Wizara ya Afya yathibitisha uwepo wa wagonjwa wawili wa Mpox nchini

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,986
5,122
Wakuu,

Ila kwenye ile video jamaa alisema wapo wengi hapo hospitali, serikali inasema watu 2!🤔🤔

Pia soma: Huu ni ugonjwa gani? Wizara ya Afya semeni kitu

=====

Screenshot_20250310_184540_Instagram.jpg

Screenshot_20250310_185136_Instagram.jpg


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UGONJWA WA MPOX NCHINI​

Tarehe: 10 Machi, 2025, DODOMA

Mnamo tarehe 7 Machi, 2025 Wizara ya Afya kupitia mifumo yake ya ukusanyaji wa taarifa na ufuatiliaji wa magonjwa ilipokea taarifa za uwepo wa wahisiwa wenye dalili za vipele usoni, mikononi, miguuni na sehemu nyingine za mwili. Dalili hizi ziliambatana na homa, maumivu ya kichwa, vidonda kooni, maumivu ya viungo vya mwili ikiwemo misuli na mgongo. Kati ya wahisiwa hao mmoja ni dereva wa magari ya mizigo aliyetoka nchi jirani kwenda Dar es Salaam.

Baada ya kupokea taarifa za wahisiwa, sampuli zilichukuliwa na kupelekwa maabara ya Taifa kwa uchunguzi. Mnamo tarehe 9 Machi, 2025 uchunguzi wa kimaabara umethibitisha kuwa wahisiwa wawili (2) wana maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Mpox. Hivyo, hadi kufikia sasa jumla ya wahisiwa wawili (2) wamethibitika kuwa na ugonjwa wa Mpox nchini.

Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na vituo vyote vya kutolea huduma za Afya, inaendelea na ufuatiliaji, uchunguzi na utambuzi kubaini kama kuna wahisiwa wengine ili waweze kupatiwa huduma stahiki.

Chanzo cha ugonjwa huu ni wanyama jamii ya nyani, ambapo binadamu huweza kuupata kutokana na shughuli zinazoweza kusababisha kugusana na wanyama, majimaji au nyama za wanyama wenye maambukizi. Aidha, endapo binadamu akipata maambukizi hayo anaweza kumwambukiza mtu mwingine kwa kugusana moja kwa moja.

Kwa taarifa hii, Wizara ya Afya, inawahakikishia wananchi kuwa Serikali imejipanga kudhibiti ugonjwa huu na hasa kutokana na uzoefu tulionao wa kudhibiti magonjwa ya mlipuko. Serikali inaendelea kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa katika ngazi zote, upimaji wa watu wanaoingia na kutoka kupitia mipaka ya nchi, kuimarisha utoaji wa elimu ya afya na kuhamasisha jamii ili kuwawezesha wananchi kuchuka hatua za kujikinga.

Kwa kuzingatia kuwa magonjwa mengi yanayosababishwa na virusi hayana tiba mahususi ila mgonjwa anahudumiwa kulingana na dalili alizonazo. Hivyo Wizara inawasihi na kuwasisitiza wananchi wote kuzingatia na kutekeleza afua za kujikinga kama ifuatavyo:

1741622510858.jpeg

i. Kuwahi katika kituo cha huduma za afya kwa uchunguzi na matibabu unapoona mojawapo ya dalili za ugonjwa wa Mpox au piga simu nambari 199 bila malipo;

ii. Kuepuka kuchangia vitu kama nguo na matandiko ambavyo vimetumiwa na mtu mwenye dalili za Mpox;

Kuepuka kugusana kwa kupeana mikono, kubusiana, kukumbatiana au kujamiiana na mtu mwenye dalili za Mpox;

iv. Kuepuka kugusa majimaji ya mwili ya mtu mwenye dalili za Mpox.

V. Kuepuka kumuhudumia mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa wa Mpox bila kuchukua taharadhari;

vi. Watumishi wa afya kuzingatia kanuni za kujikinga na magonjwa wakati wote wanapowahudumia wagonjwa ikiwemo wenye dalili za vipele na homa;

vii. Kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono.

Wizara ya Afya, itaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa ugonjwa huu, kadri taarifa za ufuatiliaji na uchunguzi zitakavyopatikana. Wizara inashauri wananchi kuendelea na shughuli za kila siku kwa kuzingatia tahadhari za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu.

