Makao Makuu
Member
- Aug 28, 2016
- 7
- 4
Agizo la Rais Magufuli la serikali kuhamia Dodoma linaonekana kupata msukumo mkubwa hata kwa wananchi.
Wengi wanaamini serikali ikihamia Dodoma kunaweza kupatikana msukumo wa maendeleo kwa maeneo mengi ya Tanzania hasa mikoa ambayo iko mbali na Dar es Salaam kama Rukwa, Ruvuma, Mbeya, Kigoma, Katavi, Kagera na mingineyo, kwani walau Dodoma ni katikati ya nchi.
Hebu soma utafiti huu hapa:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 28/08/2016
TANGAZO LA RAIS DK. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI LA KUHAMIA DODOMA KABLA YA KUMALIZA MUDA WAKE LAUNGWA MKONO NA WENGI
CZI ambayo ni taasisi huru isiyo ya kiserikali inayojihusisha na ushauri wa mambo ya habari, utafiti na jamii, ilizunguka mikoa 18 na kuuliza wananchi maswali ya papo kwa papo, kwa njia ya simu ama kwa kuhoji kimakundi kulingana na umri wa wahusika kuhusu tamko la Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli la kuhakikisha serikali inahamia Dodoma kabla hajamaliza muhula wake.
Tulihoji wananchi wa kada na umri mbalimbali kwa kuweka kwenye makundi matatu - umri wa miaka 14 – 18; umri wa miaka 18 – 30; na kuanzia miaka 30 hadi 60.
KUNDI LA I: MIAKA 14-18
Kundi hili baada ya kuhojiwa wanaamini rais John Magufuli atafanya mabadiliko ya kweli na kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi katika mikoa mbalimbali nchini na kwa kiasi kikubwa amerejesha nidhamu kwa walimu, madaktari na watumishi wengine wa umma.
Asilimia 89% ya vijana hao kwenye ngazi ya elimu ya msingi na sekondari wanaamini na wanaunga mkono agizo la Mhe. Rais John Magufuli la kuhamia Dodoma na wao wangependelea kuona anatimiza malengo hayo kwa haraka zaidi.
Sababu walizozitoa ni kwamba, serikali itakapohamia Dodoma mikoa ambayo ilisahaulika kimaendeleo itaendelea kwa kasi kama Kigoma, Tabora, Singida, Rukwa, Katavi, Lindi na Mtwara pamoja na Dodoma yenyewe kwa kuwa huduma za maendeleo zitapatikana kirahisi kuliko ilivyokuwa kwa Dar es Salaam.
Aidha, wanaamini Rais Dk. John Magufuli atasaidia kuleta mageuzi kwenye elimu kwa kumaliza kero ya madawati, mitaala, madai ya walimu nchini pamoja na kuboresha taaluma kwenye mikoa hiyo ambayo iko nyuma kielimu pamoja na mikoa mingine Tanzania Bara na Zanzibar. Hata hivyo, asilimia 11% ya waliohojiwa kwenye kundi hilo wana mashaka makubwa kwamba huenda Mhe. Magufuli asifanikiwe kwenye harakati zake za kuhamia Dodoma na hata kushindwa kuleta mageuzi kwenye sekta ya elimu kwenye mikoa hiyo ya pembezoni.
KUNDI LA II: MIAKA 18-30.
Watanzania kuanzia miaka 18-30, asilimia 79% wanaamini serikali ya Rais John Magufuli itatimiza lengo la kuhamia Dodoma kwa kasi kubwa na pia wanaunga mkono uhamishaji wa Serikali kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Kada hiyo inaamini pia kuwa Rais Magufuli ataondoa kero ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na kumaliza tatizo la mabweni ya kulala wanafunzi wa vyuo vikuu kwa baadhi ya mikoa ambayo haina kabisa miundombinu hiyo, na kupunguza tatizo la ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu pamoja na vijana nchini Tanzania.
Sababu kubwa ambayo imewafanya waseme hayo ni kutokana na dhamira ya dhati ambayo rais ameonyesha katika kusimamia kauli zake mwenyewe kwa vitendo tofauti na awamu zingine ambazo zilishindwa kutekeleza na kusimamia kauli zao kama wakuu wa nchi.
Tumeshuhudia katika uteuzi wa viongozi wa serikali ya Awamu ya 5, Mh. Rais amezuia shamra shamra za kupongezana viongozi wa serikali wanapoteuliwa na kufanya uteuzi wa serikali ya awamu ya tano kutumia bajeti ndogo katika siku hizo za uteuzi. Mfano, uteuzi wa Wakuu wa Wilaya, Mawaziri na Wakuu wa Mikoa hakukuwa na shamra shamra kama ilivyozoeleka katika awamu zilizopita.
