Mowwo
JF-Expert Member
- Aug 15, 2015
- 1,011
- 1,529
Wakuu, umeibuka wizi ambao ningependa kuwasilisha ili mamlaka husika ichukue hatua stahiki na kulinda heshima ya Jeshi la Polisi.
Jana, tarehe 4/2/2025, majira ya saa 1 jioni, majirani zangu wawili walikuwa maeneo ya Njiro, Kata ya Lemara, mtaa wa Korongoni wakitembea kuelekea barabara ya East Africa.
Ghafla, pikipiki tano ziliwazunguka, na waliokuwa kwenye pikipiki hizo walijitambulisha kama askari (bila kueleza wanatoka kituo gani). Walipowapiga pingu, waliwauliza maswali kama: "Hamvuti bangi? Hamtumii mirungi? Mnafanya kazi wapi?" Wote walijibu kwa kusema hapana.
Baada ya hapo, waliwalazimisha kupanda pikipiki mbili huku wamefungwa pingu. Pikipiki tatu zilizobaki ziliondoka, na mmoja wa wale waliobaki akawanyang’anya simu zao.
Wakiwa kwenye pikipiki, waliwaambia kila mmoja atoe shilingi laki moja ili waachiwe huru.
Waliposema hawana pesa hiyo, waliwatukana na kuondoka nao kuelekea Muriet. Walipopita Sheli ya Simba (East Africa), walikunja kulia kuelekea mafichoni, wakasimamisha pikipiki zao na kuwapigia simu wenzao waliokuwa na zile simu walizochukua awali.
Simu hizo zilirudishwa pale mafichoni, na wakawataka watoe pesa taslimu walizokuwa nazo. Washkaji hao walitoa jumla ya shilingi 26,000, baada ya hapo wakatukanwa na kuambiwa waondoke na wasigeuke nyuma.
Maswali ya kujiuliza:

- Kama walikuwa ni wezi, kwanini wasiondoke na simu zao ambazo zilikuwa za thamani?
- Kama ni polisi, walitumia sheria gani kuwanyang’anya pesa taslimu?
- Kwanini hawakujitambulisha kwa uwazi na kusema wanatoka kituo gani?
- Je, kama ni polisi, wanapewa target ya makusanyo wakiwa doria?