Picha ya pamoja ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Wakuu wa Mikoa baada ya kuwaapisha wakuu wa Mikoa, Kamishena Mkuu wa Mamlaka ya Mapata Tanzania na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam Marchi 15,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Kamishena Mkuu wa Mamlaka ya Mapata Tanzania Ndg. Alphayo Japani Kidata na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Kamishna wa Polisi Valentino Longino Mlowala (waliosimama) Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kuwaapisha Marchi 15,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John .P. Magufuli anawaapisha wakuu wa mikoa wateuliwa kabla ya kuanza rasmi shughuli zao za kiutendaji.
Rais Magufuli ameongelea suala la wafanyakazi hewa kwenye Halmashauri zote nchini, amewapa siku 15 wakuu wapya wa mikoa kuhakikisha hakuna wafanyakazi hewa katika Halmashauri zote nchini.
Rais Magufuli wafanyakazi hewa, vijana wafanye kazi watakao kataa wapelekwe kwenye makambi wakafanye kazi, awaagiza wakuu wa mikoa ndani ya siku 15 kuhakikisha hamna wafanyakazi hewa katika mikoa yao
Rais Magufuli amewataka wa kuu wa mikoa hao kuhakikisha hakuna vijana ambao watakuwa wanakwenda kucheza pool table asubuhi na badala yake vijana hao wanatakiwa kufanya kazi kweli kweli hata kwa kulazimishwa.
"Nimeamua kuwateua wakuu wa Mikoa nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri katika mikoa yenu, Napenda niwape pole kwa sababu mtakwenda kufanya kazi kweli kweli kutatua kero za wananchi wetu.
Lakini pia niwaombe wakuu wa mikoa mkasimamie watu wafanye kazi hasa vijana haiwezekani vijana leo hii unamkuta saa mbili asubuhi anacheza Pool table wakati wa kina mama wanalima shambani, kama hawataki kufanya kazi kwa kupenda walazimishwe kufanya kazi."
Rais Magufuli: Nimeamua kuwateua nyinyi kama wakuu wa mikoa nikiamini mtaniwakilisha vizuri popote.
Rais Magufuli: Wananchi Kusindikizwa na polisi maana yake hakuna usalama.
Rais Magufuli: Na hasa kutambua nyinyi ndio wenyekiti wa kamati za ulinzi na usalama mkaniwakilishe.
Rais Magufuli: Haiwezekani kwa nchi ambayo inajitawala miaka 50 raia wake wakisafiri wasindikizwe na polisi.
Rais Magufuli: Nataka Tanzania katika awamu yangu isitokee mahali mkuu wa mkoa anaomba chakula.
Rais Magufuli: Niwape grace time ndani ya siku 15 wakurugenzi wawe wamejumlisha wamewatoa wafanyakazi hewa katika payroll
Rais Magufuli: Mshahara wa mwezi tukigundua mkurugenzi amelipa mshahara hewa ajue hana kazi na tunampeleka mahakamani
Rais Magufuli: Singida na Dodoma ina wafanyakazi hewa 202
Rais Magufuli: Leo pia tumeapisha Kamishna mkuu wa TRA na kamanda wa TAKUKURU.
Rais Magufuli: Nyinyi mna mamlaka ya kuwaweka watu ndani hata masaa 48, kawawekeni wengi ili kusudi wajue kwamba wananchi wanatakiwa kuheshimiwa.
Rais Magufuli: Tusiogope kuchukua maamuzi, nafuu uchukue maamuzi hata kama ni mabaya yatarekebika huko mbele.
Rais Magufuli: Haiwezekani kila siku majambazi, kwa nini Rwanda hakuna majambazi, kwa nini Tanzania tu, mkafanye kazi.
Magufuli: Morogoro watu wanauana sana ndio maana sikuona sababu ya mkuu wa mkoa kubaki pale. 'Mesage sent and delivered'.