Yale yaliyotokea uchaguzi wa 2015 ndani ya CCM, yatajirudia Tena uchaguzi 2025

Hennes kolon

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
673
1,292
Uchaguzi wa 2015 ulikuwa mzito na mgumu Sana kwa CCM, kuanzia ndani ya chama kwenye Kura za maoni, na pia nje ya chama dhidi ya vyama pinzani.

Kwanza CCM walianza kugawanyika baada ya Mkwere kutaka Benard apite, lakni mpango ukagoma wajumbe wakaona bola waende na mzee Lowasa, lakini walipomkata Lowasa, wajumbe wakaona Sasa bola wakose wote, wakaamua kumpa asiyetarajiwa na wengi, akapita JPM.

Lowasa akaamua kuhama chama akaenda kupambana na JPM, mtanange ulikuwa mkali na mzito haswa.
haya naona yanaenda kujirudia tena, ikiwa tu CCM watashikilia ule utaratibu wao wa mwenyekiti hapigwi kwenye Kura za maoni ndani ya chama, na ukizingatia kwa Sasa Khali si shwari tena huko ndani.

Wajumbe kwa sasa wametulia tu, lkn wanalo moyoni Jambo lao, naogopa kwa Hali ilivyo kwa Sasa na jinsi mambo yanavyoenda kwa Sasa nchini, Yale yaliyotokea 2015, huenda yakajirudia 2025, na huenda ikawa ndo Mara ya kwanza ule utaratibu wao wa mwenyekiti hapingwi, ukavunjwa!!
 
enda yakajirudia 2025 ,na huenda ikawa ndo Mara ya kwanza ule utaratibu wao wa mwenyekiti hapingwi, ukavunjwa !!
Na iwe hivyo kwa afya ya taifa letu
 
Naelewa walundavyuma walivyomkamia mwenyekigoda.

Hatoboi
 
JK alikua sio mgombea 2015 so wangeweza mpinga maana hakuwa tena na mamlaka baada ya uchaguzi ila Samia Bado ni mwenyekiti na anapitisha majina ya wabunge 2025 so unadhani nani hapo atachukua fomu kumpinga si mtafutwa wote ubunge au ujumbe wa NEC!!

CCM hakunaga demokrasia ndio maana neno la mwenyekiti ndio mwisho, nakumbuka kipindi kile sukuma gang walisema hawatakubali Samia awe mwenyekiti ila akashinda kwa kura zote za Ndioo ndio sembuse sahivi alipojaza "vijana" wake kwenye idara zote nyeti?
 
Uchaguzi wa 2015 ulikuwa mzito na mgumu Sana kwa CCM, kuanzia ndani ya chama kwenye Kura za maoni, na pia nje ya chama dhidi ya vyama pinzani.

Kwanza CCM walianza kugawanyika baada ya Mkwere kutaka Benard apite, lakni mpango ukagoma wajumbe wakaona bola waende na mzee Lowasa, lakini walipomkata Lowasa, wajumbe wakaona Sasa bola wakose wote, wakaamua kumpa asiyetarajiwa na wengi, akapita JPM.

Lowasa akaamua kuhama chama akaenda kupambana na JPM, mtanange ulikuwa mkali na mzito haswa.
haya naona yanaenda kujirudia tena, ikiwa tu CCM watashikilia ule utaratibu wao wa mwenyekiti hapigwi kwenye Kura za maoni ndani ya chama, na ukizingatia kwa Sasa Khali si shwari tena huko ndani.

Wajumbe kwa sasa wametulia tu, lkn wanalo moyoni Jambo lao, naogopa kwa Hali ilivyo kwa Sasa na jinsi mambo yanavyoenda kwa Sasa nchini, Yale yaliyotokea 2015, huenda yakajirudia 2025, na huenda ikawa ndo Mara ya kwanza ule utaratibu wao wa mwenyekiti hapingwi, ukavunjwa!!
Hamna mjumbe mwenye jeuri ya kufurukuta mbele ya mwenye kiti cha enzi huko CCM!! Hao wote mbwa mwitu wenye njaa kali....hawana lakufanya mbele ya bwana wao awapaye minofu
 
Uchaguzi wa 2015 ulikuwa mzito na mgumu Sana kwa CCM, kuanzia ndani ya chama kwenye Kura za maoni, na pia nje ya chama dhidi ya vyama pinzani.

Kwanza CCM walianza kugawanyika baada ya Mkwere kutaka Benard apite, lakni mpango ukagoma wajumbe wakaona bola waende na mzee Lowasa, lakini walipomkata Lowasa, wajumbe wakaona Sasa bola wakose wote, wakaamua kumpa asiyetarajiwa na wengi, akapita JPM.

Lowasa akaamua kuhama chama akaenda kupambana na JPM, mtanange ulikuwa mkali na mzito haswa.
haya naona yanaenda kujirudia tena, ikiwa tu CCM watashikilia ule utaratibu wao wa mwenyekiti hapigwi kwenye Kura za maoni ndani ya chama, na ukizingatia kwa Sasa Khali si shwari tena huko ndani.

Wajumbe kwa sasa wametulia tu, lkn wanalo moyoni Jambo lao, naogopa kwa Hali ilivyo kwa Sasa na jinsi mambo yanavyoenda kwa Sasa nchini, Yale yaliyotokea 2015, huenda yakajirudia 2025, na huenda ikawa ndo Mara ya kwanza ule utaratibu wao wa mwenyekiti hapingwi, ukavunjwa!!
Kwenye uongozi kunatakiwa IQ ya kiongozi iwe juu ya wastani wa Taifa la Tanzania. Labda wakati huo hili wazo litakuwa pande zote, CCM na kwenye Vyama vya Upinzani. Tupate kiongozi mwenye viwango na siyo Bora kiongozi!
 
Uchaguzi wa 2015 ulikuwa mzito na mgumu Sana kwa CCM, kuanzia ndani ya chama kwenye Kura za maoni, na pia nje ya chama dhidi ya vyama pinzani.

Wajumbe kwa sasa wametulia tu, lkn wanalo moyoni Jambo lao, naogopa kwa Hali ilivyo kwa Sasa na jinsi mambo yanavyoenda kwa Sasa nchini, Yale yaliyotokea 2015, huenda yakajirudia 2025, na huenda ikawa ndo Mara ya kwanza ule utaratibu wao wa mwenyekiti hapingwi, ukavunjwa!!
Mkuu Hennes kolon , kwanza naheshimu mawazo yako, ila CCM ni chama kinachoheshimu sana taratibu zake!, kama Mwenyekiti hapingiwi ni uteuzi wa mserereko, ni Mwenyekiti hapingwi!

Ila 2025 ni Mwenyekiti mwenyewe atasema imetosha na kupendekeza jina moja la ile nafasi yake!, hivyo utaratibu wa fomu moja na jina moja utaendelea.

Ila hili litafanyika only if kama HII ni sauti ya kweli ya kwake YEYE, hii ina maana huyo YEYE aliyeniambia mimi, pia atamwambia na yeye, hivyo atachukua ile fomu moja na kumpa mwingine ndie ajaze na CCM itamkubalia huyo mwingine!. Kama Sauti Hii ni Sauti ya Kweli, Nimeelezwa Mpango Ndio Mpango Mzima!. Swali ni... Akiwa Mkristo, Kwanini ni Lazima Awe Mkatoliki?!.

P.
 
Back
Top Bottom