Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,828
- 13,585
Wizara hizo zimekutana jijini Dodoma kufuatia taarifa zilizowasilishwa kwa Serikali na Chama cha Wazalishaji Chumvi Tanzania (TASPA) kuhusu changamoto zinazoikabili sekta hiyo ndogo ya chumvi ikiwemo kudorora kwa biashara ya chumvi hapa nchini.
Kikao hicho kilijumuisha Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Jaffo,Waziri Wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Madini Anthony Mavunde pamoja na Wadau wa Chumvi Nchini.
Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa,Wizara ya Madini kupitia STAMICO imewahakikishia wadau juu ya ufungwaji wa kiwanda cha kusindika Chumvi katika Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi kabla ya mwisho wa Mwezi Desemba 2024.