Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,717
- 13,467
Kama una maswali, maoni au mapendekezo kuhusu Usonji unaweza kuyaweka hapa kwenye jukwaa na yatawasilishwa au unaweza kuja kuuliza mojamoja kwenye mjadala na wataalam wa afya watayatolea ufafanuzi.
---
Mjadala umeanza
Ili kushiriki ungana nasi kupitia link hii: JamiiForums
JamiiForums
The Home of Great Thinkers Tumia Lugha ya Staha: Washiriki wanapaswa kutumia lugha ya kiungwana na kistaarabu ili kuhakikisha kuwa heshima na uvumilivu vinatawala katika mijadala Tofauti ya mawazo si uadui: Kubali kuwa na mawazo au majibu yenye kujenga na wala yasiwe makali yenye kumshambulia...
clubhouse.com
Dkt. Paschal Kang'iria: Usonji (#Autism) ni tatizo la kinafsi ambalo humpata Mtu. Mara nyingi huanzia Utotoni na huathiri uwezo wa Mtoto kufanya mawasiliano na wengine
Ktk hali hii ukuaji wa Neva hupelekea kuathirika kwa namna ambavyo Mtoto anapokea taarifa. Huanzia miaka 2 - 3
Saldeen Kimangale: Usonji unaweza kuwa na vyanzo vya Kibailojia ambapo mtu anakuwa na Vinasaba vinavyobeba ulemavu ambao unaathiri ukuaji wa Ubongo wake
Pia, Mtu anaweza kupata Brain injury ambayo inaweza kupelekea kupata hili tatizo. Tafiti zinaonesha Wanawake wanaojifungua wakiwa na miaka zaidi ya 35 huweza kusababisha Mtoto kupata tatizo
Dkt. Saldeen: Dalili za Usonji zimegawanyika katika makundi makuu matatu. Wanakuwa na ‘limited eye contact’, kuongea kwao kunaweza kuwa kwa maneno mafupi mafupi
Thinking process yao ipo slow. Kwa hisia zao, kuonesha furaha au huzuni ni ‘very limited’.
Dkt. Saldeen: Pia, wenye #Autism hisia zao huwa hawaoneshi sana. Unaweza kumuona nje ana furaha lkn ndani kumbe ana huzuni
Kwny tabia huwa na tabia ya kurudia rudia vitu hata katika namna ya kucheza. Anaweza kuwa na tabia za kujiumiza kama kujing'ata vidole au kujibamiza ukutani
Nazma Chagani: Mtoto wangu alipokuwa na miaka 2 ndipo niligundua kwamba ukuaji wake ulikuwa uko nyuma hata anapokuwa na Rafiki zake.
Pia, nilikuwa nikimpeleka sehemu ambazo kuna Watu wengi alikuwa akilia sana na kutapika lakini sikuwa naelewa ni tatizo gani.
Pia, hisia zao huwa hawaoneshi sana. Unaweza kumuona nje ana furaha lakini ndani kumbe ana huzuni.
Kwenye tabia huwa na tabia ya kurudia rudia vitu hata katika namna ya kucheza. Anaweza kuwa na tabia za kujiumiza kama kujing'ata vidole au kujibamiza ukutani.
Nazma Chagani: Nilimpeleka Nairobi na aliweza kufanyia Uchunguzi wa kina ndipo akagundulika kuwa na tatizo hili
Kama Mzazi una Mtoto mwenye Usonji hutakiwi kukata tamaa. Watoto wenye Usonji wanahitaji sana 'therapy' kila wakati.
Nazma Chagani: Mtoto wangu niligundua anaweza kuchora vizuri sana pamoja na kuogelea. Nilianza kuongeza nguvu ili kumpa nguvu zaidi kwenye hilo
Mpaka sasa ameendelea vizuri sana. Jambo la muhimu ni kuzingatia 'routine' yao, usimbadilishe vitu kila wakati kwani huwakasirisha
Hilda Nkabe: Autism tunasemaga ni Ugonjwa usio na dalili za kimwili hivyo hata Mtoto wangu sikugundua kwamba ana tatizo hilo kwasababu alikuwa akiendelea kukua vizuri na hata kuongea
Ilikuja kutokea ghafla tuu akaanza kukataa Chakula na kushindwa kupata choo hata siku 10
Hilda Nkabe: Tuliamua kumpeleka Shule kwa kuamini kwamba atachangamka akiwa huko kwasababu alichelewa kuongea
Nilipompelea kwa Mtaalamu alimpa tu peni. Watoto wengi wangeanza kuichezea ile peni lakini yeye hakufanya chochote, ndipo akagundulika ana tatizo la Usonj
Hilda Nkabe : Alikuwa anatumia nusu saa kuvaa soksi, unafundisha hivyohivyo taratibu. Nchi za wenzetu wameendelea sana hivyo ilisaidia sana kumfikisha Mwanangu hapa alipo
Tuliporudi Tanzania na kuona upungufu uliopo ndipo niliamua kuanzisha taasisi ya kusaidia wenye Usonji
Hilda Nkabe: Hatujui namna Sayansi inavyokwenda lakini mpaka sasa Usonji ni tatizo la kudumu kwenye Maisha ya Mtu
Kitu ambacho kinashughulikiwa ni zile dalili kwa kuangalia ni wapi ameathirika zaidi
Ukizishughulikia dalili zinaweza kuisha kabisa na nyingine hupungua.
