beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,367
Kwa mujibu wa Takwimu za Wizara ya Afya, 94% ya Watanzania wapo katika hatari ya kupata maambukizi ya Ugonjwa wa #Malaria katika kipindi cha mwaka mzima. Hayo yameelezwa na Waziri Ummy Mwalimu katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani
Amesema kwa Mujibu wa takwimu za Mwaka 2021, kati ya kila Wagonjwa 100 waliohudhuria Hospitali/Zahanati/Vituo vya Afya, 10.6 kati yao walihudhuria kwasababu ya Malaria
Ameeleza, "Bado Ugonjwa huu unaweka mzigo mkubwa katika utoaji Huduma za Afya, bado ni chanzo cha vifo vya Watanzania. Mikoa inayoongoza kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ni Kigoma, Kagera, Geita, Mtwara, Lindi na Ruvuma"