Mkuu, angalia usimamizi wa hifadhi za taifa ulivyo.
TANAPA wanahusika na National Parks tu na huko hali naweza kusema ni nzuri au si mbaya.
Idara ya Wanyama Pori (Wildlife Department) inasimamia Game Reserves (kama Selous nk) na Game Controlled Areas. Hizo sehemu mbili ndiyo kwenye matatizo makubwa ya ujangili.
Kuna wakati kulikuwa na pendekezo la kuwa na kitu kimoja tu kama Tanzania Wildlife Services kama ilivyo Kenya lakini nahisi haiwezi kuwa ufumbuzi pia maana Kenya wana ujangili kama sisi tu.
Ndiyo maana nikasema irudishwe operation Uhai kama ile ya miaka ya sabini na isimamiwe na JWTZ angalu miaka mitano tu. Nina uhakika katika kipindi hicho, tembo wataongezeka sana.