Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na wenzake - Desemba 1, 2021. Shahidi asimulia alivyowekwa chumba cha mateso gerezani. Uamuzi kusomwa Desemba 14, 2021

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
746
2,103
Leo tarehe 1/12/2021 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe na wenzake inaendelea baada ya kuahirishwa siku ya Jumanne, tarehe 30 Novemba, 2021.

Kujua kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri Mahakama Kuu divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, kesi ya Mbowe na wenzake - 30 Nov 2021

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

UPDATES

Jaji ameshaingia Mahakamani Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ikupendeze naitwa Robert Kidando Wakili wa Serikali Mwandamizi nipo pamoja na

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Esther Martin
Nassoro Katuga

Wote Mawakili wa Serikali Waandamizi Tulimanywa Majige ni Wakili wa Serikali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza Naitwa Peter Kibatala, Naomba Kuwatambulisha

Nashon Nkungu
Paul Kaunda
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata S
eleman Matauka
Evaresta Kisanga
Maria Mushi

Jaji anaita Washitakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali: Mhe Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Session inayo endelea ni Cross Examination, Tupo tayari Kuendelea Na WS Abdallah Chavula Yupo tayari Kuendelea na Maswali ya Cross Examination

Peter Kibatala: Tupo tayari Mheshimiwa Jaji

Jaji: Shahidi Umeamkaje kwanza

Shahidi: Nashukuru Mungu nimeamka Vizuri

Jaji: Naomba Nikikumbushe Kwamba Upo Chini ya Kiapo na Utaendelea Kujibu Maswali Chini ya Kiapo

Jaji: Karibu Wakili

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kabla hatuja endelea Naomba Mahakama Yako inipatie D2 D3, D4 and D5 (Vielelezo)

Wakili wa Serikali: Shahidi hebu tuambie, Tukumbushe, Kwamba Ulisema Uliulizwa Kutaja na DC Msemwa Tarehe 14 May 2020 Ndiyo?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Unafahamu Kwamba Jeshi la Polisi Limegawanyika Katika Idara Mbalimbali

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Na Wewe Elimu yako umesoma Mpaka Level Gani

Shahidi: Nina Digrii ya Elimu

Wakili wa Serikali: Unasema Kwamba Ukiona Yule Bwana Siku ile amevaa Baji yake ikiwa na namba H4323

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni Uniform Kama na huyo Bwana?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Unaelewa Maana ya Neno D/C

Shahidi: Sifahamu

Wakili wa Serikali: Umesema unafahamu Jeshi la Polisi na Idara zote

Shahidi: Sijui zote

Wakili wa Serikali: Unafahamu Idara gani

Shahidi: Idara Ya Ukamataji na Upelelezi

Wakili wa Serikali: na Wale Wa Ukamataji Wanavaa Uniform?

Shahidi: Wengine Wanavaa na Wengine hawavai Wakati wanatukamata

Wakili wa Serikali: Idara ya Upelelezi Wanavaa Uniform

Shahidi: Sifahamu

Wakili wa Serikali: Mimi Sasa Ndiyo Nakwambia Hawavai Uniforms

Wakili Peter Kibatala: OBJECTION huu siyo Wakati wa Submission, Wakili anaanza kutoa yeye Ushahidi

Jaji: Sawa

Wakili wa Serikali: Unasema Siku unaenda Pale Oysterbay Kwamba Ulimkuta D/C Msemwa

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Shahidi Naomba Usimame nataka Nikuonyesha kitu

Shahidi: Mguu unauma

Wakili wa Serikali: Sawa, Jana Ulisema Kwamba DC Msemwa alikuwa na Umbo Kubwa Kuliko Wewe

Shahidi: Nilisema Kwamba DC Msemwa anaweza Kuwa Mpana Kuliko Mimi au anaweza asiwe Mpana Kuliko Mimi

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Unataka Mahakama iamini hivyo

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Jana Ulisema kwamba kwamba Ulifahamu Kwamba DC Msemwa alikuja Kutoa Ushahidi Kupitia Mitandao ya Kijamii

Shahidi: Nilisema Mitandao ya kijamii au Vyombo Vya Habari

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Hukumuona Kwa Macho Alitoa Ushahidi

Shahidi: Ndiyo, ila Vyombo Vya Habari havidanganyi

Wakili wa Serikali: Hakuna Mahala Hapa Mahakamani Ulisema Kwamba Ulimtambua DC Msemwa Shahidi: Sikusema, lakini nilimtambua kwa Majina yake

Wakili wa Serikali: Je Ushahidi huo ulileta hapa Mahakamani

Shahidi: Hapana Sikuleta

Wakili wa Serikali: Shahidi Nilisikia Umesema Kwamba Siku ya Tarehe 19 May 2020 uliporudishwa Oysterbay Uliwakuta nani na nani

Shahidi: Walikuwepo Sam na Khadija

Wakili wa Serikali: DC Msemwa Umemtambua kwa Beji yake na Jina lake

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Sasa nitakuwa Sahihi Nikisema Kwamba Tangu ulipoanza Kutoa Ushahidi, Hakuna Mahala Popote Uliposema na Khadija Hukutaja namba zao za Ajira

Shahidi: Sababu sikuulizwa

Wakili wa Serikali: Uliiambia Mahakama?

Shahidi: Hapana

Wakili wa Serikali: Vilevile Hukueleza Kwamba Sam na Khadija Ulitambua Vipi Majina yao

Shahidi: Ni Kweli Sikueleza Wakili wa Serikali: Ukiachana na Tarehe hiyo, Ni lini tena pale Oysterbay Ulimkuta Sam na Khadija

Shahidi: Tarehe 10 August 2021

Wakili wa Serikali: Nitakuwa Sahihi Kwamba wewe Kwa Tarehe hiyo 10 August 2021 Hakuna Mahala Umeeleza Mahakama Uliwatambua Vipi Kwamba Wale ni Khadija na Sam

Shahidi: Nilieza Mahakama

Wakili wa Serikali: Lakini Hukueleza Mahakama Kuhusiana na namba zao za Ajira

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Kwamba Tangu Ufikishwe pale Oysterbay tarehe 14 May 2020 Ulikaa Kwa Muda Gani

Shahidi: Siku 19

Wakili wa Serikali: Nitakuwa Sahihi Kwamba Kila Siku Ulipokuwa Kule Chini aliyekuwa anakuletea Chakula kule Chini ni DC Msemwa

Shahidi: Hapana, Siyo Kila Siku

Wakili wa Serikali: Nitakuwa Sahihi Nikisema Kwamba Siku ambayo D/C Msemwa Asipokuwa zamu ni Askari Wengine Ndiyo waliokuwa wanakuletea Chakula

Shahidi: Sahihi

Wakili wa Serikali: Nitakuwa Sahihi Kwamba Wakati Wote ulitoa Ushahidi Hapa Mahakamani, hukutaja Jina la Askari Wengine Waliokuwa wanakuletea Chakula Kule chini

Shahidi: Kweli

Wakili wa Serikali: Niambie Wale Askari walipokuja Nyumbani Kwako Mwanga Kukukamata Walikupekua Maungoni

Shahidi: Hawakunipekua

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama tangu unakamatwa Mpaka Unafikishwa Oysterbay ni wakati Gani Ulipekukiwa Mauongoni

Shahidi: Nikiwa Police Central Moshi

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Wewe Ulipekukiwa Maungoni Mara Moja tu Polisi Central Moshi

Shahidi: Ndiy

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Ujaielezq Mahakama Ulipo pekuliwa Pale Central Moshi Walikukuta na nini

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Lakini Mimi naamini Kwamba Hawakukuta na Kitu Chochote

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Na Hii Inatokana kwa sababu Ulikuwa Nyumbani Kwako Umelala wakakubeba Msobemsobe, Hukubeba Chochote

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Na toka Wanakukamata Nyumbani Kwako Hawakukuachia Huru Wakati wowote, Mpaka wanakufikisha Moshi

Shahidi: kweli

Wakili wa Serikali: Licha ya Kwamba Ulikamatwa Hukuwa na Kitu chochote Ulipekukiwa Hukuwa na Kitu chochote, na Mpaka Unafikishwa Central, Lakini Bado Uliweza Kumuelekeza Msemwa akachukue hela Kwenye PPR yako Akakuchukukie Chakula

Shahidi: Kweli

Wakili wa Serikali: Ni kweli Kwamba Katika Ushahidi Wako wote hapa Mahakamani, Hakuna Sehemu Umesema Kwamba Ulipofika Oysterbay Ulimkabidhi Vitu kadha wa kadha?

Shahidi: Sasa PPR nilipataje?

Wakili wa Serikali: Jibu swali Hapa Mahakamani uliongea Kwamba Ulikabidhi Vitu

Shahidi: Sikuongea

Wakili wa Serikali: Katika Ushahidi Ulioutoa Kwamba Ulipofika Oysterbay Polisi walikuandikia PPR ukaenda naye Mahabusu

Shahidi: Nimeshalijibu kupitia swali lililopita

Wakili wa Serikali: Naomba alijibu swali langu Mheshimiwa Jaji

Jaji: Mimi sikumbuki kama ulijibu

Shahidi: Naomba arudie swali lake

Wakili wa Serikali: Katika Ushahidi Ulioutoa Kwamba Ulipofika Oysterbay Polisi walikuandikia PPR ukaenda naye Mahabusu

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Vilevile Hukueleza Mahakama Kwamba Pesa Ulizo ziacha pale Polisi ni TSh ngapi

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Na Hujaeleza Kwamba Yule DC Msemwa Ulimpa Kiasi gani akakununulie Chakula

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Nimuonyeshe Shahidi Exhibit D4

Wakili wa Serikali: hiyo ni Nyaraka gani

Shahidi: Ni Charge Sheet

Wakili wa Serikali: Unaifahamu Wewe

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Kivipi

Shahidi: Kwa sababu Siku Nafika Mahakamani Tarehe 19 May 2020 na Kwa sasa Ndiyo nimeitoa Mahakamani

Wakili wa Serikali: Kwamba Tarehe 19 May 2020 ulipewa hiyo

Shahidi: Ndiyo Nilipewa hlafu ikachukuliwa na Wakili wa Serikali

Wakili wa Serikali: Ni sahihi nikisema kwamba hiyo nyaraka ni photocopy?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Ifungue yote

Shahidi: wewe uliza swali, NISHAIONA!

