Zile enzi za A-level, nimerudi nyumbani msure hata likizo huwezi kukaa tu lazima uwende tuition sawa baba. Wakati huo ndio nimeanza kuwa na feelings na vijana, kuna handsome boy ndio ameanza kunipigia simu, ninaleta za sitaki nataka, nikiuliuzwa tutaonana lini? Si unajua niko busy.
Basi bwana ninatoka tuition, mitaa ya posta mpya ninasubiri dala dala la kurudi home, nikaamua kununu mihogo ya kukaanga, basi limekuja nimeingia na mihogo yangu nianze kula, khe kutuo cha mlaba mwekundu mkaka ameingia, kumuoana tu moyo ulikua powaa sasa mkaka anione ninakula mihogo kwenye bus, si nilitupa mihogo dirishani, tafuka kitambaa pangusa midomo, vaseline iko wapi tupia.. Alafu mihogo ilikuwa mitamu na mimi nimetoka boarding.