Vilevile, Wizara inapenda kuwapa taarifa kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa Marburg, ikumbukwe kwamba, mnamo tarehe 20 Januari 2025, Serikali ilihabarisha umma hukusu kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Marburg. Mwenendo wa udhibiti wa ugonjwa huu unaendelea vizuri na hadi kufikia leo tarehe 10 Machi 2025, zimetimia siku 41 bila kuwa na mgonjwa mpya.

Imetolewa na:

Jenista J. Mhagama (Mb). WAZIRI WA AFYA​
 
Sijui na sina hakika ya idadi ya wagonjwa lakini nakukumbusha, katika nyakati hizi uongo ni utamaduni mpya kwa watanzania.
Yaani wamemwacha Mungu wanayemfahamu tokea utotoni wanamwamini Uchumi,
Ndio maana naanzq kuamini kuwa Dini zimefika kwenye Kona ya juu mwishoni,↗️↘️
 
TOKA MAKTABA :
15 January 2025


Siyo mpox hiyo ?

1741858067521.jpeg


Mpox husambazwaje?
Mpox inaweza kusambazwa kuanzia wakati dalili zinaanza hadi vipele vipone kabisa na tabaka jipya la ngozi
lifanyizwe. Kirusi hicho kinaweza kusambazwa kutoka mtu hadi mtu kupitia mgusano wa karibu, mara nyingi
wa ngozi kwa ngozi, ikiwemo:
• Mgusano wa moja kwa moja na vipele vya mpox, makovu, au umajimaji fulani wa mwili kama vile mate,
au kamasi
• Mahusiano ya karibu kama vile ngono, kubusu au kukumbatiana
• Kugusa vitu (vikombe, sahani), nguo (mavazi, malazi, au taulo), na sehemu ambazo zimetumiwa na mtu aliye
na mpox lakini ambazo hazijasafishwa bado.
• Watu wajawazito walio na mpox wanaweza kusambaza kirusi hicho kwa fetasi wakati wa ujauzito au kwa
vitoto vichanga wakati wa ujauzito au baada ya kuzaliwa
Mpox HAISAMBAZWI kupitia mgusano wa kijuujuu kama vile unapokuwa
na watu ukifanya kazi ofisini, kwenda sokoni, au unapokuwa kwenye basi.
Unaweza kujilindaje?
• Epuka mgusano wa karibu, wa ngozi kwa ngozi na watu walio na vipele vinavyoonekana kama mpox.
• Usimbusu, kumkumbatia au kufanya ngono na mtu aliye na mpox.
• Epuka kugusa vitu na vifaa ambavyo mtu aliye na mpox ametumia, kama vile vyombo, malazi, au mavazi.
• Nawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji au utumie kitakasa mikono kilicho na alkoholi.
Nikigusana na mpox, nifanye nini?
• Angalia dalili kwa siku 21 kuanzia mara ya mwisho ulipogusana
na mpox. Unaweza kuendelea kufanya shughuli zako za kawaida
za kila siku maadamu huna dalili au ishara za mpox.
• Ikiwa una vipele vipya au ambavyo huvielewi au dalili nyingine
za mpox,mwone daktari na upimwe mpox.
• Iwapo utaambukizwa mpox, kaa mbali na watu wengine kadiri
iwezekanavyo, funika vidonda vyako, na uvae barakoa unapokuwa
karibu na watu wengine hadi vipele vyako vitoweke kabisa,
Ni nani anayeweza kuugua vibaya?
Mpox inaweza kuwa hatari sana kwa watu fulani, kama vile:
• Watu ambao mfumo wao wa kingamaradhi ni dhaifu sana au walio na VVU (HIV) ambayo haijadhibitiwa
• Watoto wenye umri chini ya mwaka 1
• Watu walio na historia ya ugonjwa wa ukurutu (kizema)
• Watu ambao ni wajawazito
Iwapo wataugua mpox, huenda wakahitaji utunzaji wa ziada ili kuwasaidia kupata

Source : cdc.gov
 
Siyo mpox hiyo ?
15 January 2025
Zaidi ya wakazi 200 wa Mtaa wa Yombo Dovya, wilayani Temeke mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania wameathirika kwa kubabuka ngozi katika maeneo mbalimbali mwilini baada ya kudaiwa kutumia mafuta ya kula yenye sumu.Mafuta hayo inasemekana yamenunuliwa katika duka la mfanyabiashara anayefahamika kwa jina la Kamau maarufu kama Mangi.


View: https://m.youtube.com/watch?v=iaA2-FkNCkw
 
Back
Top Bottom