Wakili wa Serikali: Hiyo Nyaraka ni wapi Ina Muhuri Wa Mahakama Kwamba Ni Nyaraka ya kweli kutoka Kwenye Nyaraka halisi

Shahidi: Haina

Wakili wa Serikali: Ni wapi Katika Nyaraka Hiyo Pameandikwa ni Copy kutoka katika Nyaraka halisi

Shahidi: Hakuna

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakamani, ni Mahala gani inatambulisha au kuonyesha kwamba wakati Unaleta Kisutu Kwamba Ulikuwa Unatoka Oysterbay

Shahidi: Hakuna Nyaraka Inaweza Kuonyesha hivyo na Haiwezi Kuwa nayo

Wakili wa Serikali: Nyaraka hiyo inakuhusisha na makosa yapi?

Shahidi: Matumizi mabaya ya mtandao

Wakili wa Serikali: Unaweza kutusomea

Shahidi: Nimeshaisoma jana

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba anisomee, shahidi amekuwa mkaidi

Jaji: Shahidi soma, Jana wakati unasoma Hakuwa anakuuliza maswali

Shahidi ANASOMA

Wakili wa Serikali: Ni Makosa gani Umeshtakiwa nayo

Shahidi: Publication of phonograph

Wakili wa Serikali: Soma na Sehemu za Particulars

Shahidi anasoma

Wakili wa Serikali: Soma hizo phonograph sasa

NASHON NKUNGU: Mheshimiwa Jaji Shahidi ameshasema, Tukiendelea na Mfumo huo hatutomaliza

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ni Busara tena aweze Kusoma?

Jaji: Mwanzo wakati anasoma Sikuandika, Sasa wakili anataka ataje ili niweze Kuandika

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji haina shida Tunamruhusu shahidi wetu asome Kwa Kadri iwezekanavyo.

Shahidi anasoma

Wakili wa Serikali: Nitakuwa Sahihi Kwamba Wakati Unatoa Kielelezo hapa Mahakamani, Hakuna Mahala Umeiambia Mahakama Kwamba Wakati Yote yanaendelea Kwamba Ulitoa Malalamiko yako Juu ya sahihi wa Mashtaka hayo

Shahidi: Nilieleza Mahakama

Wakili wa Serikali: Kwa ulivyosoma nyaraka hii, D4

Shahidi: Naiomba, unaniambia nyaraka wakati sina nyaraka hiyo!

Wakili wa Serikali: ukiingalia nyaraka hii haina mahusiano na shauri hili ambalo wewe unalitolea ushahidi

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Nitakuwa Sahihi Nikisema Miongoni Mwa Mambo Uliyo muelekeza Wakili wako Kibatala ayafanye ni Kuomba Mwenendo Wa kesi iliyokuwa inakukabili wewe Mahakama Ya Kisutu

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Na wewe ulipewa Mwenendo huo

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Uliisoma yote

Shahidi: Ndiyo Baada ya Kutoka Kisutu

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Kwamba Ulivyosoma Ulielewa yaliyomo Ndani ya hiyo Nyaraka

Shahidi: Ndiyo nikiongozwa na Wakili Fredrick Kihwelo

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Ulisoma Mkiwa Wawili?

Shahidi: Ndiyo Baada ya Kusoma na Kuona Sielewi Nikamuomba Wakili Fredrick Kihwelo anifafanulie

Wakili wa Serikali: Baada ya Kumuhusisha Wakili Fredrick Kihwelo Nitakuwa sahihi Yaliyomo Ndani wewe Unayafahamu Sana

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba ni Muonyeshe D5, Umetambua?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Umetambua ni nini

Shahidi: Mwenendo wa Kesi

Wakili wa Serikali: Ilikuwa Ikimuhusu Nani

Shahidi: Lembrus MCHOME

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Kwamba Inaonyesha Ulirudishwa Kituo gani Cha Polisi

Shahidi: Inaonyesha Kwamba Nilirudishwa Polisi lakini haijataja ni Kituo gani kwa sababu Hakimu hakuwa anajua

Wakili wa Serikali: Unasema Kwamba Ulipelekwa Mahakamami Siku ya Tarehe 19 May 2020

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Na Ni sahihi Hakimu aliagiza Kwamba Upelekwe Gereza la Keko

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Hii ilikustaajabisha sana kwa sababu Ulitakiwa Upelekwe Gereza la Keko wewe Ukarudishwa Polisi Oysterbay

Shahidi: Sikustaajabu Kwa Sababu Ndiyo Ulikuwa Utaratibu Wa wakati huo

Wakili wa Serikali: Uliridhika nao

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi nitakuwa Sahihi Kwamba Ukitizana Kielelezo namba 05 Kwamba Hakuna Sehemu inasema ulikuwa Kituo Cha Polisi Oysterbay

Shahidi: Ndiyo haiwezi Kuwepo Hapo

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Kwamba wewe tuh Ndiyo ulikuwa unajua Umehifadhiwa wapi

Shahidi: Mimi na Wakili Wangu Ndiyo tulikuwa tunajua

Wakili wa Serikali: Lakini Wewe na wakili wako Hakuna Sehemu Mlieleza Mahakama Ya Kisutu Mlikuwa wapi

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: nitakuwa sahihi kwamba Wakili wako alijua umefikishwa mahakamani Tangu siku ya tarehe 19 May 2020

Shahidi: Hakupata taarifa siku hiyo, nilipelekwa KIHUNIHUNI Bila wakili wangu kujua

Wakili wa Serikali: Nitakuwa Sahihi Nikisema Kwamba Ulipata Kuonana Na Wakili wako tarehe 02 June 2020

Shahidi: Ndiyo, na Ndiyo ilikuwa Mwanzo wa Kuonana na Wakili Wangu

Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Hili Shauri wewe, Kesi hii kwa Ujumla nitakuwa Sahihi Kwamba Ulianza kuifutilia toka Ilipoanza Kusikilizwa na Mahakama

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Mpaka Kufikia Sasa Matukio Yaliyokuwa yanajiri Kipindi cha Nyuma yote Unayafahamu

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Jana Wakati Unahojiwa na Wakili Mwenzangu, Juu ya Ufahamu wako wa Kesi Ndogo Ya Hassan Kasekwa, na wewe Ukasema Kweli Ulikuwa na Ufahamu Wa Kesi Ndogo,

Sasa Licha ya Kuwa Ulikuwa unafahamu Kesi Ndogo Ya Adam Kasekwa, hukueleza Mahakama Sababu ya wewe Kutokuja Kutoa Ushahidi, hilo wewe Huku zungumza Katika Ushahidi Wako.

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Samahani Mheshimiwa Jaji nawasiliana na Wenzangu Kidogo

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba nimkaribishe Mwenzangu Pius Hilla naye ana machache

Jaji: Mr Hilla, yale ambayo yameshaulizwa naomba Usiulize

Wakili wa Serikali: Nashukuru Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumuonyesha Shahidi D3

Wakili wa Serikali: Mr Mchome Nyaraka hiyo Niliyo Kuonyesha ni nini

Shahidi: Ni Dispatch Book

Wakili wa Serikali: Ni kweli hiyo Dispatch Book haina sehemu ya entry ya Msemwa

Shahidi: Ndiyo kwa Sababu ilikuwa inahusu Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu

Wakili wa Serikali: Je ina Ushahidi Wowote Kuhusiana na Ushahidi alioongea Msemwa?

Shahidi: Hapana

Wakili wa Serikali: Dispatch hiyo ina Jina lako wewe Kwamba Ulikuwa Oysterbay

Shahidi: Siyo Kazi ya Dispatch hiyo, kazi yake ni Kupokea Barua

Wakili wa Serikali: Jibu swali

Wakili Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji Lazima tupinge hilo, Kuna tabia, Jibu likibiwa hawataki, Tunaomba Jibu liheshimiwe

Wakili wa Serikali: Kuna hii tabia Mheshimiwa Jaji tunaomba Mahakama Yako Itoe ufafanuzi, Wakili wa Mshtakiwa hasimami ila Unakuta anasimama Wakili Mwingine.

Wakili Kibatala: Mheshimiwa Jaji Wanapaswa wafahamu Kwamba Mohammed Ling'wenya ni Co-Accusate wa Kila Wakili

Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Shahidi ameshajibu hilo swali

Jaji: Kwa hiyo tukubaliane Kuanzia Leo tuweke Precedent Kwamba Shahidi anajibu Jibu lolote?

Wakili Fredrick Kihwelo: Simaanishi hivyo, Basi tunasikiliza Mwongozo Wako..

Wakili wa Serikali: Kwenye Dispatch Kuna Sehemu inasema Uliwekwa Oysterbay

Shahidi: Hapana

Wakili wa Serikali: Kwenye Dispatch Kuna Sehemu inasema Ulikutana na Msemwa

Shahidi: Hapana

Wakili wa Serikali: Kwenye Nyaraka Ulizo leta Mahakamani Kuna Namba Ya kazi ya DC Msemwa, Ni kweli Kwamba Ulielezea Mahakama namba ya DC Msemwa Uli' note?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Uli' note Kwenye Kitu gani

Shahidi: Nili note kwa kuangalia

Wakili wa Serikali: Uli' note Kwenye Nyaraka gani

Shahidi: Siku note Kwenye Nyaraka

Wakili wa Serikali: Tangu Upelekwe Oysterbay ni Muda gani umepita

Shahidi: Mwaka na Miezi kama Mitano

Wakili wa Serikali: Umekutana na Askari Polisi Wangapi

Shahidi: Wengi

Wakili wa Serikali: Yupi hapa Mahakamani Umemtaja namba yake

Shahidi: Hakuna

Wakili wa Serikali: Ni kweli kwamba hukuwa na ukaribu na D/C Msemwa

Shahidi: Ndiyo Kwa sababu sina michongo naye

Jaji: Samahani, neno MICHONGO tafsiri yake nini?

Shahidi: MICHONGO ni SHUGHULI ZA UTAFUTAJI

Wakili wa Serikali: Ulisema Kwamba Umepata Taarifa za Hii Kesi Kwenye Mitandao

Shahidi: Mitandao na Vyombo Vya Habari Wakili

Dickson Matata: Mheshimiwa Jaji tunakiuka Makubaliano ya Juu Muda na Kutokurudia rudia Maswali

Jaji: Wakili Nakukumbusha Concern ya Muda, na Kutokurudia Maswali

Wakili wa Serikali: Ni sahihi wewe Siyo Wakili wa Washitakiwa

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo wewe ujapewa Vitabu Vya Ushahidi wa kesi hii

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Kwamba Kwenye kesi hii Hapa Mahakamani hujui zaidi ya kwenye Mitandao na Vyombo Vya Habari?

