Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,590
- 13,273
RAIA wa China, Xie Xiamao maarufu Celine, amehukumiwa kulipa faini sh. milioni mbili au kwenda jela miaka mitano , baada ya kutiwa hatiani kwa shtaka la kufanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni bila kuwa na kibali.
Hukumu hiyo imetolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Hakimu Mkazi Mkuu, Rahim Mushi, baada ya mshitakiwa huyo kusomewa shtaka hilo kisha kukiri kosa.
," Mshitakiwa ninamtia hatiani kama alivyoshitakiwa na amekiri mwenyewe kwani hajaisumbua Mahakama kutokana na kukiri kwake.
Aliongeza," hivyo adhabu yake ni kulipa faini sh. milioni mbili na akishindwa atatumikia kifungo cha miaka mitano jela , fedha alizokamatwa nazo zitaifishwa ziwe mali ya Serikali," alisema.
Hata hivyo, mshitakiwa alifanikiwa kulipa faini ya sh. milioni mbili na kuepuka adhabu ya kwenda jela miaka mitano.
Kabla ya kupewa adhabu hiyo Wakili wa utetezi Mrisho Mrisho aliiomba Mahakama impunguzie adhabu mshtakiwa kwasababu ni mkosaji wa mara ya kwanza.
Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi Christine Joas alimsomea mshitakiwa shtaka linalomkabili.
Mshitakiwa alitenda kosa hilo kati ya Januari na Mei 16, mwaka huu eneo la Supermarket ya Peninsula iliyoko Oysterbay Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Raia huyo alifanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni bila kuwa na leseni kutoka Benki Kuu ya Tanzania( BoT), ambapo alikutwa na sh milioni 16,797,000, USD 64,255 na fedha za China 500.