ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 60,387
- 71,038
Inashangaza kusikia kwamba Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akitumia Jina la Rais Samia kutaka kuhalalisha ulaji wa pesa zaidi ya Shilingi Bilioni 625 za Ufadhili/Mkopo kutoka World Bank Kwa kuanzisha programu hewa eti ya Madaktari Bingwa Kwenda Kuwajengea uwezo Watumishi Vituo vya Afya waongeze Utendaji wao Kuwahudumia Wananchi.
Kiufupi hizo Bilioni 625 zitaliwa Kwa njia ya posho,training allowances na blaa blaa zingine zisizo na msingi.
Watu wenye dhamana jitahidini kuwa na aibu na Huduma Kwa Wananchi.Kama Rais anamfundisha Madaktari Bingwa Kwa Ufadhili wa ndani na Nje ya Nchi,Kama Serikali inawapa mikopo Wanafunzi kwenye fani za kipaombele za Afya Ili wapate mfunzo Bora ,hii ya Programu uchwara inatokea wapi kama sio wizi?
Hospitali na Vituo vya Afya vinalia Shida kubwa ya vifaa tiba,vitenganishi, madawa na Wataalamu harafu nyie mnakuja na mradi wa kipigaji.
On top of that Nchi hii Ina upungufu mkubwa wa Vituo vya kutokea Huduma kuanzia Mahospitali Hadi Vituo vya Afya na Zahanati kiasi Watu wanatembea umbali mrefu Kufuatia Huduma hususani akina mama na Watoto matokeo yake ni vifo vya uzazi na Watoto kuwa wvingi.Badala ya kujenga miundombinu ya Huduma za Afya jirani na Wananchi na kuviwekea vifaa stahiki nyie mnakuja na mradi wa wizi.
Pesa hizo zinatosha Kujenga Vituo vya Afya Zaidi ya 700 Nchi nzima na kufunga vifaa tiba vyote.Zinatosha kujenga hospitali zaidi ya 60 Nchi nzima zikiwa full na vifaa vyake.
Wizi kama huu ulipitishwa Kwa lazima Bungeni na Serikali kwenye Wizara ya Ardhi ambapo zaidi ya Bilioni 60 ziliwekwa kwenye fungi la posho badala ya kwenda kupima Ardhi nazo zilikuwa ni pesa za Mkopo kutoka WB.
View: https://www.instagram.com/p/C1MBcmnKsI5/?igsh=NmJiYWZiY2E0Mg==
My Take
Namuimba Mh.Rais asiruhusu wizi huu kufanyika na pia Bunge la JMT lizuie Bajeti ya Wizara ya Afya endapo watakuja na proposal hii ya upigaji.
Wabunge msikubali kuburuzwa kama ilivyotokea Wizara ya Ardhi maana ni Mkopo huo tutakuja kulipa ila wachache watakuwa wamekula.