Wakili wa Serikali: Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji

Shahidi: UMESAHAU DISPATCH YAKO HAPA

Jaji: Asante Shahidi, Hiyo siyo ya kwake ni ya Mahakama

Jaji: Wakili, Kaomba kasahau Kurudisha

Mahakama: Kicheko

Wakili Fredrick: Jana Uliulizwa Kuhusiana na Tweet zako, Michongo, Je zilikuwa na Maana gani

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji OBJECTION Jana niliuliza kuhusu Maana,

Jaji: Jana nyie Mliuliza nini

Wakili wa Serikali: Kuhusu Maana ya Hizo Tweet

Jaji: Sasa Tatizo lipo wapi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kuondoa Hiyo OBJECTION yetu tumuache ajibu tu swali

Wakili Fredrick: Jana Uliulizwa Kuhusiana na Tweet zako, Michongo, Je zilikuwa na Maana gani

Shahidi: Zilikuwa na Maana Kwamba Kuna Baadhi ya Mashahidi Wanaoletwa Mahakamani siyo Mashahidi Wa Ukweli, Mashtaka ya Kutungwa.. Na Vilevile Mahakama Itende Haki.

Wakili Fredrick: Uliulizwa Kuhusiana na Uanachama wako na Mapenzi yako kwa Freeman Mbowe

Shahidi: Mimi nafahamiana na Mbowe na ni Mwenyekiti wangu na Ni Mwanachama na Kiongozi wa Chadema lakini Hapa Sijaja Kumtolea Ushahidi Mbowe Nimekuja Kutolea Ushahidi Mohammed Ling'wenya

Wakili Fredrick: Uliulizwa Kwamba Ulipoenda Central Moshi Hukukutwa na Chochote, Ulikuwa na unamaanisha nini

Shahidi: Kwamba Nilikaguliwa sikuwa na Kitu chochote zaidi ya nguo zangu

Jaji: Wakili Matata Una jambo Lingine

Jaji: Bwana Mchome, Asante Kwa ushahidi wako, na Vilevile naomba radhi tumekukalisha hapo ukiwa mgonjwa na maumivu. Lakini kama ulivyosema kwamba unataka haki itendeke basi naamini umefanya hivyo sababu ya Haki

Shahidi: Ahsante Mheshimiwa Jaji

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Wenzetu Wana Shahidi Mwingine lakini tunaomba Hisani yako na Understanding ya Wenzetu Tupewe Nusu Saa na tuingie Saa 6 Kamili na Shahidi Mwingine

Wakili wa Serikali: Sawa Mheshimiwa Jaji

Jaji: Basi tuna break Kwa muda wa dakika 7 hivi, tutarudi Mahakamami Saa 6 Kamili

Jaji kaongeza muda wa mapumziko, tutarudi mahakamani tena saa saba, saa za Afrika Mashariki

Jaji amerejea Mahakamani

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa tena Muda huu

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji tupo Kama awali isipokuwa Pius Hilla amepatwa na dharula, Sisi tupo tayari Kuendelea Wakili

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa Ruhusa yako sisi tupo tayari na Quorum ipo kama awali

Jaji: Mlisema mnae shahidi mwingine

Shahidi anaenda kizimbani

Jaji: Majina yako Shahidi: Amiri Samheta Mhina

Jaji: Umri wako

Shahidi: 32

Jaji: Kabila

Shahidi: Mzigua

Jaji: Dini yako

Shahidi: Mkristo

Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii, Kwamba Ushahidi nitakaotoa utakuwa wa kweli, kweli tupu Eehee Mwenyezi Mungu Nisaidie

Wakili Dickson Matata: nitamuongoza Mheshimiwa Jaji

Dickson Matata: Shahidi kazi yako kwa sasa ni nani

Shahidi: Mkulima

Dickson Matata: Unafanyika wapi huo Ukulima

Shahidi: Mkoani Tabora

Dickson Matata: Unalima Mazao Gani

Shahidi: Mahindi

Dickson Matata: Kabla ya hapo Ulikuwa wapi

Shahidi: Askari Wa Kikosi cha Special Force Kilichopo Mkoani Morogoro

Dickson Matata: Morogoro ni Kubwa ni Wapi

Shahidi: Ni Sangasanga, Wengi wamezoea Kuita Ngerengere

Dickson Matata: Kikosi Kinaitwaje?

Shahidi: 92 Special Force battalion

Dickson Matata: kazi ya inakuwa nini

Shahidi: Askari Ambaye yupo tayari Kwa Muda wowote Kuitwa a kwenye Mapigano

Matata: Tutajie Kazi zenu

Shahidi: Ikitokea Upo Kwenye Ndege unakuwa Paratroopers, Unashuka Kutoka Kwenye Ndege kwa kuruka Kuja Ardhini Kutekeleza Majukumu Mbalimbali

Matata: Kazi Nyingine

Shahidi: Majukumu Mbalimbali kama Vile Operesheni mbalimbali nchi za Nje kama Sudan na Congo

Matata: We Ushawahi kwenda wapi

Shahidi: Nishawahi Kwemda Sudan

Matata: Ulikwenda Mwaka gani

Shahidi: 2014

Matata: Ulikwenda Kufanya nini

Shahidi: Kutunza Amani

Matata: Kazi ya Jeshi Ulianza Mwaka gani

Shahidi: Nilianza JKT Mwaka 2006, 2007 Nikaenda Jeshi la Wananchi (JWTZ), 2011 Nilienda Kupiga Intake ya Special Force inaitwa 01 INTAKE

Matata: ieleze Mahakama Nini Kilitokea Mpaka Sasa Haupo Jeshini

Shahidi: nilipata Shida ya Afya ya Brain Sarcastic

Matata: ni nini

Shahidi: Ni Ugonjwa wa Akili

Matata: Unatokana na nini

Shahidi: Siwezi Kusema Sababu za Kidaktari lakini ni Ugonjwa Unatokea nilipokuwa kazini

Matata: Uliumwa Muda gani

Shahidi: Kwa Misimu kama Miwili, Ikapelekea Kupelekwa Lugalo na Nikawa nimekaa Kwa Muda kiasi Kumpelekea Kuwa Mtoro Kazini

Matata: Una kitu Gani unachoweza Kuthibitisha Kwamba Uliumwa na Ulifikishwa Lugalo

Shahidi: Hakuna Taarifa niliyopewa kwa Sababu Taarifa zote zilibakia Palepale Lugalo

Matata: Kwanini zilibakia Pale Lugalo Shahidi Siwezi Kusema Nini Kilitokea Kwa sababu baada ya Matibabu nilirudi Kambini na Taarifa zote zilibakia Hospitali

Matata: Ieleze Mahakama Kuna Uhusiano Gani ya huo Ugonjwa na wewe Kutokuja Kazini

Shahidi: Baada ya Mimi Kuumwa na Kupelekea Sababu za utoro, nilifungwa kijeshi, nilipomaliza Kifungo cha Kijeshi nilirudi Kambini Kuendelea Na Majukumu Mengine ya kazi

Matata: Ikawaje

Shahidi: Nilikutana na Mkuu wa Kikosi ambaye alisema hawezi Kukaa na Mtu Mwenye Matatizo Kama Yangu hivyo akani' alert Muda wowote atanifukuza Kazi

Matata: Mkuu wako wa Kikosi anaitwa Nani

Shahidi: Luteni kanali Hiera, sasa kashastaafu Wakili

Matata: Baada ya Pale nini Kiliendelea

Shahidi: Baada ya Kuni alert Atanifukuza alikuja Karani Mkuu wa Kikosi, kanijazisha Fomu ambazo ni Kibali cha kuachishwa Kazi

Matata: Baada ya fomu Ilikuwaje

Shahidi: Baada ya Kuona Kuna Malipo nadai Baada ya Kuwa kwenye Kifungo, na Haki zangu ikanilazimu kwenda Makao Makuu ya Jeshi Kwa Malalamiko zaidi

Matata: Baada ya kwenda Huko

Shahidi: Nikijazishwa Fomu za malalamiko na Kutaarifiwa kwamba baada ya wao Kumjulisha Mkuu wa Kikosi Changu Kuhusu Malalamiko nitatarifiwa tena

Matata: Baada ya Hapo

Shahidi: Nilikaa Kwa Muda Mrefu Kwa ajili ya Majibu Lakini Hakuna Kilichotokea Wala Sikupata Mrejesho Kutoka Wizara ya Ulinzi

Matata: Ukiachishwa Kazi lini

Shahidi: Tarehe 26 April 2020 ndipo nilipoachishwa kazi Rasmi kwa Maana Kutolewa Kwenye Nguvu ya Jeshi

Matata: Sasa Umesema Kwa Utovu wa Nidhamu, Wewe Unasemaje Kwa Ajili ya utovu wa kinidhamu?

Shahidi: Kwenye Malalamiko Niliandika Kwamba nimeonewa na Situation Yangu ilikuwa inatambulika Kidaktari

Matata: Sasa Baada ya Kupewa Taarifa, Ulipewa nini Kuonyeshwa Kwamba Umefukuzwa Kazi

Shahidi: Hakuna Nyaraka Yoyote Niliyopewa, Baada ya Kutoka Upanga (NGOME) kwenda Kupeleka Malalamiko ilinilazimu Kumuona Chief Personnel ambaye ni Ndiye Afisa Muajiri Mkuu wa Jeshi

Matata: Kwanini Sasa Ulienda Dodoma

Shahidi: Nilienda Dodoma Kwa Chief Personnel kwa sababu Ndiye anayehusika na Ajira Jeshini Niliona Kwa Kwenda Kule Naweza Kupata Majibu ya Malalamiko Yangu

Matata: Ilikuwaje Ulipofika kwa Chief Personnel

Shahidi: Kwa sababu Sikuwa na appointment Naye, ilibidi nifuate taratibu za Kijeshi Niache Malalamiko Yangu ili yatakapo Mfikia aniite tena

Matata: Nini Majibu Kutoka Kwa Chief Personnel

Shahidi: Pamoja na Kusubiri Kwa Muda wote Hakuna Majibu yalitoka Rasmi Mpaka Kibali Kilipokuja Kutoka Rasmi hiyo Tarehe 26 April 2020

Matata: Shahidi Unakumbuka nini Kuhusu Tarehe 19 September 2020

Shahidi: Mnamo tarehe 19 September 2020 nikiwa Maeneo ya Nyumbani Rafiki yangu alikuwa anaitwa Dida alinipigia Simu Twende Kuna sehemu Kuna Pub Tukaangalie Mpira

Matata: Unaposema Nyumbani ni Nyumbani Wapi

Shahidi: Nyumbani Mkoani Tabora

Matata: Shahidi Tabora Mjini?

