Reuben Challe
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 2,865
- 5,376
Mwaka huu zimetoka simu nyingi sana ila Mchina kanifurahisha zaidi.
Kampuni ya Xiaomi imetoa flagship zao mpya October mwaka huu ambazo ni Xiaomi 14 na Xiaomi 14 Pro.
Nadhani zinastahili kuwa flagship bora zaidi kwa mwaka huu.
Xiaomi 14 Pro imefikia level ambayo inaweza kushindanishwa na iPhone 15 Pro Max na kuizidi Samsung Galaxy S23 Ultra.
Xiaomi 14 Pro inakuja na Qualcomm Snapdragon 8 Gen 3, na inafikia hadi 16GB RAM 1TB ROM, Inakuja na 1440p display, kamera ya mbele sasa inaweza kurekodi video za 4K@60fps na pia inakuja na USB Type C 3.2
Kitu kingine chema ni kwamba Xiaomi 14 na 14 Pro sasahivi hazijaja na software ya MIUI, Sasahivi ziatumia software mpya ya Xiaomi inayoitwa "Xiaomi HyperOS"
Xiaomi HyperOS inafanana na MIUI kimwonekano ila wamebadilisha mwonekano kidogo sana. Xiaomi HyperOS iko more optimised kushinda MIUI 14 na imekuwa very stable kuliko MIUI ilivyokuwa hapo awali mpaka baadhi ya phone reviewers wameshangaa
Kwenye upande wa kamera Xiaomi anaendelea kushirikiana na Mjerumani "LEICA" na kamera ya Xiaomi 14 Pro imekuwa very improved, kama ulifuatilia vizuri kamera ya nyuma ya Xiaomi 13 Ultra ilikuwa ni nzuri kushinda iPhone 14 Pro Max. Sasahivi kamera ya nyuma ya Xiaomi 14 Pro iko vizuri kiasi cha kushindana na iPhone 15 Pro Max
Kwa sasa hii simu ipo official kwa China tu ila Global version inaweza kuachiwa February 2024. Nadhani na Samsung Galaxy S24 Ultra itaachiwa kipindi hichohicho
Nchini China, Xiaomi 14 na 14 Pro zilipoachiwa tu, waliuza takribani simu milioni 1.45 (Xiaomi 14 series) ndani ya siku 10 tu na kufanya Xiaomi 14 series kuongoza kwa mauzo nchini China katika wiki ya 44 ya mauzo ya simu huku Huawei na Honor ndio wanafuatia.
Xiaomi 14 Pro version ya 16GB RAM 1TB ROM imetengenezwa na titanium kwa nje kama tu iPhone 15 Pro Max. Mfano angalia hii picha, hiyo ya kushoto ni Xiaomi 14 Pro (titanium) na kulia ni iPhone 15 Pro Max. Zote ni titanium
Kadri siku zinavyoenda Mchina anazidi kuionesha dunia kuwa na yeye anaweza