Wizara ya Afya imeonesha udhaifu Mkubwa katika ajira zao

2025DG

JF-Expert Member
Jan 30, 2023
520
1,488
Habari.

Mchakato wa ajira zilizotolewa kwa kibali cha Raisi wa Jumhuri ya muugano wa Tanzania.

Majina yaliweza kutolewa siku za hivi karibuni lakini kiukweli kumekuwa na malalamiko makubwa katika majina yaliyotolewa .

Nitaambatanisha Hoja zinazoongelewa zaidi na jamii ambazo hazikukizi Vigezo.

1.Mwaka wa Kuhitimu, Mara nyingi serikali katika hizi ajira uzingatia mwaka wa mtu kuhitimu na kada Adimu lakini hii imeweza kwenda Tofauti katika nafasi ya DAKTARI DARAJA LA PILI wameweza kumchukua mhitimu wa mwaka 2021 kada ya AFISA MUUGUZI MSAIDIZI wameweza kuchukua mhitimu wa mwaka 2022..Kwa upande wa udaktari bwiga inaeleweka uhaba wao lakini kwa upande wa kama mbili hizo zina ushindani mkubwa na watu wengi tu lakini kwanini MOH wameshindwa kufuata utaratibu waliojiwekea.


Kwenye Kigezo cha kuangalia Muda wa mtu kutoajirika muda mrefu kada ya AFISA MUUGUZI MSAIDIZI wizara imeweza kuajiri mhitimu wa mwaka 2007, 2008, 2009 wakati mchakato wao wa ajira siku zote wanasema wanaanzia kuajiri mwaka 2015 ambapo mfumo wa ajira za moja kwa moja uliondolewa.

Kuna Daktari Bigwa Ameajiriwa ikiwa LESENI YAKE YA USAJILI HAIKO ACTIVE.

Kuna HOJA SIO RASMI lakini nitaziweka.

1..Kanda ya kaskazi imeonekana watu wengi wameajiriwa ukiangalia kwenye yale majina MOLLEL,MOSHI, URASSA, MASSAWE imeonekana Mara nyingi kwa kujirudia.

2.DINI ya kiislamu majina yake ni machache Sana.

MAPENDEKEZO.

1. Serikali itumie mfumo wa Usaili katika kuajiri.

2. Idadi iongezeke ya Waajiriwa.

3. Mchakato uwe wa wazi na Haki.
 
Hizo hoja za udini waliokosa Tamisemi pia wangezileta ingekuaje....

Kikubwa amini wakati wako upo na utafanikiwa... Huenda Mungu anapima akili na mienendo yako, hiyo ni bahati yao... Kuwa mtu wa kukubali kuwa umeshindwa kupata nafasi au waliokaribu yako wamekosa, uridhishe moyo huenda ukapata siku moja
 
Kuweka ajira za afya na walimu , zisimamiwe na ajira portal, wamefeli kwa kiwango cha juu sana 🤔🤔🤔