Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,715
- 4,453
Wakuu,
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema kufuatia taarifa ya Serikali kuhusu agizo la baadhi ya Watumishi wa Umma kufanyia kazi nyumbani, Wizara hiyo inaelekeza Shule zote za Msingi, Sekondari na Vyuo katika Mkoa wa Dar es Salaam kufungwa kwa siku mbili January 27 na January 28, 2025.
Taarifa iliyotolewa leo January 26,2025 na Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa imesema “Tangazo hili ni kwa Vyuo na Shule za Serikali na Binafsi, Wadau wote wa elimu wanaombwa kuzingatia tangazo hili ili kuepusha changamoto za usafiri zinazoweza kujitokeza kutokana na kufungwa kwa baadhi ya barabara, masomo yataendelea kama kawaida kuanzia January 29, 2025”
Soma pia: Serikali tangazeni tar 27 na 28 kuwa siku za mapumziko kwa wote na wanafunzi wakae nyumbani kuondoa kabisa huo 'usumbufu' mnaosema
Hatua hii inakuja ili kuepusha usumbufu utakaosababishwa na kufungwa kwa barabara kutokana na ugeni mkubwa wa Watu wanaokuja kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Kuhusu Nishati utakaofanyika Jijini Dar es salaam kesho na keshokutwa.