Shahidi: Tabora Mjini, Sehemu Inaitwa Makokora

Matata: Unasema Uliligiwa Simu na Rafiki yako Mkaangalie Mpira Je ni Pub gani

Shahidi: Inaitwa OXYGEN PUB

Matata: Ikawaje

Shahidi: Nilipokuwa Najaribu kwenda Kwenye Lile eneo Kuangalia Mpira Ghafla Nilikamatwa na Task Force Police

Matata: Walikuwa wangapi

Shahidi: Walionikamata Walikuwa wawili lakini baadae niligundua nimezungukwa na Askari Wengi waliokuwa wanasubiri kuwa na Nitachukua Hatua Gani.

Matata: Baada ya Kukukamata Pale Oxygen, Kabla ya Kukukamata Walifanya nini

Wakili wa Serikali: OBJECTION hiyo ni Leading Question

Matata: Kabla ya Kukukamata Walifanya nini

Shahidi: Kuna Askari Mmoja alitoa Pistol akasema nahitajika Mkoani Kwa RCO

Matata: Ikawaje sasa

Shahidi: Baada ya Kuona Naitwa sehemu salama ilinilazimu Kukubali Kupanda Hiyo Gari Kuelekea Mkoani

Matata: Ilikuwa ni Gari Gani

Shahidi: Toyota Land Cruiser, Nyeusi

Matata: Mlikuwa wangapi Kwenye Gari

Shahidi: Jumla ya Watu 4 Wao 3 na Mimi 1, Sababu Ndani ya Hilo Gari palikuwa na Dereva

Matata: Wewe Ulikaa sehemu gani Kwenye hilo gari

Shahidi: nilikaa Mbele Wao wawili Walikuwa wamekaa Nyuma

Matata: Hapo Mbele Ulikuwa na nani

Shahidi: Nilikuwa Mimi na Dereva

Matata: Wakati Unakamatwa ulisema Ulikamatwa na Watu wawili lakini Uligundua Kuwa Kuna Askari Wengine wengi Ulijuaje

Shahidi: Nilikuja kugundua baada ya kufikishwa Kituo cha Polisi baada ya Kuona Palikuwa na Convoy Iliyokuwa Inanifuata

Matata: Kwa sisi ambao hatujapita Jeshi, Ukisema Convoy Unamanisha Nini

Shahidi: Msururu wa Magari ambayo Magari Yenyewe Yalikuwa Mawili

Matata: Mlipofika Pale Tabora Ilikuwaje

Shahidi: Wakati wanasema wanasubiri Kuniunganisha na Huyo RCO walinifunga Pingu na Kunipeleka Ndani ya Kituo cha Polisi Nyuma Kabisa

Matata: Nakurudisha Nyuma Kidogo Ulisema wakati Unakamatwa Kuna Askari alikuwa anakuongelesha Je Alikwambia Maneno gani

Shahidi: Kwamba Nisipotii Amri ya kwenda Polisi Watanimaliza Palepale Kwa Kunitishia na Bastola

Matata: Nini Kingine Walisema

Shahidi: waliniambia Unajua Kesho Kuna Nini Hapa Mkoani, NikaJibu Kwamba Kuna ujio wa Rais anakuja Kufanya kampeni

Matata: Unamaanisha Rais gani

Shahidi: Wakati Ule Hayati Rais Magufuli akiwa anafanya kampeni

Matata: Haya kule nyuma polisi walipokupeleka walikuwa wanakuambia nini?

Shahidi: Walikuwa wananihoji nina uhusiano gani na MH. FREEMAN MBOWE huku wakinipiga vibaya mno.. Kila sehemu ya mwili
wangu

Matata: Pale Kituo Ni sehemu gani yalitendeka hayo

Shahidi: Pale Kituoni Mbele Kuna Meza, Sasa wao Walinipeleka Kwa Nyima kabisa ya Kituo cha Polisi Nyuma Kabisa, Ila Unakuwa Kituoni bado

Matata: Unasema Central Polisi Tuambie Inapakana na nini kama unapajua

Shahidi: Ipo Kama Unaelekea Shule Ya Msingi Itete, Kama Unaelekea Makao Makuu ya Brigedi

Matata: Brigedi Ya nini

Shahidi: Inaitwa 101 Brigade, Ipo Maeneo ya Mtaa wa Kanyenye

Matata: Sasa Umepelekwa kwa Nyuma na ukawa Unapigwa, Je Walikuwa wana Kupiga kwa Kutumia nini haswaa?

Shahidi: Walikuwa Wanatumia Fimbo pia walikuwa wananipiga Ngumi za Taya, mateke na Kadhalika

Matata: Walikuwa Askari wangapi wanakupiga?

Shahidi: Palikuwa na Goodluck, Kiongozi wao anaitwa Afande Jumanne, kulikuwa na Mtu anaitwa Minja na Afande AZIZI, mmoja simkumbuki.

Matata: Zoezi la Kukupiga Lilichukua Muda gani

Shahidi: Muda kama WA MASAA MATATU

Shahidi: Nilipokuwa nakataa kuwa na mawasiliano na Mheshimiwa Mbowe, walinipiga zaidi. Walinipeleka Kituo cha Polisi Cha Reli pale Tabora Maana Hali yangu Ilikuwa mbaya Sana.

Matata: Wakina nani walikupeleka Kule Kituo cha Polisi RELI

Shahidi: Wote waliokuwa wananisurubu pale Kituoni Mkoani, Wakanifuata Tarehe 20 September 2020 Saa Nne Asubuhi, Baada ya Kuona Namkataa Mheshimiwa Mbowe

Shahidi: walianza Kuniuliza Kama Namfahamu Mohammed Abdilah Ling'wenya na Nina Uhusiano Naye gani.

Matata: Ukawajibuje?

Shahidi: Nili kiri Kumfahamu Kwakuwa nilishawahi Kufanya naye kazi Siku za Nyuma na Pia alipokuwa ametoke kazini alikuwa bado ni Rafiki yangu wa Karibu

Matata: Baada ya Kukuhoji nini kiliendelea

Shahidi: Waliendelea Kunihoji kuwa Je nafahamu Kwa sasa hivi Mohammed Ling'wenya Yupo wapi, lakini Kwa Kipindi Kile niliwaJibu sijui Alipo

Matata: Baada hivyo nini kiliendelea

Shahidi: Baada ya Kujibu sijui alipo, Tarehe hiyo hiyo tulielekea Nzega, Tarehe 20 September 2020

Matata: mliondoka Muda gani

Shahidi: Tuliondoka Muda wa Saa 5 Asubuhi, Nikiwa nimefungwa Kitambaa na Kutokana na Hali yangu Ilivyo, Nilikuwa nimefungwa Pingu Muda wote

Shahidi: Nikijaribu Kuwa uliza Mahabusu Wenzangu, Maana Kule walinichanganya

Matata: Kituo gani Nzega

Shahidi: Kituo cha Polisi Nzega

Matata: Baada ya pale nini Kiliendelea

Shahidi: Waliniacha Palepale na Sikujua wameenda wapi

Matata: Kwenye Gari Ya Kwenda Nzega Mlikuwa wangapi

Shahidi: Nilikuwa na Jumanne, Goodluck Minja, ana AZIZI wengine Magari ya Nyuma sikujua wakina nani Kutokana na Kufungwa Kitambaa

Matata: Ilikuwa ni Gari gani

Shahidi: Ileile Cruiser Nyeusi waliyonikamata Nayo Nyumbani

Matata: Wakiwa Wamekufunga Kitambaa, Nini Kilikufanya Ujue Kwamba Ni Jumanne, Goodluck Minja Na Azizi

Shahidi: Kule Nyuma Nilipokuwa Nimekaa Nilikuwa nasikia Wakiitana Majina, Jumanne alikuwa Mbele, Azizi alikuwa Dereva

Matata: Baada ya Kukuacha pale Kituo cha Polisi Nini Kiliendelea

Shahidi: Baada ya Kuniacha na au kunitelekeza Walirudi Siku ya Pili, wakiwa na Mtu Mmoja anaitwa MALEMA ambaye na Yeye alishawahi Kuwa Komandoo.

Matata: huyo Mtu anaitwa MALEMA alikuwa nani

Shahidi: Alikuwa Komandoo, Nilifahamu kuwa alikuwa Komandoo kwa sababu Mazingira Yake ya Kukamatwa Yalikuwa kama Yangu, Ndipo Nikamuuliza wewe nani, akasema anaitwa MALEMA na alishawahi kuwa Komandoo

Matata: Mahojiano yako wewe na MALEMA Uliyafanyia Wapi

Shahidi: Palepale Polisi Tukiwa Mahabusu

Matata: Nini Kilifuatia

Shahidi: Siku inayofuata Asubuhi Yake, tulianza Safari Kila Mtu na Gari yake Kuja Dar es Salaam

Matata: Ili Kuokoa Muda wa Mahakama, Kwenye Gari yako Ulikuwa nani

Shahidi: Nilikuwa Mimi, Afande Jumanne,Minja na Yule Dereva Anaitwa Azizi

Matata: Kuanzia Pale Central Police Tabora, Mpaka Nzega Uliwahi Kuandikwa Kwenye Nyaraka ipi

Shahidi: Kufuatia Kufungwa Kitambaa Cha Macho Hakuna Sehemu ambayo Niliandikwa, Tulipofika Nilikuwa naingizwa Mahabusu Moja Kwa Moja

