Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 2,021
- 5,313
Wakuu,
Nimeangalia tangazo la Tone Tone kwakweli nimebubujikwa machozi ya huzuni! Mmefikaje huku? Mlikuwa mnaenda vizuri lakini mnaanza kuharibu!
Sawa mlitaka kuja na idea tofauti, iwe catchy ndio mkaona iwe kwenye mfumo wa mwanamke kutaka kuelolewa? Wanawake hawa hawa ambao kila leo wanapigwa vita kuhusu 'kupenda pesa' mkaona itafaa kabisa mkiweka idea ya mwanamke kuchorwa kwenye picha hiyo, sababu jamaa hayupo Tone Tone akamtolea macho mwenye Tone, baada ya aliyetaka kumuoa kuwa na Tone ndio akakubali! Sababu anajua jamaa mfuko uko vizuri? Au sababu atakuwa anacontrol ana access ya miala ataweza kumchotea kiasi?
Ukija kuangalia scene yenyewe, mtu anayeweza kufanya sherehe ya engagement kama hiyo na kualika watu kama akina Mwabukusi na wakufanana naye lazima awe na pesa. Hii inasend ujumbe kuwa Tone Tone ni ya watu wenye hadhi fulani, tayari mmeshatenga aina fulani ya watu.
Mazingira ya video hiyo; kuna setting ya maua imefanyika kwenye, viti na meza, magari ya kukodi, chakula na mapambo mengine. Kama umefanya kazi sehemu za settings na kama props na make up artist utaelewa hela ndefu iliyotumika hapo, unless tangazo liwe limefadhiliwa na mdau ambalo pia haikuwa na haja.
Ajenda ya Tone Tone ilikuwa kuwahamasisha watu kuchagia hata buku ili haba na haba ijaze kibaba. Tangazo hili linaonesha jinsi mmetumia pesa vibaya huku mkijua mna hali mbaya kwenye mfuko, na michango ndio salama yenu. Mtu akiangalia hivi anaona kabisa hela yangu imeenda kuchezewa.
Concept yenyewe, ilibidi tangazo liwe rahisi mtu akione direct anajua hii ni kwaajili ya kuwachangia CHADEMA. Ile rangi ya chama kwenye gari haitoshi kueleza kama tangazo linahusu Tone ya CHADEMA, ukiondoa hizo tisheti hakuna chochote kinachoeleza ni tanzango la CHADEMA. Na hii ni kampeni ambayo mnataraijia watanzania na hata wa nje ambao sio wanachama wawasapoti!
Yaani kiufupi mmefeli, mjadala sasa hivi ni kuhusu concept ya ndoa, settings na mengine lakini sio kuchagia. Hiyo noise ilitakuwa iwe kwenye account, hiyo kelele ibidi iwe kwenye watu kuhamasishana matokeo yake mmetoa content ya watu kutumia kuchambia.
Mnaongelea kuhusu hali ngumu ya maisha ya watanzania kila siku, na nyinyi kuwa kama mkombozi wa watanzania, hilo halionekani kabisa kwenye tangazo lenu, yaani hata that concept ya kuchagia kidogo kidogo haipo!
Mngetafuta watu wa kuwatengenezea concept nzuri, kuna wataalamu wa script wamejaa, mgewatumia kufanya tangazo hilo liguse watanzania wote lakini pia liguse lengo lenu kuu kwenye kampeni hiyo ya Tone Tone.
Bado hamjachelewa mnaweza kufanya bora zaidi. Anyhu, mkija na mapovu poa tu, ila hapa mnatakiwa kufikiria upya.