Hili limesaidia kuokoa fedha nyingi ambazo zimekwenda kufanya shughuli za maendeleo ya wananchi. Wale waliodhani kwamba utendaji wa Dk. Magufuli ni mfumo wa kujilundikia majukumu bila utekelezaji (Slack Management Style) walikosea sana, kwa sababu tangu wakati ule tumeshuhudia watendaji wengi wazembe, wala rushwa na mafisadi wakiwajibishwa huku wengine wakifikishwa mahakamani.
Aidha, asilimia 21% ya kada hii haiamini kama serikali ya awamu ya tano itatimiza lengo la kuhamia Dodoma wakisema ni kawaida ya serikali inapoingia madarakani huja na mbwembwe na ahadi nyingi ambazo mwishowe hushindwa kukamilisha malengo yao.
KUNDI LA III: MIAKA 30-60
Asilimia 88% ya Watanzania wenye umri wa miaka 30-60 waliohojiwa katika mikoa hiyo 18 ambayo CZS ilitembelea wanaamini serikali hii ya awamu ya tano itatimiza malengo yote ya kuhamia Dodoma kwa kuwa imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha ile mipango iliyojiwekea inatekelezeka kwa haraka. Wanaunga mkono serikali kuhamia Dodoma kwa kuwa itarahisisha mikoa mingine kupata maendeleo kwa haraka na huduma za kijamii zitaimarika kwa wananchi hususan wa kada ya chini.
Wanaeleza kwamba, suala la kuhamia Dodoma lilikuwa linahitaji utekelezaji na uthubutu kwa sababu lipo kisheria kwa takriban miaka 43 sasa wala siyo la kutungwa na Rais Magufuli. Wanapongeza uamuzi huo na kusema utaokoa fedha za umma kwa sababu mawaziri na watendaji wengi wa serikali hutumia takriban siku 185 kuwepo Dodoma kuhudhuria vikao 182 vya Bunge ambavyo hufanyika kila mwaka. Wanapokuwepo Dodoma hulipwa posho na masurufu mengine, lakini kama watendaji hao wangekuwa wanaishi Dodoma gharama zisingekuwa kubwa kwa watumishi hao ambao wengi huenda huko kusaidia masuala mbalimbali yanayohusiana na wizara ama idara za serikali.
Kada hii pia wanasema watumishi wa umma wamerejesha imani kwa serikali kutokana na juhudi za Mhe. Rais anavyopambana na ufisadi na rushwa kwa dhati.
Aidha kada hii wanaamini mhe rais Magufuli atasaidia wazee kupata stahiki zao kwa kuwa zikiwemo kuwalipa posho kwa mwezi kwa wale wenye umri wa kulipwa.
Wanaamini nidhamu itaongezeka miongoni mwa watumishi wa umma pamoja na binafsi kutokana na namna serikali inavyopambana na watumishi hewa na utumbuaji majipu unaoendelea kwenye serikali ya awamu ya tano.
Aidha, kada hii inaamini kuwa Serikali itakapohamia Dodoma, Tanzania itaendelea kuwa na umoja na mshikamano na Muungano utazidi kuimarika bila wasiwasi wowote.
Vilevile kada hii inasema Rais Magufuli anazidi kuwa maarufu ndani na nje ya nchi kwa kuwa ameonyesha mfano kwa viongozi wengine wa Afrika kupambana na rushwa waziwazi lakini pia wanasema wapinzani wanapaswa kubadili mbinu za kupambana na serikali kama wanataka kufikia malengo ya kushika dola.
Asilimia 12% ya kada hii ina mashaka kwamba uamuzi wa serikali kuhamia Dodoma utafanikiwa kwa maelezo kwamba suala hilo limekuwa mtaji wa kisiasa wa watawala wengie.
Pia ndani ya asilimia hizo wanasema kwamba serikali haitaleta mageuzi yoyote kwa wazee na nidhamu kwa watumishi wa umma kamwe haitabadilika kutokana na aina ya viongozi wanaowasimamia watumishi hao ambao wengi wao siyo waadilifu na siyo watendaji na wafuatiliaji wa mambo kwenye maeneo ya kazi nchini.
Kwa ujumla wake baada ya kufanya utafiti huo asilimia 85.3% ya Watanzania wote wanaunga mkono serikali ya awamu ya tano kuhamia Dodoma na 14.7% hawaungi mkono serikali kuhamia Dodoma na wanaamini serikali haitahamia Dodoma.
Mwenye nia njema na maendeleo ya taifa hili, anapaswa kuiunga mkono kwa dhati kabisa serikali ya Dk. Magufuli kuhamia Dodoma ili kuimarisha uchumi wa wananchi kwa utendaji huu na siyo kumhujumu, kumbeza ama kutoka visingizio vyovyote vile.
Imewasilishwa na :
Juma George Chikawe
Daniel Mahelela
Chikaka Nyamagambile
Dotto Nyirenda