Matata: Pale Tabora Kwa Ufahamu Wako Kuna Nyaraka Yoyote Ulipewa Kuandika

Shahidi: Hakuna Nyaraka Yoyote Nilipewa Kuandika

Matata: Pale Nzega Kuna Nyaraka Yoyote Ulipewa kuandika

Shahidi: Hakuna Nyaraka Nilipewa Kuandika

Matata: Pale Nzega Pia hukiandika

Shahidi: Kwa Mazingira Ya zile Pingu nisingeweza Kuandika

Matata: tuje Kwenye Safari, Hapa Dar es Salaam Mlifika Lini na Mlifikishiwa wapi

Shahidi: Siku tulivyotoka Nzege Ndiyo Siku ileile Tulifika Dar es Salaam

Matata: Mlifikishiwa Wapi Shahidi: Kituo cha Polisi Tazara

Matata: Nzega Mlitoka Saa ngapi

Shahidi: Nzega Tulitoka Asubuhi Siku ileile Mbayo Walifikia na MALEMA

Matata: Unasema Mlifikishiwa Tazara, Je Unaweza Kukumbuka Ilikuwa tarehe Ngapi

Shahidi: Siku ya 23 September Mwaka 2020

Matata: Na Mlipofika Tazara Mliandikwa Kwenye Nyaraka Ipi

Shahidi: Tulipofika Tazara nilifikishwa Moja Kwa Moja Mahabusu

Matata: Ni akina nani hao walikufikisha Tazara

Shahidi: Ni Wale wale akina Jumanne, Goodluck na Azizi

Matata: Na Tazara ulikaa kwa Siku Ngapi

Shahidi: Nilikaa Kwa Siku 2 na Baada ya Hapo nilifikishwa Mahakamani Siku ya 25 September 2020

Matata: We Ulijuaje upo Tazara

Shahidi: Kwa sababu Mimi Nilikuwa nimetengwa tofauti na Wenzangu Kwa Kila Kitu, Ndipo Mahabusu Mmoja akaniuliza Kwani wewe ni nani na Una makosa gani, Ndipo Nikawajibu Sijui, lakini nimekamatiwa Nyumbani Tabora, Na mimi nikawa uliza Hapa ni Wapi, Wakasema ni TAZARA

Matata: Ukiachana na Mahabusu Kwamba nani Mwingine alikwambia Pale no Tazara

Shahidi: Palikuwa na Afande Mmoja aliniuliza Wewe Mbona Umefungwa Pingu, nikamueleza Mkasa wangu na Baadae Nikamuuliza Afande hapa ni wapi akanijibu hapa ni TAZARA

Na Kwa Kuwa Nyumbani wala Ndugu walikuwa hawajui nipo wapi Nilimuomba yule Afande simu niweze Kuwajulisha Ndugu zangu nyumbani.. Akaniambia Kwamba sijui walikuleta huku wamekuleta kwa Makosa gani, siwezi Kuchukua Jukumu la Kukupa simu Mimi...

Matata: Vipi Kuhusu Chakula

Shahidi: Kwakuwa nilikuwa nimepigwa sana Chupa za Soda Magotini, hali yangu Ilikuwa mbaya Sana, Hakuna chakula nilipewa Chakula, Nilikuwa nakunywa Maji tu TAZARA. chakula Nilikuja Kula Siku ya Tarehe 25 September 2020 baada ya kufika gerezani Segerea

Matata: Baada ya Kukufikisha Tazara wakina Jumanne, Goodluck na Azizi, walirudi tena Lini

Shahidi: Walirudi tena Kesho yake tu, Wakawa wananiuliza Kwamba Je najua yupo wapi Mohammed Ling'wenya Kwa sasa na Adam Kasekwa?

Matata: Hayo Mahojiano Mlikuwa mnayafanyia Wapi

Shahidi: Palikuwa na Chumba Juu, palepale Tazara

Matata: Na Siku hiyo Walikuwa wangapi na nani na nani

Shahidi: Tukiwa katika hicho Chumba Mahita alikuwa anafanyia Mahojiano yule Malema, Mimi nilikuwa na Jumanne na Goodluck, Wakati Yule Mzee Mnene tuliyetoka naye Tabora Sikumuona tena

Matata: Sisi tunataka Tujue kama unapafahamu Tazara, Je Mahabusu palikuwaje?

Shahidi: Yule Malima alikuwa amewekwa Katika Cell ya peke yake, Kule Mahabusu Kuna Vyumba, Ila mimi Nilichanganywa na wengine

Matata: Yule Mahabusu aliyekwambia Hapa ni Tazara Unaweza kumkumbuka Kwa Majina

Shahidi: Hapana Sikumbuki kwa Majina

Matata: Shahidi Kabla ya Tarehe 19 September 2020 Ulikuwa unafahmiana na Goodluck Minja, Azizi & Jumanne

Shahidi: Wote Nilikuwa siwafahamu kabla

Matata: Mahita Pia

Shahidi: Wote Nilikuwa siwafahamu

Matata: Hebu eleza Mahakama Uliwa fahamu fahamu vipi

Shahidi: Tulipokuwa Safarini Minja Nilisikia Jina lake, Ila Tulipokuwa Tazara Kwa a Mahojiano wengine Wote Walikuwa Wakiitana Majina yao, Ila yule Mzee Mnene Sikubahatika Kumfahamu

Matata: Unasema Kwamba Walikuwa wanakuja Tazara Kunihoji Kwani Walikuja Mara Ngapi

Shahidi: walikuja Mara Mbili Kabla ya Kunipeleka Mahakamani

Matata: Katika hizo Mara Mbili walikuwa wanakuja Muda gani

Shahidi: Muda Mwingi Walikuwa wanakuja Asubuhi

Matata: Walikuwa wanaweza kuja kukaa kwa Muda gani

Shahidi: Kwakuwa walikuwa wananisisitiza Kwamba Wenzangu Wapo wapi

Matata: Sikiliza Maswali yangu, Walikuwa wanakuja Kukaa Masaa Mangapi pale Tazara

Shahidi: Masaa Matatu Mpaka Manne, inategemea na torture waliokuwa wananipa

Matata: Nani alikuwa anakupa torture?

Shahidi: Goodluck Minja Ndiyo walikuwa ananipiga sana

Matata: Unasema walikupeleka Mahakamani, Mahakama Gani

Shahidi: Mahakama Ya Kisutu

Matata: Kisutu Ipo wapi

Shahidi: Ipo hapa Dar es Salaam

Matata: Nani alikuja Kuku chukua Kukupeleka Mahakamani

Shahidi: Jumanne, Mahita, Goodluck Minja Na Azizi

Matata: Mlitumia Usafiri Upi

Shahidi: Toyota Land Cruiser Nyeupe

Matata: Wakati Wanakubeba Tangu Tabora Walikwambia Kosa lako no Nini

Shahidi: Niliwahoji tangu Natoka Tabora Wakasema Utaenda Kujua Mahakamani

Matata: Sasa Mlipofika Mahakama Ya Kisutu Ikawaje

Shahidi: Tarehe 25 September 2020 baada ya Kufika Kisutu Nilikutana na Hakimu Na Nikasomewa Mashtaka yanayohusiana na Vitendo Vya Kigaidi

Shahidi: Anaitwa Mheshimiwa Simba

Matata: hiyo kesi ilikuwa kesi namba Ngapi na Mwaka gani

Shahidi: ilikuwa kesi namba 63 ya Mwaka 2020, ya Ugaidi na Uhujumu Uchumi

Matata: Mlikuwa wangapi

Shahidi: Kutokana na Maelezo Niliyosomewa niliambiwa Nitaunganishwa na Wenzangu Wanne Jumla tutakuwa Watano

Matata: Ambao ni akina nani

Shahidi: ambao nilikuwa nawafahamu walikuwa ni Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya

Matata: Baada ya Kukusomea Mashtaka Hayo, huyo Hakimu Simba alikwambia Nini?

Shahidi: Nikijaribu Kunyoosha Mkono Mbele ya Hakimu Simba, Pale Kisutu aweze Kunipa Ufafanuzi Kuhusu hayo Mashtaka Ya Ugaidi, lakini akaniambia Kwamba Mahakama haina uwezo wa kunisilikiza

Matata: Baada ya Pale nini Kilifuata

Shahidi: Baada ya Pale Nilichukuliwa nikapelekwa Gerezani Segerea

Matata: Kule Segerea nini Kiliendelea..

Shahidi: Ndipo Nilipokutana na Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya Ambao Walikuwa wameshapelekwa Magereza muda Mrefu

Matata: Baada Ya Kukutana naye ilikuwaje

Shahidi: Baada ya Kuwa Nimefika Magereza Nilipelekwa Moja Kwa Moja kwenye Sehemu Inaitwa PUNISHMENT CELL

Matata: Kwanini Walikufikisha Kwenye Punishment Cell

Shahidi: Nahisi Kwa sababu Ya Kesi iliyokuwa Inatukabali, Hatukuwahi Kuambiwa sababu Za Msingi ambazo Zilipelekea sisi Kufikishiwa Punishment Cell

Matata: Unasema Ulionana na Mohammed Ling'wenya Ikawaje Sasa

Shahidi: akaanza Kunieleza Namna walivyoapata Matatizo, KUTOKA Moshi Mpaka Walipofikishwa Tazara na Baadae Mbweni

Matata: Ni Lini tena ukirudi Mahakamani

Shahidi: Kutoana Janga la Corona Mahakama Zilizokuwa zinaendelea ni Kwa Njia ya Mtandao, Tulikuwa tunachukuliwa Kwenye Vyumba Vyetu na Kupelekwa Kwenye Mahakama ya Mtandao

Matata: Ni Hakimu gani alikuwa anaendesha Kesi yenu

Shahidi: Alikuwa ni Hakimu Simba na Pale ambapo Hayupo anaudhuru basi Walikuwa wa nahairisha Mahakimu wengine

Matata: Kutoka na Janga La Corona Ulikaa Muda Gani Segerea Kabla Ya Kurudi tena Mahakamani

Shahidi: Baada ya Kumuomba Sana Hakimu Simba Na Kumshimikiza Kwamba Tunashida zetu tunaomba Kwenda Mahakamani, na pia tuliomba Kumuona Mkuu wa Gereza

Tulifanikiwa Kumuona Hakimu Siku Ya Mwisho kwa Kukubaliwa Kwenda Kwa Hakimu Simba, Tulimuomba Hakimu Simba suala la Kukaa Kule Punishment Cell Lakini Akajibu Kwamba Hilo suala Lipo Juu Magereza Wenyewe.

