Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 710
- 1,858
Unaambiwa, vigogo wa soka la Morocco, Wydad Casablanca, hawajakata tamaa. Wakifukuzia saini ya mshambuliaji wa Taifa Stars na Yanga SC, Clement Mzize. Hii ni baada ya klabu yake kuweka wazi kuwa hajupo sokoni. Lakini Wydad hawajali, hawasikii wala hawaogopi—wanaendelea kushindilia mlango ambao unaonekana kufungwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya, Micky mwandishi wa Ghana, amefichua kuwa ofa ya hivi karibuni ya Wydad ni kama wameamua kurudi tena, wakiwa na begi zima la fedha ofa ikifikia—USD 500,000, sawa na takriban Tsh. bilioni 1.4, na masharti maalum ya kuongeza USD 300,000 (Tsh. milioni 815.4) zaidi endapo Mzize atatimiza malengo fulani, kama kushinda tuzo ya mfungaji bora na kuchangia ushindi wa mataji ya ligi na Kombe la Dunia la Vilabu.
Ni kama mchezo wa bahati nasibu—kila mmoja anasubiri kuona kama Yanga watasalimu amri au kama Wydad watavunja ngome hiyo ya Yanga.
Klabu hiyo yenye mamilioni ya mashabiki maarufu "Ultras Winners", wamekuwa wakikatiza kwenye page ya instagram ya Mzize na kumkaribisha kwenye klabu yao.
Je, Yanga wataruhusu ajiunge na Wydad AC?
Soma zaidi:
• Clement Mzize huyu hapa kwenye rada ya Wydad Casablanca ✅
• Yanga imekataa ofa ya pili ya klabu ya Wydad ya Tsh Bilioni 1.7