Yakiwa Yamebaki Masaa Machache; Tupate dondoo mbili tatu kuhusu Mtibwa Sugar.

sembo

JF-Expert Member
May 25, 2011
4,350
3,451
1. Aliyekua kocha na mchezaji wa mda mrefu wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime alijiunga na Kagera Sugar kwa ajili ya Msimu huu wa 2016/2017 kama Kocha Mkuu.. Nafasi yake ilichukuliwa na Salum Mayanga.

2. Katika Msimu huu, Mtibwa Sugar wameondokewa na wachezaji takribani 5 wa kikosi cha kwanza.
Wachezaji hao na timu walizokwenda ni


Shiza Kichuya, Ibrahim Mohamed na Mzamiru Yasini walisajiliwa Simba SC, Vicent Andrew aliyesajiliwa Yanga SC na Hussein Sharif aliyemfata Mecky.

3. Baadhi ya wachezaji walioletwa kuziba mapengo ya walioondoka ni


Rashid Mandawa toka Mwadui FC, Cassian Ponera toka Ndanda FC na Haruna Chanongo toka Stand United.

4. Matokeo ya wakata miwa hao wa Manungu ni haya hapa
20/08/2016: Mtibwa Sugar 0 - 1 Ruvu Shooting
27/08/2016: Mtibwa Sugar 2 - 1 Ndanda
03/09/2016: Maji Maji 1 - 2 Mtibwa Sugar

Ikumbukwe leo [11.09.2016] mida ya saa 10 jioni, Simba SC itakua inapambana na hawa jamaa.

Wito wangu kwa mashabiki na wanachama wa wenzangu wa Simba SC tujazane kwa wingi Shamba la Bibi, pia wale wazee wenzangu wa vibanda umiza tunatakiwa tuwahi siti zetu mapema maana hii mechi tunaimaliza "mapema sana".

SIMBA SPORTS CLUB, NGUVU MOJA.
 
Leo ngoma ni draw au mtu mzima kuumbuka mchana kweupe. Mtibwa go gol goli.
 
Leo ngoma ni draw au mtu mzima kuumbuka mchana kweupe. Mtibwa go gol goli.

Mkuu unazungumzia hii mechi;

11/09/2016: Simba SC Vs Mtibwa Sugar

au nyingine? Kama ni hii Mtibwa hawana chao leo.
 
Na gazeti bora kwa sasa la michezo "MwanaSOKA" lina yapi ya kusema kuelekea mechi ya leo??

1473574699881.jpg
 
Back
Top Bottom