Bunge la 11, Mkutano wa tatu
Maswali na Majibu
Swali : Serikali inatoa kauli gani kuhusu kupeleka milioni 100 tuu kati ya 300 za kujenga daraja la Kihungwe wilayani Kilosa?
Majibu : Katika bajeti ya mwaka 2016/17 Serikali imetenga milioni 700 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.
Swali : Ni lini ujenzi wa barabara ya Itoni hadi Njombe utaanza?
Majibu : Maandalizi kwa ajili ya ujenzi wa barabara umeanza ambapo upembuzi yakinifu na usanifu wa kina unaendelea. Aidha juhudi za kumpata mkandarasi zipo katika hatua za mwisho.
Swali : Ni lini serikali itaipatia wilaya Kiteto mahakama ya baraza la ardhi kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi
Majibu : Wizara imepanga kuunda mabaraza matatu ya ardhi kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi, Pia kikosi kazi kimeundwa kwa ajili ya kushughulikia migogoro hiyo ya ardhi.
Aidha kuna Mpango shirikishi wa kupima mashamba zaidi ya 2000, pia kutoa elimu kwa wananchi.
Swali : Serikali imejipangaje kumaliza mgogoro ya ardhi?
Majibu: Kuandaa orodha ya inayoonesha migogoro ya ardhi na kuandaa fidia kwa waathirika wa ardhi.
Aidha halmashauri zinatakiwa kupima maeneo yote ya uma ili kuzuia uvamizi na migogoro.
Swali : Serikali ina mpango gani wa kupeleka afisa ardhi katika wilaya ya Rufiji?
Majibu : Mkurugenzi wa halamshauri ya manispaa ya Rufiji afuate utaratiibu kumpata afisa ardhi huyo.
Swali : Serikali inatoa kaulikuhusu kutoa fidia ya wananchi wa Kaliuwa ili waweze kupisha mradi unaoendelea?
Majibu : Tathmini ya wananchi 71 imefanyika na tayari wananchi 71 wamelipwa fidia na kampuni ya Chiko. Aidha wananchi ambao hawajalipwa fidia watalipwa hadi
Serikali imepanga kufanya tathmini na malipo kwa wananchi kabla ya mradi wa kuanza.
Swali : Je serikali imefanya tathmini kujua kama walimu tuu ndo wanasababisha mwanafunzi kushidwa kusoma na kuandika?
Majibu : Utafiti unaonesha mwalimu ana nafasi kubwa katika kumwezesha mwanafunzi katika stadi zake, mengine ni uwiano wanafunzi darasani, upatikanaji wa vitabu na ushirikaino wa wazazi.
Wizara inatoa wito kwa wazazi kuwapa ushirikiano ili waweze kutekeleza wajibu wao vizuri.
Serikali imetoa mafunzo kwa walimu 22,627 kwa ajili ya kuboresha uwezo wao.
Serikali inaweka utaratibu wa kuwatambua walimu wa darasa la kwanza na la pili.
Swali la nyongeza : Serikali imejipangaje kuzalisha wahitimu wenye viwango?
Majibu : Serikali itachukua hatua stahiki kwa taasisi zinazozalisha wahitimu hao
Swali : Je serikali iko tayari kutoa kibali kwa kila kijiji na mtaa kama kwa kampuni ya Sao Hill?
Majibu : Ugawaji unaongozwa na sheria ya misitu. Wizara imepokea maombi mengi kupita uwezo.
Kutokana na uchache wa rasilimali serikali inatoa vibali kwa makampuni yenye ubia na serikali na kwa baadhi ya wananchi wanaozunguka maeneo ya misitu.
Swali : Je serikali ina mpango gani wa kuboresha chuo cha afya na uuguzi Kibondo wilayani Muhambwe ili kiweze kukidhi mahitaji?
Majibu : Serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajilli ya kufanya ukarabati kupitia mfuko wa ufadhhili wa pamoja yaani basket Fund
Katika bajeti ya 2016/17 serikali imetenga bilioni 8 kuboresha vyuo vya afya nchini na chuo cha afya cha Kibondo kimetengewa milion 600 kwa ajili ya kukiboresha.
Swali : Je serikali haioni muda umefika wa kurekebisha sheria ya ndoa ya 1971 ambayo inaruhusu mtoto kuolewa akiwa na umri wa miaka 15?
Majibu : Serikali imeshaanza kufanyia marekebisha sheria hiyo na waraka umeshaandaliwa ambao kwa sasa upo katika baraza la mawaziri.
Swali la Nyongeza : Serikali ina mpango gani wa kutunga sheria ya kuzuia kubeba mimba kabla ya miaka 18?
Majibu : Ni suala lenye utata kidogo na wizara imechukua ushauri wake.