Wizara ya Kilimo,Mifugo na uvuvi imeahidi kuichukua changamoto ya Magadi Chumvi kwenye mashamba ya mpunga kuwa tatizo la kitaifa linalotakiwa kuingizwa kwenye mipango na sera za kitaifa na kupatiwa ufumbuzi wa haraka ili kilimo cha Mpunga kiendelee kuwa na mchango kwa uchumi na maendeleo ya taifa.