Wadau hope mko fine.
Nimekua nikifuatilia matukio mengi na changamoto tunazokumbana nazo kuwa mara nyingi utokana na tabia za wivu.
* Fulani mambo yake yanaanza kubadilika toka apate kazi yake nzuri , rafiki zake humuonea wivu na kuanza kumchongea kwa boss wake kuwa atakaua anaiibia kampuni.
* Mungu kajalia umepata mchumba ambaye ukipita naye kitaa watu wote wanakonyezana.....
Hata uchumba wenu ujafika mbali , wafitini wanaanza kupitisha figisufigisu ili muachane eti kisa wanakona unafaidi.
* Uko na mpenzi wako kwenye part inayowakutanisha na watu wengi...ila ukionyesha kumcangamkia mtu mwingine wa jinsia tofauti , tayari mpenzi keshavimba na wivu umemjaa.
# Leo nataka mnisaidie hivi wivu husababishwa na nini na ni kwa nini wanadamu wengi hawapendi kuona mtu fulani aki enjoy maisha yake?