Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,796
- 14,131
Kiongozi mkazi wa Hamas ndani ya Gaza ameibuka kwa mara ya mwanzo tangu mashambulizi ya oktoba 7 na kusema jeshi lake linapigana vita vikali na ambavyo havijawahi kutokea.
Matamko yake hayo yamekuja kwa njia ya maandishi na kuonesha ni matamko ya muda unaoendelea ametoa matamko kuashiria mipango ya Misri kutaka kumaliza vita hivyo ambayo ndiyo kwanza yanaanza kujadiliwa.
Sinwar ameahidi askari wake kuwa wataliangamiza jeshi la Israel na kwamba hawana mpango wa kuridhia mashariti ya Israel katika kumaliza vita hivyo.
katika tamko lake amesisitiza kuwa askari wa Israel waliouliwa na Hamas ni zaidi ya elfu moja na kwamba wametia hasara kubwa kwa kuharibu vifaa vya kivita vya jeshi hilo.
Wiki mbili zilizopita jeshi la Israel lilitangaza kuizingira nyumba ya Yahya Sinwar na kwamba wakati wowote wangekuwa wamemkamata.
Hata hivyo hawakumuona na wala hawakumkata, yawezekana kwa umahiri mkubwa aliwaponyoka.