Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 423
- 1,044
Ukisikia wasomi wa Afrika kushindwa kutumia maarifa kutatua changamoto zinazoikabili jamii, hili la NHIF, wizara ya afya na wamiliki wa vituo binafsi ni mfano tosha wa kufeli kwa wasomi wetu
NHIF iliwahi kulalamikiwa na waziri mwenye dhamana ya afya kwa ubadhilifu wa michango ya wanachama. Kwamba wafanyakazi wa NHIF wanajikopesha sehemu kubwa ya michango bila kufanya marejesho
NHIF waliwahi kulalamika hadharani kuwa vituo vya afya vya binafsi vinazidishi gharama sana zaidi ya gharama halisi alizohudumiwa mgonjwa
Pia NHIF hao hao wakalalamikia wanachama wao kuwa kadi moja inaweza kutumika na zaidi ya mgonjwa mmoja
Hoja ya wafanyakazi wa NHIF kujikopesha kiasi kikubwa cha michango pasipo kufanya marejesho haijawahi kujibiwa wala kuchukuliwa hatua
Hoja ya vituo binafsi kuzidisha gharama zaidi ya ile aliyohudumiwa mgonjwa hili liko wazi kwa baadhi ya vituo. Hatua hazijawahi kuchukuliwa kwa vituo hivyo
Mabishano yanayoendelea kati ya serikali na wamiliki binafsi ni matokeo ya mfuko wa NHIF kuzidiwa nguvu kwa vyote. Hawana mifumo madhubuti ya kudhibiti mapato yao na hawana mifumo madhubuti ya kudhibiti matumizi yao
Kwanini NHIF inakimbilia kupunguza gharama za huduma badala ya kutatu hoja zilizowahi kuibuliwa??
Hoja pekee waliyojaribu kufanyia kazi ni kudhibiti matumizi ya kadi kwa zaidi ya mtu mmoja. Hili limewaongezea gharama za uendeshaji kwasababu wamelazimika kuajiri watu wao watakaofanya kazi hiyo kwenye baadhi ya vituo binafsi hivyo hapa hakuna walichookoa
Vituo binafsi vinapata kiburi cha kuja hadharani na kutishia kuwafukuza wagonjwa wa NHIF waliomahututi baada ya saa48 kwasababu wanajua serikali haina uwezo wa kuhudumia wananchi wake wote vizuri
Kwanini wanapata hiki kiburi? Kauli kama hizi za kuwafukuza wagonjwa wa NHIF unaweza kuitafsiri kama kufanya mauji hadharani huku wakiamini serikali haina cha kuwafanya. Endapo serikali itaruhusu hali hii itokee itakuwa imekiri udhaifu mkubwa sana na huku ni kumchezea simba sharubu
Wanaoifilisi NHIF ni vituo binafsi na wafanyakazi wa NHIF wenyewe halafu vitisho vinakuja kwa wachangiaji.
Je, hii ni kwamba wachangiaji wa NHIF hawana mtetezi? au Mtetezi wa wanachama wa NHIF hana nguvu dhidi ya vituo binafsi vilivyosaini mkataba wa kuhudumia wanachama hawa?
Imefika hatua sasa wananchi tujifunze namna ya kudai haki zetu kwa nguvu.
Hizi sarakasi haziwaumizi vituo binafsi wala NHIF wala serikali, zinawaumiza wanachama wa NHIF. Hivi mchangiaji atakayefariki kwasabau ya sakata hili, NHIF, serikali au hivi vituo binafsi vitaweza kurudisha uhai wake pale watakapokuwa wamemaliza migogoro yao? Watarudisha maisha ya wagonjwa waliowapoteza kwa makusudi? Hivi ndivyo taaluma zao zinavyoeleleza??
Kwa nchi yenye wananchi na serikali inayojitambua, mkurugenzi wa NHIF, mwenyekiti wa Bodi ya wamiliki wa vituo binafsi na waziri wa afya walitakiwa wawe lockup wanatafutia ufumbuzi huko sio kulala usingizi mnono wakati wagonjwa wa NHIF wanasubiri kufukuzwa kutoka vituo binafsi baada ya saa48