Kuelekea 2025 XSPaces nayo imepigwa pini, hakikisha una VPN kwenye kifaa chako yasije kutokea ya 2020 ukiwa hujajiandaa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,292
3,593
Wakuu,

Ya Clubhouse yanazidi kujitokeza kadri tunavyoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2025, ClubHouse ilipigwa pini toka 2023 nadhani (kama sijakosea), Telegram ikafata mkondo huo, na yenyewe ni mara chache sana utaipata bila VPN.

Sasa ni XSPaces, huwezi kuhudhuria space sasa hivi mpaka utumie VPN! Serikali mnatuangusha sana wananchi, na hili linaonesha jinsi tulivyokuwa na mabogus kwenye nafasi muhimu.

Mngekuwa na utendaji mzuri mngefikiria kuanza kufungia mitandao? Tena mngekuwa mstari wa mbele kuhimiza watu kutumia digitali.

Sijui maendeleo ya digitali mnayojifanya mnapromote kila siku ni yapi!

Anyhu, hakikisha hukosi VPN kwenye simu/laptop yako, kuna wasiwasi ya 2020 yakatokea tena, sio tu kwamba utashindwa fuatalia matukio yanayotokea nchini bali hata mishe zako zitashindwa kufanyika.

Moja ya VPN Bora ni hii 1.1.1.1, changamka, usijekusema hukustuliwa mapema.

Pia soma: Telegram inafanya kazi kwenu ndugu zanguni?
 
Serikali inaogopa maoni tofauti na yao. Inaweza kufikia kama mazingira ya Rwanda bila hata maendeleo kama yao.
 
CCM na TCRA inashindana na nini hasa? Teknolojia inaendelea kwa kasi isiyozuilika, na badala ya kufikiria namna ya kutumia teknolojia kwa manufaa ya jamii, mamlaka inaonekana kukumbatia vizuizi.

Ni hofu ya uhuru wa maoni, au ni mapambano dhidi ya nini?
 
Back
Top Bottom