Yaliyojiri Kuapishwa kwa Mkuu wa Majeshi, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ na Mabalozi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Leo ndio siku ya kuapishwa kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usala Jenerali Venance S. Mabeyo na Mnadhimu Mkuu wa Majeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Luteni Jenerali James Aloyce Mwakibolwa.

Fuatilia tukio hili mubashara:
> Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anawasili akiambatana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mawaziri mbalimbali na viongozi nao wanaingia.

> Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt John Magufili awasili ndani ya ukumbi na Wimbo wa Taifa unaimbwa.

> Rais Magufuli amewaapisha Paul Mela kuwa Balozi nchini Democratic Republic Congo na Samwel Shelukindo kuwa Balozi nchini Ufaransa.

> Rais Magufuli amemuapisha Nyamula Matias kuwa Katibu mpya wa Tume ya Utumishi wa Umma.

> IGP Mangu amuapisha Kamishna Robert Boaz Mkomangwa kuwa DCI(Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai).

> Rais Maguli awapongeza waapishwa wa leo na kuongea kuwa anampongeza kipekee kabisa Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Davis Mwamunyange kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi chote.

>Rais Magufuli asema kuwa kazi ya kuteuwa ni ngumu haswa ukiangalia kuwa Meja Jenerali wote wanasifa za kufanana na wote wanaitaka hiyo kazi.

>Rais Magufuli: Nilishinndwa kuteua Mkuu wa Majeshi mpya mapema kwasababu watu wangesema kuwa 'Nimekutumbua'.

> Rais Magufuli nilimuacha Mwamunyange kwasababu ndiye ninayemfahamu, kwasababu nilikuwa nasafiri kuelekea Ethiopia.

> Nilipokuwa Ethipia watu wa mataifa mengine walikuwa wakiniuliza Mkuu wa Majeshi mpya atakuwa nani? Ndipo nikajua hii nafasi ni muhimu kiasi gani.

> Rais Magufuli: Ombi langu ni Tanzania ya viwanda ionekane kwenye majeshi yetu, haiwezekani hadi leo tunaagiza sare kutoka nje ya nchi.

> Rais Maguli anamaliza kuhutubia sasa anaelekea sehemu maalum kwaajili ya kupiga picha.
 
Wanaapa kuilinda na kuitumikia lakini hakuna kipengele cha kung'atuka na waking'atuka hawachukuliwi hatua za kukiuka kiapo kwa nini? Hii si kwenda kinyume na maadili wakuu?
 
Awamu hii hata protocl haifutwi?1 Anaongea makamu wa rais ndio anamkaribisha rais kuongea? inakuwaje hii au ndio KUNYOOSHA nchi huku
 
Hivi wanaapaje?
Ni Kutii amri ya wakubwa wao au katiba ya nchi?
Mimi naona kizungu mkuti tuu.
 
Kuapishwa kwao hakusaidi chochote,hakuna tofauti na kutoapishwa kwasababu hata kama wakiapa sheria zenyewe hawazifuati. Kuapishwa kwa viongozi chini ya serikali ya ccm ni changa la macho kwa watanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…