Matata: Ukitumia Muda gani Mpaka Kwenda Kuonana na Hakimu Simba

Shahidi: Sikumbuki lakini Najua baada ya Kulalamika sana Na Kumuona Mkuu wa Gereza tukaenda Mahakamani

Matata: Ulikuja Kwenda lini Tena Mahakamani

Shahidi: Tarehe 27 July 2021, Tulifika Mahakamani, Hakimu akasema Kwamba Serikali haina Nia ya Kuendelea na Shauri Letu, Nikatolewa Mimi, Kaaya, pamoja na Khalid

Matata: Wewe Uliwafahamu Vipi

Shahidi: Baada ya Kuomba Kufikishiwa Mahakamani na Kuonana Na Mkuu wa Gereza Ndipo Nilipo Pata nafasi ya Kuwaona Na Kuwafahamu

Hawa wengine Nilikiri Kwa sababu Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Na Khalfani Bwire Nilifanya nao kazi, Pia Wale walikuwa Ukonga Mimi Nilikuwa Segerea kwa hiyo Siku Tulipopata Fursa Ndiyo Niliwaona

Matata: Sasa Kwa Ujumla Mlikuwa Washtakiwa wangapi Shahidi Kesi ya Uhujumu Uchumi namba 63 tulikuwa Sita na Mimi Nikiwa ni Mshitakiwa Wa Sita. Walikuwa nani na nani

Shahidi: Khalfani Bwire, Mohammed Ling'wenya, Adam Kasekwa, Justin Kaaya, Khalid na Mimi Wa sita

Matata: Sasa hii Tarehe 27 Mlienda Mahakamani, Ila Kuna Kitu Ulizungumzia Kuhusu Tarehe 26

Shahidi: Tarehe 26 July 2020 Tulipata Taarifa Kwamba Mheshimiwa Mbowe amekamatwa na Yupo Gerezani Ukonga Kupitia Vyombo Vya Habari

Matata: Ikawaje Shahidi: Tarehe 27 July 2021 tukaitwa Mahakamani na Baada ya Kusomwa Shauri Letu, Sisi tukawa Huru Siku hiyo

Matata: Shahidi Ilikuwaje Leo Mpaka Ukaja hapa Kutoa Ushahidi

Shahidi: Taarifa Nilipata Kutoka Kwa Mama yake Mohammed Abdilah Ling'wenya

Matata: ambaye anaitwa nani

Shahidi: Somebody SALOME

Matata: anaishi Wapi

Shahidi: Anaishi Mombasa Ya Banana Kama Unaenda Ukonga

Matata: ambayo Ipo Mkoa Gani

Shahidi: Ipo hapa hapa Dar es Salaam

Matata: Akakwambia nini

Shahidi: Kwamba amewasiliana na Wewe Wakili Matata Kwa Shauri la Kesi Ndogo Ya Mohammed Abdilah Ling'wenya, Aliniunganisha na wewe, Tukaonana Jana Na Ukanipa Maelekezo Ya Namna ya Kufanya.

Shahidi: Nilifika Tarehe 23 September 2020

Matata: Shahidi Ikumbushe Mahakama Kwamba Ukifika lini Tazara

Shahidi: Nilifika Tarehe 23 Mwezi September 2020

Matata: Sasa Nataka Nikuonyesha Detention Register unionyeshe Siku hiyo ya Tarehe 23 September 2020 kama Jina lako Lipo

Jaji: upande Wa Serikali mnasemaje

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji, Ni kitu gani Kinatanguloa Kabla hajamuonyesha Shahidi Kielelezo, Sisi tunaona hajajenga Misingi bado...Tunaona itakuwa ainakiuka Utaratibu, Na Ilitakiwa Misingi yenyewe Ijengwe Kwa Either anakifahamu Kitabu Hicho au Moja kwa Moja Kina Exist.. Misingi hiyo hajajenga, Tunaona akataliwe unless ajenge Misingi..

Matata: Mheshimiwa Jaji Sidhani Kama wakili yupo sahihi, Kielelezo hiki Kipo Mahakamani

Jaji: labda niseme Kwanza Kwamba Hiki ni Kielelezo ambacho Kipo Mahakamani, Mimi sioni shida Kwa Shahidi Kupewa hicho Kielelezo, Shida yangu Ilikuwa ni Juu ya Wakili Kumuonyesha Shahidi Tarehe Hiyo, Je atakuwa hamsaidii Shahidi Kutoa Ushahidi?

Wakili wa Serikali: Nadhani siyo Sahihi, Ampatie Kielelezo Ambacho Shahidi ataweza Kuulizwa M

Matata: Shahidi Shika hii Ni Detention Register naomba Utafute Tarehe ambazo wewe Ulipelekwa Tazara

Jaji: Kielelezo namba Ngapi P3

Shahidi: Sijaona Tarehe 23 September 2020

Matata: Kwa hiyo Jina lako Limo au Halimo

Shahidi: Sijaona Jina langu

Matata: Angalia pia Tarehe 24 na Tarehe 25 Siku Uliyoenda Mahakamani

Jaji: amesema apekue Upya

Shahidi anatafuta Tarehe 23 September 2020 kwenye Detention Register ya Tazara

Jaji: Sasa Upo Tarehe ngapi Shahidi: 18 July 2020

Shahidi: Nimefika Kwenye Tarehe 23 September 2020

Matata: Hapo Ulipofika Tarehe 23 September 2020 Kuna sehemu yoyote Kuna Jina lako?

Shahidi: Hapana Hakuna

Matata: Je Kwa Tarehe 24 September 2020

Shahidi: Wala Tarehe 24 September 2020 sijaona Jina langu

Matata: Na Tarehe 25 September 2020 Kuna Jina lako

Shahidi: Hapana Sijaona Jina Langu

Matata: Shahidi Unasema Ulipoenda Segerea Ulionana na Ling'wenya akasema amepata Matatizo, Je Alikwambia Matatizo Gani

Shahidi: Aliniambia Kwamba Walikamatwa Moshi, Wakaletwa Tazara na Baada ya Hapo Wakapelekwa Mbweni na Kisha Wakasomewa Mashtaka Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu

Matata: Na wewe Kwa sababu Ulikuwa Umeona naye kwa Mara Ya Kwanza alikuwa na Haki gani

Shahidi: Kiafya alikuwa Kawaida

Matata: Inavitu gani Kwamba Unaweza Kuthibitisha Ulikamatwa na Kupelekwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Shahidi: Vitu ambavyo ninaweza Kuthibitisha ni Nakala ya Commital, Ambayo Inaonyesha namna Niivyo Kamatwa na Kuletwa Mahakamani Tarehe 25 September 2020 Mpaka Nakuja Kutoka July 27 2020

Matata:Nakala ya Commital Ipo wapi

Shahidi: Nakala ya Commital Unayo wewe, Nilikupatia

Matata: Hiyo Nakala ya Commital ambayo umesema ninayo Mimi, Ipo wapi Sehemu Nyingine

Shahidi: Nilikupatia Kama Sehemu ya Kuambatanisha Ushahidi Wangu

Matata: Ushahidi Mwingine Ulionao Shahidi.? ukiacha hiyo Nakala ya Kumbukumbu, Kuna Kitu gani hasa ambacho Kinaweza Kuthibitisha Kwamba Tarehe 25 September 2020 Ulifikishwa Mahakamami Nakusomewa Mashitaka Ya Ugaidi

Shahidi: Ni Charge Sheet

Matata: Charge sheet Yako Ilikuwa wapi Shahidi: Nilikuwa nayo lakini baadae Ikapotea, Nikaenda Kwa Karani wa Mheshimiwa Simba Nikamuimba anipatie Charge Sheet

Matata: Ulipofika Kisutu Ilikuwaje

Shahidi: Nilipanda Kule Mara ya Mwisho Tukiposomewa Mashitaka, Nikamuona Karani wa Mheshimiwa Simba, inaonekana alikuwa na Vikao Vinaendelea Nikamuimba anipatie Nakala

Matata: Huyo Karani anaitwa nani

Shahidi: Simkumbuki Jina ila Mrefu na Mweupe, na Kwamba Hakimu ana vikao lakini Baada ya Kumtajia Kesi namba 63 ya 2020 alinikumbuka

Matata: Alikwambia Hakimu gani anaendelea na Vikao

Shahidi: Hakimu Simba, akaniambia niende Leo Asubuhi

Matata: Ikawaje

Shahidi: leo Asubuhi Nilienda Baada Ya Kuthibitisha ina muhuri wa Mahakama, Nikaja nayo Kutoa Ushahidi

Matata: Wakati Unakuja Huku hiyo Charge Sheet nani alikiwa nayo

Shahidi: Nilikuja nayo mimi

Matata: Kitu gani Kilikufanya Ujue Kuwa Charge Sheet hii ni sawa na Uliyopoteza

Shahidi: Kwanza Ina jina la Mahakama, Hakimu Makazi Kisutu Ina Namba ya Kesi 63/2020 Ina Muhuri Wa Mahakama, Ina majina ya Washtakiwa Sita tuliokuwa nao

Matata: Ikumbushe Mahakama Majina yao

Shahidi: ni Khalfani Bwire Adam Kasekwa Mohammed Ling'wenya Justin Kaaya Khalid Na Mimi Mshtakiwa Wa Sita

Matata: Kingine Kilichokufanya Utambue ni Nini

Shahidi: Ni Muhuri Wa Mahakama uliogongwa Leo pia Mashtaka tuliokuwa tunakabiliwa nayo Kuanzia Mshtakiwa Wa kwanza Mpaka wa Sita

Matata: Mashtaka Gani hayo

Shahidi: Kila Mtuhumiwa alikuwa na Mashitaka Yake, Mimi nilikuwa nashitakiwa Kwa Kufanya Mkusanyiko Usio halali..

Matata: Kuna Kingine?

