Yaliyojiri katika maadhimisho ya Siku ya Watetezi wa Haki za Binadamu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,715
13,467
Kauli Mbiu inasema,
“kudai na kulinda nafasi ya kiraia mtandaoni kwa ajili ya kuboresha na kulinda Haki za Binadamu Tanzania.”

JamiiForums yashiriki maadhimisho ya siku ya Watetezi wa Haki Tanzania, Maxence Melo atunukiwa Tuzo ya kinara wa Uhuru wa Kujieleza Mtandaoni
JamiiForums imeshiriki katika maadhimisho ya Tano ya Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

Mratibu wa THRDC Onesmo Olengurumwa amesema 'Siku hii ni jukwaa la majadiliano miongoni mwa watetezi wa haki za binadamu nchini pamoja na wadau wa maendeleo ili kuwatambua na kuwalinda watetezi hawa'

"Tanzania ina watu takribani milioni 52.6, ambapo kati yao watu milioni 23 wanatumia intaneti na mitandao ya kijamii. Watu wote hawa wanatumia intaneti na mitandao ya kijamii walau mara mbili kwa siku"

Mwakilishi kutoka Kampuni ya mawasiliano ya TTCL amesema wataendelea kutoa huduma bora ya mawasiliano kwa wananchi ili kuunga mkono jitihada za THRD COALITION katika kulinda na kutetea haki za binadamu kupitia mitandao ya kijamii.

Balozi wa Sweden nchini Tanzania, amesema wanawake ndio kundi ambalo haki zake zinakiukwa sana kupitia mitandao. Hivyo, watetezi wa haki za binadamu Tanzania wanapaswa kulinda na kuteteza haki za kundi hilo.

Balozi wa Norway nchini Tanzania amesema, Watetezi wa haki za binadamu sio maadui. Isipokuwa ni wadau muhimu katika maendeleo.

Mwakilishi kutoka Serikalini, Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi amesema, Serikali inatambua umuhimu wa matumizi ya mitandao na iko tayari kubadilisha sheria za mawasialiano kwa kadri ambayo mahitaji yanatokea.

WASHINDI

Walioshinda ni Maxence Melo kwa kupigania Uhuru wa Kujieleza Mtandaoni nchini Tanzania, Access now kwa kupigania Haki za Kidijitali duniani kwa mwaka 2018

Wengine ni CIPESA kwa kupigania Uhuru wa Mtandao Afrika, Mwanablogu Friday Simbaya kwa kupigania Haki za Binadamu kupitia blog ya mtandaoni

Maria Sarungi Tsehai ametambuliwa kwa kutetea Haki za Binadamu kupitia Twitter, Millard Ayo ametambulika kwa kuwa kinara wa Televisheni za Mtandaoni Tanzania

Mwandishi wa Habari za Uchunguzi, Salma Said ametambulika kwa kutetea Haki za Binadamu kupitia Facebook huku TTCL wakipewa tuzo kwa kuhakikisha upatikanaji wa internet ya kuaminika nchini Tanzania kwa mwaka 2018

THRDC.jpg

Picha ya Washindi kwa Pamoja

MJADALA: Kudai na Kulinda Nafasi ya Raia Mtandaoni kwa ajili ya kuchagiza na kulinda Haki za Binadamu nchini Tanzania

Maxence Melo

Miaka 5 iliyopita suala la “online civic space” lilikuwa halijaeleweka. Nafasi hii ni yetu na inabidi tuipiganie. Nafarijika kuwa tumeanza kuwa na mijadala hii.

Haki ya ‘Access’ ya mitandao imetolewa lakini naona kwa namna moja ama nyingine inavutwa; yaani inachukuliwa taratibu kupitia sheria na kanuni.

Mary Shao(TCRA)
Mitandao imesaidia kutoa ajira. Tumeona Millard Ayo, JamiiForums imeajiri watu pia . Changamoto inayotokea ni kuwa uelewa wa matumizi ya vifaa vya dijitali. Pia kuna matumizi yasiyo sahihi kama wizi na utapeli, udhalilishaji hususani kwa wanawake.

Fursa zipo mtandaoni lakini kila atumiaye mtandao anatakiwa ajue kuna wajibu. Kuna haki lakini pia kuna wajibu. Haki haiendi bila wajibu

Maxence Melo
Sheria ya Ulinzi wa Data ni muhimu sana. Imegundulika mtu akiwa na 50,000 au Laki 1 anaweza tu kupata taarifa zako kutoka mitandao ya simu. Tunapotakiwa sasa kusajiliwa kwa fingerprints tunategemea TCRA kama walinzi wetu watulinde sisi walaji.

Tunaongea kuwa wanawake wanadhalilishwa kwenye mitandao lakini hata Wanaume tunadhalilishwa. Pia TCRA inapaswa kutulinda kuhakikisha tunapata haki yetu. Ukisema kutojua sheria sio kinga wakati zinatungwa sheria bila kutushirikisha, ni kutuumiza.

Internet Society
Msingi wa kila kitu ni Wananchi, kuna shida naiona hapa. Mtu mwenye kujiona mtawala hawezi kuwashirikisha wananchi katika kutunga sheria. Sheria yoyote yenye harufu ya ukandamizaji ukiichunguza haitokani na kushirikisha Wananchi.

Watawala (ambao si viongozi) mara nyingi wanakuwa na kitu kinaitwa ‘fear of unknown’. Mara nyingi wanakuwa wanatumia sheria mbalimbali kujilinda wao wenyewe

Maxence Melo
Mamlaka zetu mara nyingi wakitaka kutunga Sheria au Kanuni wanaita wadau kutoa maoni lakini huwa ni kwa ajili ya picha tu kwani hurudi na kile walichokiandaa wao bila kuzingatia maoni.

Taarifa nyingine ya tukio:-

 
maria sarungi the great... kwanini bi Fatuma Karume hayupo she is real stronger
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa kweli tunamshukuru sana Maxence Melo kwa kutupatia sehemu ya kupunguzia hasira zetu, tunakuombea kwa Mungu azidi kukubaliki na kukupa maisha marefu ili tuendelee kupata mahali pa kupatia hewa nzuri
 
Shangazi, Halima Mdee na Maria Tseshai Sarungi nawapenda sana hawa wadada kwa kusimama imara dhidi ya hii serikali dhalimu pamoja na vitisho mbali mbali kwao.

maria sarungi the great... kwanini bi Fatuma Karume hayupo she is real stronger
 
Back
Top Bottom