Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Rais Dkt. John Magufuli leo Disemba 20, 2018 anatarajia kuzindua uwekaji wa jiwe la msingi tayari kwa ujenzi wa daraja la kisasa la Selander litakalopita juu ya bahari kutoka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach lenye urefu wa kilometa 6.23 hivyo kupunguza adha ya foleni jijini Dar es salaam.
=======
UPDATES:
Mhandisi Patric Mfugale: Mradi una lengo la kupunguza msongamano wa magari yanayoingia na kutoka jijini na litakuwa na njia 4 za magari.
> Mradi unagharamiwa na fedha za mkopo Serikali ya Jamhuri ya Korea pamoja na Tanzania
#JFLeo
Mhandisi Patrick Mfugale: Mradi utagharimu fedha za kimarekani dola milioni 112.8 na ujenzi umekwishaanza ambapo mkandarasi ameshatengeneza daraja la dharura ambalo litakuwa linatumika kwa kipindi chote cha ujenzi kama ambavyo ilifanyika kwenye ujenzi wa daraja la Kigamboni.
#JFLeo
Waziri wa ujenzi: Katika ujenzi wa BRT tutakuwa na awamu ya 3 na 4 ya awamu ya 3 itaanzia katikati ya jiji la Dar es Salaam kwenda Gongo la Mboto ili kurahisisha usafiri.
> Nakushukuru sana Rais kwa kazi kubwa unayoifanya kwenye wizara yangu hii ya ujenzi na uchukuzi
#JFLeo
Waziri wa ujenzi: Nimejipanga kuhakikisha sekta ya uchunguzi inaongeza kiwango chake inachochangia kwenye pato la taifa.
- Reli yetu inatakiwa kubeba tani laki 9 lakini mwaka juzi na mwaka jana ilibeba tani chini ya laki 2.
#JFLeo
Waziri wa ujenzi: GDP ilikuwa 15% lakini kwa kuweka jiwe la msingi leo nina imani itaongezeka.
- Nimepata taarifa wageni wengi hawapendi kuwapa watanzania mikataba ya kazi na hili nitalisimamia kuhakikisha linatekelezwa
#JFLeo
Rais Magufuli: kipindi tunapata uhuru uchumi wa Tanzania ulikuwa unalingana na wa Korea. Lakini wenzetu waliamua kufunga mkanda na leo hii wametupatia mkopo huu wa ujenzi.
- Nawasihi nasi tuamie sasa kukaza mkanda
#JFLeo
Rais Magufuli: Natoa wito kwa "ma-contactor" kufanya kazi mapema na nitafurahi kama mradi huu utamalizika mapema.
- Hakuna sababu ya kuchelewa maana fedha zipo na makandarasi wapo, tumalize mapema ili tusherehekee.
#JFLeo
Rais Magufuli: Hili jina la daraja mnaloliita New Selander Bridge, nafikiri mngelibadilisha na kuliita jina lingine ambalo litaitangaza Tanzania vizuri kimataifa.
- Hata mngeliita Tanzanite kwani ni madini pekee yanayopatikana Tanzania ila msiite jina la mtu.
#JFLeo
Rais Magufuli: Coco Beach kunatia aibu, watu wanakwenda pale lakini hakuna hata choo, sasa hivi ndiyo wameanza kujenga choo.
- Mtu anakwenda pale na gari analipa TZS 2,000, sasa sijui huwa wanazipeleka wapi. Wameshindwa hata kujenga vibanda vya kufanana watu wafanye biashara.
#UjenziDarajaSelander
#JFLeo
Rais Magufuli: Daraja la Selander litakuwa ndio daraja refu zaidi hapa Tanzania (lina Kilometa 6.23), likifuatiwa na Daraja lile la Mkapa la mto Rufiji lenye Mita 970.
#UjenziDarajaSelander
#JFLeo
Rais Magufuli: Tuhamasishe vijana kufanya kazi hapa ili fedha za miradi hii zibaki hapa nchini.
Hii miradi iwe mwanzo wa kuchapa kazi. Mwl.Nyerere alisema "watu lege lege wenye mioyo kama ya kuku hulizwa na changamoto lakini wale shupavu hukomazwa na changamoto".
#JFLeo
RC MAKONDA: MWAKA 2020 VIONGOZI WOTE WA DAR WATATOKA CCM
-
Makonda amesema kwa maendeleo yanayofanyika kwenye mkoa huo ana uhakika wapinzani wengi wataunga mkono juhudi hizo na kufanya viongozi wengi kutoka CCM
-
Dar kwa sasa kuna baadhi ya viongozi wa kuchaguliwa wanaotokana na vyama vya upinzani, wakiwemo Madiwani, Wabunge na Mameya wa CHADEMA na CUF.