Shahidi: Ni hizo tu

Matata: Baada ya Kuja nayo Hapa Ilikuwaje Kuwaje, Leo Asubuhi

Shahidi: Tulionana na wewe Wakili nikawa Nimekuonyesha, Kwa sababu Sitakiwi Kupanda nayo Hapa Kizimbani Nilikukabidhi na Kwa sababu Mahakama Ilikuwa inaendelea nikakuachia

Matata: Umeleta Kwanini Hii Hati Ya Mashtaka kwenye kesi hii

Shahidi: Nimeomba Mahakama Ipokee Kama Ushahidi

Matata: Kwanini Ulifuata Leo Mahakamani Kisutu Kuleta Hapa

Shahidi: Huo ndiyo Ushahidi Wangu

Matata: Nikikuonyesha Unaweza Kuitambua

Shahidi: Ndiyo Yenyewe

Matata: Kwanini Unasema Ndiyo Yenyewe

Shahidi: Nathibitisha Kwamba Ndiyo Yenyewe, kuna Jina La Mahakama Ya Kisutu Ndipo tuliopo fanyia Shauri Lakini pia Kuna Kesi Namba 63 ya Mwaka 2020

Matata: Kingine Kilichokufanya Utambue

Shahidi: Kuna Majina Ya Washitakiwa pamoja na Maeneo wakiyikwepo Kwa Maana Gerezani, Kingine ni Haya Mashauri tuliokuwa tunatuhumiwa nayo

Matata: Kingine

Shahidi: Ni Huu Muhuri ambao hata Ile Charge Sheet Niliyo kuwa nayo Mwanzo Ulikuwa nayo

Matata: Ungependa Mahakama I fanyie nini

Shahidi: Ningeomba Mahakama Ipokee Kama Ushahidi

Matata: Shahidi anaomba Nyaraka hii Ipokelewe Kama Ushahidi

Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji Sina Pingamizi

Paul Kaunda: Mheshimiwa Jaji Na sisi Kwa Upande wetu Hatuna Objection

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshitakiwa Wa Nne hatuna Pingamizi tunaona Ipokelewe

Sasa ni zamu ya Mawakili Wa Serikali, wamepewa hiyo Nakala ya charge sheet. Wameizunguka Charge sheet, wanaikagua kwa umakini, wanazungumza pale

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi

Jaji: Mahakama Inaipokea Hati hii ya Mashitaka Inayihusu kesi ya Uhujumu Uchumi iliyofunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Na Itakuwa ni Kielelezo D6

Matata: Mheshimiwa Asome Ukurasa wa Mwanzo na Mwisho

Shahidi ANASOMA

Shahidi Kamaliza Ukurasa wa Mbele na Nyuma

Matata: Ni hayo Mheshimiwa Jaji naomba Kuishia Hapo

Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wangu Sina swali la Dodoso Kwa Shahidi

Paul Kaunda: Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wetu Hatuna swali la Dodoso

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa Wa 4 pia Sina Swali

Wakili wa Serikali: Gabriel unaweza Kututajia majina yako Vizuri

Shahidi: Naitwa Gabriel Samheta Mhina

Wakili Wa Serikali: Unasema Wewe Ulikuwa Mwanajeshi

Wakili Wa Serikali: na Unasema Jeshi la Wananchi Uliingia Mwaka 2007

Shahidi: Ni sahihi

Wakili wa Serikali: Na pale Special Force unasema Ulienda Mwaka 2011

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Sasa Wakati Unaenda Mwaka 2011 hawa Watuhumiwa uliokuja Kukutana nao, Kati ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya yupi ulimkuta

Shahidi: Nilimkuta Khalfani Bwire na Mohammed Ling'wenya ila Huyu Dam Kasekwa ni Depoment Wangu, Yeye alikuja Moja Kwa Moja Tofauti na Mimi niliyo toka Kikosini

Wakili wa Serikali: Kwa Hiyo Mnafahamiana Vizuri

Shahidi: Ndiyo

Wakili Wa Serikali: Wewe Jeshini Uliachishwa

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: VIpi kuhusu hao Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya Na wao Pia waliachishwa

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Unasema Wewe Uliugua Ugonjwa Uliouita Brain Sarcastic Malaria

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: na Ulikaa Muda Mrefu Lugalo

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Hivi huu Ugonjwa ni Ugonjwa wa Akili

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Na Ukiumwa Ugonjwa wa akili ni Kitu unacho ambiwa Baadae au Unajua wewe

Shahidi: Unaambiwa wewe

Wakili wa Serikali: Sasa Huenda Kwamba Ulikuwa unafanya Vitu visivyo Vya Kawaida

Shahidi: Ndiyo nilikuwa naambiwa

Wakili wa Serikali: Ukiachana na hilo la Kutoroka na Kuondoka kabisa Kuna kingime

Shahidi: Hakuna

Wakili wa Serikali: Ni kweli Kwamba Ili utoke Kambini kwa Jambo lolote lile lazima upewe Ruhusa

Shahidi: Sahihi

Wakili wa Serikali: Nini Madhara ya Kutoroka kazini, Hatu gani zinaweza Kuchukuliwa

Shahidi: Ni Kuadhibiwa

Wakili wa Serikali: ila adhabu ya Kifungo Ulichopewa Ilitokana na Utoro?

Shahidi: Sahihi Kabisa

Wakili wa Serikali: Lakini Ile adhabu iliyopelekwa Kufungua Kule Jeshini Haikupelekea Kufukuzwa kazi

Shahidi: Haikwendana na Kufutwa Jeshini

Wakili wa Serikali: Wakati Unatoa Ushahidi Wako, Naomba utoe Ufafanuzi Kwamba Ni Jinsi Gani Ulipata Taarifa ya Kuachishwa kazi, Ilikuwa Tarehe ngapi

Shahidi: Tarehe 26 April 2020

Wakili wa Serikali: Taarifa hizo zilikufikiaje wewe

Shahidi: Nilipewa Taarifa na Rafiki Yangu Aliyekambini 92 Kikosi cha Jeshi

Wakili wa Serikali: Na wakati huo Wewe Ulikuwa wapi Wakayi Unapewa Taarifa

Shahidi: Nyumbani Tabora

Wakili wa Serikali: Pale kikosini 92 Kj Ulitoka Lini

Shahidi: Sina Kumbukumbu Vizuri, lakini Baada ya Kutoka kifungoni Mkuu wa Kikosi alinihaidi Kuwa akai na Mtu Mwenye tatizo kama hilo

Wakili Wa Serikali: Mwaka?

Shahidi: Ni 2020

Wakili wa Serikali: Unataarifa Yoyote Ya Maandishi Inayoonyesha Kwamba ulifukuzwa Kazi Kwa Huo ugonjwa

Shahidi: Sina Taarifa Yoyote

Wakili wa Serikali: Wakati Rafiki yako anakupa Taarifa Ya Kuondoshwa Jeshini Uliwahi Kufuatilia pale 92Kj kuhusu Usahihi wa hiyo Taarifa

Wakili wa Serikali: Hukusema Kwamba Utovu wa Nidhamu wa Jambo gani

Shahidi: Utovu wa Nidhamu

Wakili MATATA: Mheshimiwa Jaji Swali hilo Halipo Sawa, Mr Kidando anauliza as if Mimi Sikuuliza

Jaji: lakini Umesikia Jibu la shahidi anasema Kwamba hakuongozwa

Wakili wa Serikali: Upo Vizuri kwa Kumbukumbu?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Je, Ulisema Kwamba Ulirudi tena kwa Chief Personnel

Shahidi: Ndiyo Nilisema

Wakili wa Serikali: Kwa sababu Huna Barua Je Unaweza Kufahamu Ni sababu ipi iliyopelekea Kufukuzwa Kwako kazi Jeshini

Shahidi: Nimesema Kwamba ni Utovu wa Nidhamu

Jaji: Basi Kama Una amini Ulimuongoza Usiwe na Wasiwasi Ipo Kwenye Kumbukumbu

Wakili Wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Pia Jibu la Kwamba Sikuongozwa liingie

Jaji: Sawa

Wakili wa Serikali: Kufukuzwa Jeshi Kulikuja baada ya Kifungo

Shahidi: ndiyo

Wakili wa Serikali: Na Kifungo Kilitokana na Utoro

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Sasa wewe Unasema Kwamba Ulikamatwa Tabora Tarehe 19 September 2020

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Wakati wote huo walikuwa Wa nakuuliza Kama Unamfahamu MH Mbowe

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Ilikuwa wapi

Shahidi: Tazara

Wakili wa Serikali: Ilikuwa Tarehe ngapi

Shahidi: sikumbuki

Wakili wa Serikali: Ni kweli kwenye Ushahidi wako Hakuna Mahala umetaja hata Askari Mmoja aliyekukamata

Shahidi: Nimetaja

Wakili wa Serikali: Mimi Nakumbuka Ulisema Kwamba Askari Waliokukamata ni Wawili

Shahidi: Ndiyo nikataja na Majina

Wakili wa Serikali: Pale Tabora Wakati Wanakuja ata ni Kweli Hukutaja Askari aliyekushikia Bastola

Shahidi: Ni sahihi Sikutaja Kwa Sababu Sikuwa namfahamu kama Wengine

Wakili wa Serikali: Rafiki yako alivyokupigia Simu ili chukua Muda Gani Kufika pale

Shahidi: Muda Mfupi, Ulichukua Muda

Wakili wa Serikali: Je Rafiki yako Ulionana naye?

Shahidi: Hapana Nilipokaribia tu Nilikamatwa

Wakili wa Serikali: Je Baada ya Kutoka Jela Umeonana naye

Shahidi: Hapana tangu nitoke Jela Sijarudi Tabora

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Umesema Kwa Sasa Shughuli zako ni Mkulima?

Shahidi: Ndiyo Wakili wa Serikali: Kuna Kitabu ulikuwa unakikagua

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Ni Kitu gani Kile

Shahidi: Ni Kitabu Kinachotakiwa Kuthibitisha Mtu anapotoka Mahabusu

Wakili wa Serikali: Wewe ulisaini

Shahidi: Hapana Mimi nilishatoka mahabusu

Wakili wa Serikali: Hiki Kitabu ambacho Umekiita Cha Kuonyesha Mahabusu na Kutoka, wewe Ulikifahamu lini

Shahidi: Muda Mrefu

Wakili wa Serikali: Kabla ya Kukamatwa au Baada ya Kukamatwa

Shahidi: Kabla ya Kukamatwa, Sisi si tupo Kwenye system za kijeshi, Hizo ndiyo Taratibu

Wakili wa Serikali: Wewe Umejuaje Kama Kile Kitabu ni Cha Tazara

Shahidi Kwa Kuangalia watu wanaoingia na Kutoka

Wakili wa Serikali: Wewe Ulikamatwa Tabora Je ulikiona

Shahidi: Sikukiona kwa Sababu Mimi nilipitishwa Moja kwa Moja Mahabusu

Wakili wa Serikali: Je wewe KAMA Mahabusu Kuna Siku Nyingine Ulikiona

Shahidi: Mimi Nipo Mahabusu, Nitakiona Vipi Mle ndani

Wakili Wa Serikali: Ni kweli Kwamba Umekiona Mara ya Kwanza Leo Mahakamani

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Kile Kitabu umekagua Kurasa Ngapi

Shahidi: nimekagua Kurasa ambazo nimeelekezwa

Wakili wa Serikali: umeongea hapa Mahakamani Kwamba Mahabusu Uliwakuta Mahabusu wangapi

Shahidi: Ndiyo nimeongea

Wakili wa Serikali: Je ulitaja Majina yao Mahabusu uliokutana nao Tazara?

Shahidi: Mimi nitawajulia wapi? Kwani nimetolewa Tabora nije kuwajua Mahabusu wa Dar es Salaam?