Hilda Nkabe: Inawezekana sasa hivi tunasikia zaidi kuhusu wenye Usonji kwasababu labda ya Mitandao Watu wanapata Elimu hivyo wazazi wanatafuta matibabu
Lakini Mimi naamini kama ambavyo wanaokuja kutafuta matibabu wanaongezeka basi hata wanaopata #Autism pia wanaongezeka
Hilda Nkabe: Autism Awareness ni area ambayo inahitajika sana, Watoto hawa wanatakiwa kutambulika
Ifike mahali tuwaone wenye Autism kama watu wa kawaida. Awareness itapekea Acceptance
Dkt. Saldeen: Kwa Autism na related disorders tunachopigania ni equality of life. Wanao-improve ni wale ambao wapo mild, mara nyingi ni ulemavu wa kudumu
Watu wengi wenye Autism wana vipaji kupita kiasi. Mtu anaweza kuwa mchoraji, mwimbaji mzuri lakini ana Autism
Dkt. Saldeen: Autism ni tatizo la kudumu kwa Mtu ambalo linaweza kulinganisha na mwenye Ulemavu wa Viungo
Tunachopigania ni Quality of life hasa kama Mtoto hayupo kwenye 'Mild condition'. Kama anajing'ata tutajitahidi aache hiyo tabia ila haimaanishi kwamba tabia hiyo haitarudi
Dkt. Saldeen: Hii kwasababi ni Ulemavu wa Ubongo hivyo inakuwa ngumu kuweza kuondoa kabisa tatizo. Ndio maana tunapigania kuboresha Maisha yao
Wengi wenye Autism huwa wana vipaji kama Uchoraji, Mathematics. Hivyo Mzazi ajitahidi kuendelea kile kipaji ambacho ameona Mtoto anacho.
Paschal Daniel: Changamoto ya Afya ya Akili kwenye jamii yetu uelewa bado uko chini. Hata utunzaji wa Takwimu nao bado hauko sawa hivyo inakuwa ngumu kusema tatizo la #usonji kwa Tanzania liko vipi?
Tunashukuru kwamba Uelewa unazidi kuongezeka kwa jamii hasa Wazazi.
Godfrey Kimathy: Hakuna takwimu zinazoweza kutuonesha kwa namba idadi ya wenye Usonji wako wangapi
Lakini kwenye Kliniki zetu idadi ya Wazazi ambao wanakuja kupata huduma kwa ajili ya Watoto wao wenye Usonji imeongezeka
Kuganda: Kwa kweli takwimu haziko wazi, hata kwenye Wizara zetu ukienda bado hautapata kuona hizo Data
Kwenye idara zetu wanaokuja wengi kupata huduma ni wenye Kifafa halafu kundi linalofuata na wenye Usonji. Kwasababu hatujafanya tafiti hatuwezi kusema wenye Usonji ni wangapi.
Kinjama: Serikali ina juhudi inazoziweka, na tunaziona. Mwanzoni Wanafunzi wa Autism walikuwa wamejumuishwa kwenye kundi la watu wenye ulemavu, lakini sasa wamewekwa katika kundi maalum
Katika uwanja wa Elimu tunapokea Wanafunzi wenye Usonji. Sisi kwenye Elimu hatusemi Autism ni ulemavu
Kinjama: Wazazi wengi wanawaambia Watoto 'acha' badala ya 'fanya hivi'. Tunashauri usimwambia 'usi' mwambie 'fanya'. Wazazi wasiwe negative
Mzazi kama Mwanao ana Autism anakwenda Shule mwangalie. Wengine wanalia kwasababu kuna tabia hapendi
TOFAUTI YA USONJI NA MTINDIO WA UBONGO
Dkt. Isaac Maro: Mtindio wa Ubongo ni changamoto ambayo mtoto hupata kutokana na ajali au kabla hajazaliwa. Anakuwa na aina fulani ya mapungufu katika muonekano au namna ana-operate
Mpaka sasa hatujafahamu sababu hasa kwanini Watoto wanapata Usonji
KWA SASA WADAU WANAULIZA MASWALI MBALIMBALI
Swali
Haroun: Ningependa kufahamu uhusiano kati ya Autism na Vinasaba
Jibu
Kuganda: Vinasaba vipo vya kurithi, lakini si kweli kwamba kila mwenye hivyo vinasaba atapata Autism
Swali: Usonji na suala la kuoa na kuolewa
Hilda Nkabe: Kuna mtu anaweza kuwa kaolewa au kaoa na ana Autism lakini hajui. Watu wenye Usonji wanaweza kuolewa au kuoa, inategemea na severity.
Swali: Je mtoto mwenye Usonji anatakiwa kusoma shule maalum?
Dkt. Isaac Maro: Mtoto mwenye Mild Autism nashauri apelekwa Shule ambayo ina mchanganyiko lakini lazima Shule hiyo imtambue ana mahitaji maalum (Special needs)