-
Makonda ametoa kauli hiyo leo Desemba 20, 2018 katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Selander na barabara unganishi
-
Amedai kitendo cha Wabunge wa upinzani kuhamia CCM ni toba na bado wapo Wabunge na Madiwani hadi sasa wanaulizia kujiunga na chama hicho
Rais Magufuli: Hata Serikali ikifanya makosa iadhibiwe sawa sawa na wananchi wanavyoadhibiwa pindi wanapovunja sheria, ili kusudi Serikali nayo ifuate sheria.
#UjenziDarajaSalender
#JFLeo
Rais Magufuli: Mama Lishe watakuja hapa, mtakuwa mnakula na msiwasumbue, mwenye maji na auze, hakuna cha bure
- Tutumie nafasi hii, tuwahamasishe vijana wetu waje wafanye kazi hapa, Watanzania tuache kulalamika.
#JFLeo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Cho Tae-ick kufunua pazia kuashiria kuwekwa kwa jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selander na Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mama Janeth Magufuli na viongozi wengine wanashuhudia.
Habari zaidi...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 20 Desemba, 2018 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja jipya la Selander linalounganisha eneo la Aga Khan na Coco Beach Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Daraja hilo lenye urefu wa meta 1,030 na upana wa meta 20.5 litakuwa na njia 4 za magari na njia 2 za watembea kwa miguu, na litajengwa pamoja na barabara unganishi zenye jumla ya kilometa 5.2.
Sherehe za uwekaji jiwe la msingi katika mradi huo zimefanyika katika eneo la Aga Khan na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai, Mawaziri, Wabunge, Mabalozi wa nchi mbalimbali, viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa Dini, viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Paul Makonda.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale amesema ujenzi wa daraja hilo utakaochukua muda wa miezi 30 kuanzia tarehe 23 Julai, 2018 utagharimu shilingi Bilioni 256 zilizotolewa kwa mkopo nafuu kutoka Jamhuri ya Korea kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi (EDCF) na Serikali ya Tanzania.
Mhandisi Mfugale ameongeza kuwa daraja hilo litadumu kwa muda wa miaka 100 na litajengwa bila kuathiri nyumba zilizopo kando ya barabara za Kenyatta na Toure ambazo miongoni mwake wanaishi Mabalozi.
Mhe. Rais Magufuli ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kufadhili ujenzi wa daraja hilo na amemuomba Balozi Mteule wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mhe. Cho Tae-ick kufikisha ujumbe wake kwa Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Moon Jae-in kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na nchi hiyo hususani wakati huu ambapo inaendelea kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi.
“Jamhuri ya Korea ni marafiki wetu wa kweli, wametusaidia kujenga daraja la Kikwete katika mto Malagarasi na wametusaidia kujenga Hospitali ya Taaluma na Sayansi ya Tiba Mloganzila na miradi mingine, tunawashukuru sana, naomba na sisi Watanzania tubadilike, tuchape kazi, tuwe wazalendo, tuwahimize vijana wetu waje wafanye kazi kwenye mradi huu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli ameitaka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutafuta jina la daraja jipya la Selander na amependekeza lipewe jina la Tanzanite linaloakisi Utanzania.
Aidha, ametoa wito kwa Watanzania wote kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa huku wakitanguliza uzalendo, kudumisha amani na upendo na kutokukatishana tamaa ili Tanzania ifanikiwe kupiga hatua za kimaendeleo kama ilivyofanya Jamhuri ya Korea ambayo uchumi wake ulikuwa sawa na Tanzania miaka ya 60 wakati Tanzania ikipata uhuru.
Mhe. Rais Magufuli amempongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe kwa juhudi zake za kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali ikiwemo kuhakikisha mabasi yote 49,000 yaliyopo nchini yanaanza kutoa tiketi za kielekroniki, kuongeza tija katika ukusanyaji wa mapato ya usafirishaji kwa njia ya reli na kufuatilia meli moja kubwa iliyonunuliwa kwa ushirikiano wa Tanzania na China ili ianze kuja nchini na kuinufaisha Tanzania.
Mapema katika salamu zake Balozi Mteule wa Jamhuri ya Korea Mhe. Cho Tae-ick ameishukuru Tanzania kwa uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati yake na Jamhuri ya Korea ambapo katika kipindi cha miaka 26 ya uhusiano huo, Jamhuri ya Korea imetoa ufadhili wenye thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni 1 na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi inayoongoza kwa ufadhili wa nchi hiyo Barani Afrika.
Nae mwakilishi wa EDCF Mhe. Hyon-jong Lee amesema kwa umuhimu wa kipekee wa uhusiano ya Tanzania na Jamhuri ya Korea, Serikali za nchi hizo zinaendelea na majadiliano ya ufadhili wa miradi yenye thamani ya shilingi Bilioni 687.6 itakayotekelezwa nchini Tanzania katika kipindi cha kuanzia mwaka 2018 hadi 2020.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
20 Desemba, 2018