Wakili wa Serikali: Mhe Jaji naomba anijibu swali langu, Je Ulitaja majina

Shahidi: Sikutaja kwa sababu siwafahamu, Ila Nilitaja Idadi

Wakili wa Serikali: Wakati Umepekua Kitabu, Ulikuwa unakagua Jina gani

Shahidi: Jina langu Kwa sababu Nilikamatwa Pekee yangu

Wakili wa Serikali: Hicho Kituo cha Tazara ni Mara ya Ngapi Ulikuwa unafika

Shahidi: Nilikuwa Sijawahi Kufika ni Mara Yangu Ya Kwanza

Wakili wa Serikali: Hukusema Kwamba wewe Ni Mwenyeji wa Dar es Salaam

Shahidi: Sikusema hivyo

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba nikomee hapo, Wakili Abdallah Chavula aendelee

Wakili wa Serikali: Nimesikia wakati Unaelezea Hati ya Mashtaka, Kwamba pembeni kumeandikwa magereza waliokuwa wanakaa..

Shahidi: Sahihi

Wakili wa Serikali: Ni Ushahidi Wako Kwamba wewe Tarehe 25 September 2020 Uliposomewa Mashitaka Ulichukukiwa Ukapalekwa Gereza la Segerea

Shahidi: Sahihi

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Kwamba Ulipofika Mlikaa Sehemu Moja, Ni sahihi

Shahidi: Siyo Sahihi hatukukaa sehemu Moja

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Wakati Mpo Segerea Mohammed Ling'wenya Alikueleza Yaliyo Msibu Moshi Mpaka
Anafika Segerea

Shahidi: Sahihi

Wakili wa Serikali: Shahidi Angalia hii Nyaraka, Je Unaitambua

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Nyaraka Hii, Gabriel Mhina anasomeka Yupo Gereza Gani

Shahidi: Segerea

Wakili wa Serikali: Mohammed Ling'wenya anasomeka Gereza gani

Shahidi: Ukonga

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Nyaraka Hii Adam Kasekwa anasomeka Gereza gani

Shahidi: Ukonga

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Nyaraka Hii Khalfani Bwire anasomeka GEREZA gani

Shahidi: Ukonga

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Kwamba hujaeleza Mahakama Nini Kilichotokea Maeneo Yaliyotokea Kwamba Kwa nini Kuna tofauti ya Mohammed Ling'wenya Yupo Gereza lingine

Shahidi: Kweli

Wakili wa Serikali: Miaka yako ni Mingapi

Shahidi: 34

Wakili wa Serikali: Umezakiwa Mwaka Gani

Shahidi: 1988 WS: Umeanza Darasa la Kwanza Mwaka gani

Shahidi: 1995

Wakili wa Serikali: Una Elimu ya Kiwango Gani

Shahidi: Kidato cha Nne

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Kwamba Karani wa Kikosi alikuja Kukupa Fomu ya Kujaza Wewe Kuacha kazi

Shahidi: Sahihi

Wakili wa Serikali: Alikuletea Ukiwa sehemu gani

Shahidi: Kambini

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Kwamba Ujaeleza Mahakama Wewe Ulipokuwa unasaini Ulisaini Kitu gani

Shahidi: Ni kweli sijaieleza Mahakama

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Ujaeleza Mahakama kama Ulipokuwa Jeshini Uliugua Ugonjwa Ukiokufanya Uache kazi

Shahidi: Hilo nimeeleza

Wakili wa Serikali: Hata Baada ya Kuacha kazi

Shahidi: Hilo sijaieleza

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Wewe Uliugua huo Ugonjwa wa akili Mara Mbili

Shahidi: Ni sahihi Kabisa

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Kwamba Ulipokuwa unaugua walikuwa wanakukamata na Kukupeleka Kambini

Shahidi: Kweli

Wakili wa Serikali: Na Hospitali hiyo baada ya Fahamu zako Kurudi Ukajikuta ni Lugalo

Shahidi: Ni sahihi

Wakili wa Serikali: Na Mara zote Mbili ukitoka Lugalo ukiwa Umepona

Shahidi: Kweli

Wakili wa Serikali: Na hata mra ya pili ulipougua Fahamu ziliporudi ulijikuta Upo Hospitali Lugalo

Shahidi: Ni kweli

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Kwamba Walikuruhusu uondoke Baada ya Kuona Maradhi yako na Kurejea 92KJ

Shahidi: Kweli

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Kwamba Hujatoa Ushahidi Kwamba Ulipo rudi 92Kj Kwamba Uliugua Tena, mara ya tatu

Shahidi: Sikusema Kitu Kama Hicho

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Kama Ikikupendeza Naomba Tumalizie Kesho

MAWAKILI WA UTETEZI WANAPINGA

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Dakika 10 Mpaka 15

Jaji: Incharge Wa Magereza tunaweza Kupata Dakika 15?

Incharge Wa Magereza: (Cheo ni Staff sergeant): Inawezekana Mheshimiwa Jaji

Jaji: nakupa Dakika 15 umalizie

Wakili wa Serikali: Abdallah Ni sahihi Kwamba Unataka Mahakama Iamini Ulifungwa ukuwekwa Mahabusu Ukiwa Jeshini baada ya Kutoroka

Shahidi: Sijazungumzia Masuala la Mahabusu, Nimesema Nilifungwa

Wakili wa Serikali: Unasema Ulikamatwa Tarehe ngapi

Shahidi: Tarehe 19 September 2020

Wakili wa Serikali: Wakati Wote wote ni Siku Ngapi Mpaka unapelekwa Mahakamani ni Siku ngapi

Shahidi: Siku 6

Wakili wa Serikali: na wakati wote huo ulikuwa Chini ya Mateso

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Na Muda wote huo Hukuwa unakula kwa sababu Ulikuwa Umefungwa Pingu

Shahidi: Ndiyo, Nilikuwa Nashindwa Kula sababu ya Pingu na pia nilikuwa nahofia Nitashindwa kujiosha Baada ya Haja

Shahidi: Sijamkuta Mohammed Ling'wenya TAZARA

Wakili wa Serikali: Mlikuwa mnakutana naye wapi

Shahidi: Wakati wa Video Conference

Wakili wa Serikali: Mlikuwa mnakutana Wewe wa Segerea na Ling'wenya Wa Ukonga Wakati wa Video Conference

Shahidi: Hapana Mohammed Ling'wenya alikwepo Segerea nimeshalisema

Wakili wa Serikali: Umesema Segerea Ulikuwa Wapi

Shahidi: Punishment Cell

Wakili wa Serikali: Mlikuwa mnaruhusiwa Kukutana

Shahidi: Hapana, Tulikuwa tunakutana Wakati wa Video Conference na Kutembelewa na Wageni wetu

Wakili wa Serikali: Pamoja na Kwamba Kila Mtu anachumba Chake na Mnatoka kwa Sababu hizo, Ila Bado Uliona Taarifa Ya Mheshimiwa Mbowe Kukamatwa, Ulijuaje suala la Mheshimiwa Mbowe kukamatwa

Shahidi: Kule Punishment Cell Tunapata Magazeti, Kuna Askari Magereza na Wafungwa wanakuja kutuhudumia

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo ni askari magereza na Wafungwa siyo vyombo vya habari

Shahidi: Kwani magazeti siyo vyombo vya habari?

Wakili wa Serikali: Gazeti gani?

Shahidi: Jamhuri Wakili wa Serikali: la tarehe ngapi

Shahidi: la tarehe 27

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji sina swali

Matata: Shahidi Umeulizwa Swali Kuhusu Kielelezo Hiki D6 Kwamba Huyu alikuwa wapi na huyu Wapi, Je eleza Mahakama Kwamba Huku kwenye Majina Kumeandikwa kwa nini na Huku kwenye Magereza Kumeandikwa kwa nini

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji hatujauliza Hivyo

Matata: Shahidi Ifafanulie Mahakama Wakati Wakili wa Serikali anakuhoji alikuuliza kama Kumeandikwa kwa pen au lah

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Tunapinga na hilo

Peter Kibatala: Miye sioni Ubaya wa hilo swali

Jaji: Hebu rudia Swali lako sababu nini kilichoandikwa haikuwepo kwenye Examination inchief na Cross Examination..

Matata: Hapa Mbele ya haya Majina Kuna sehemu Zina Majina ya Ukonga, Segerea ni Nini hiki?

Shahidi: Majina Ya Magereza Waliyopelekwa

Jaji: Bwana Mhina tunakushukuru , Asante nafikiri tumemalizana..

Wakili wa Utetezi Fredrick Kihwelo: Upande wetu Tumemaliza na Huyu ndiye shahidi wetu wa Mwisho Katika Kesi Ndogo

Jaji: Mmefunga Ushahidi

Wakili Fredrick Kihwelo: Ndiyo Mheshimiwa Jaji

Jaji anaandika Kidogo

Jaji: Mahakama Inaridhia Kufungwa kwa Utetezi Katika kesi Ndogo kuhusu Mshtakiwa wa tatu katika kesi Ndogo..

Wakili wa Serikali: Mhe Jaji naomba tuwasilishe SUBMISSION yetu ya hii kesi Ndogo na Kama utaridhia naomba tulete lSUBMISSION kwa Njia ya Maandishi Siku ya Tarehe 07 December 2021

Na Kwa sababu siyo Majibizano Tunaomba Kila Upande Tarehe hiyo walete Ya Kwake

Wakili Fredrick Kihwelo:
Mheshimiwa Jaji hatuna na Schedule, Ila tunaomba Proceedings Za Trial Within Trial Kwanza

Jaji: Changamoto sina hakika kama nimeziprint, tunafanyaje?

Wakili Fredrick Kihwelo: Sawa Mheshimiwa Jaji tunakubali Kuendelea hivyo hivyo

Jaji: na Uamuzi lini?

Wakili wa Serikali, Robert Kidando:
Tarehe 14

Jaji: basi tarehe 14/12/2021 ndiyo tutasoma uamuzi.. Naombeni Submission Kwa Hardcopy na softy Copy

Jaji: Kwa hiyo tunakubaliana Tarehe 07 Mtaleta Submission lakini Uamuzi wake Mahakama Itatoa Tarehe 14/12/2021

Jaji: Na Wakati Wote huo Washtakiwa Watakuwa Rumande chini ya Magereza, Nawatakia Maandalizi mema ya Submission

Jaji anatoka
 
Tupo live kumfuatilia Nyerere + Mandela wa nyakati hizi.

IMG_20211127_135750.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom