wanajeshi wakashuka mikono mitupu, sanasana walichosaidia ni kusogeza watu pembeni ili magari ya wagonjwa na viongozi wapite. Jambo ambalo mgambo anaweza.

Nchi zenye majeshi yenye bajeti, zilizokaa chonjo unakuta military ina search and rescue helicopters kadhaa za nchi kavu na majini, ikitokea mafuriko au meli kuzama wanajeshi wanawahi. Kule Bukoba ajari ya ndege tungeona Navy wanatumia ujuzi wao kama wangekuwa na small base Bukoba au Mwanza, badala yake wavaa yeboyebo kina Majaliwa ndio walionekana.
Hizohizo helicopters zinatumika kuzima moto mkubwa ukiwaka mjini, au milimani kama Kilimanjaro kule moto huwaka mara nyingi.

Hapa kwenye hili jengo tungeona Engineering Brigade ambayo imefundishwa vitu kama kutengeneza airstrip ya haraka wakati wa vita, kurekebisha barabara na madaraja kama Bailey bridge, kuwa na floating piers kusafirisha mizigo ya dharura kwenye mito, kujenga base kwa haraka, kufanya demolition au kuokoa kama strategic factories, buildings zimeharibiwa na adui.

Ingekuwa hivyo tungeona jeshi wanafika na zana zao wanafanya kazi kwa haraka na kwa ufanisi zaidi maana discipline ya kuwa haraka wanakuwa nayo, mafunzo ya gharama kubwa wanayo, vifaa vya uwezo zaidi wanavyo.
Sasa bongo bajeti kama hiyo haitengwi.
Imagine Jeshi letu huwa lina yale matukio ya kufanya usafi, ni aibu sana
 
TUNGEWEZA KUTUKMIA NJIA YA ASILI,

TUNGEPANGA MISTARI KUMI,
WENGINE WANAJAZA UDONGO KWENYE NDOO.

WENGINE KWENYE FOLENI TUNAJAZA MALOLI 200 MENDE.

NDANI YA MASAA KUMI KUSINGEKUWA NA KIFUSI WATU WOTE WANGEPONA.

SELIKALI HAINUNUI HATA MITAMBO YA UOKOAJI.

NI LAANA KWA MTU MWENYE AKILI TIMAMU KUZALIWA KWENYE HILI TAIFA.
 
Kwangu mimi naona Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Livunjwe..
Na JKT chini ya Jeshi la wanachi Liwe Jeshi Rasmi na Iondolewe kwenyr Militia..
Baada ya Hapo Bajeti iliyokuwa Ikipelekwa Kwenye zimamoto Ihamishiwe Wizara ya ulinzi..
Na Moja kwa moja JKT iruhusiwe Kurecruit Wanajeshi...

Ukiangalia waliojenga Msovera ni JKT...Ukuta wa Mererani Ni JKT vitu vyote hufanya wao kwanini Sasa Tusivunje tu Hii ZIMAMOTO na Rasmi.Jukumu Liende kwa JKT
Ina maana tusiwe na jeshi la akiba?...

Ni vyema hili jeshi la zimamoto na uokoaji liboreshwe zaidi...(Vifaa )
 
Back
Top Bottom