Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,415
- 22,026
Natoa wito kwa Watanzania wenzangu wote wenye upendo na kuthamini uhai na haki za binadamu wenzao. Imetokea mara kadhaa kwamba watu wanatekwa, wanapiga kelele kuomba msaada lakini watu wanaangalia tu bila kutoa msaada.
Tafadhali sana, unaposikia mtu anapiga kelele kuomba msaada anatekwa, tunamsihi sana kila mtu, tutumie nguvu ya wingi kutoa msaada na kuzuia utekaji. Wale wenye magari mlio karibu zuieni njia ya gari la watekaji lisiondoke, na ukisha lizuia toka nje ya gari na ulipige loki gari lako.
Kisha waambieni watekaji wasubiri Polisi rasmi wafike kwenye tukio. Tujitahidi kujizuia kutembeza kipigo kwa watekaji, si mnajua ni makosa kuwaua watekaji japo wao wanatuua?
Kumbukeni kwamba tunachukua hatua hizi kwa sababu inaonekana kama serikali haitilii sana maanani vilio vya watu kutekwa, na kuna kila dalili hawa watekaji wanaahusika na vyombo vya dola vya serikali. Sasa lengo la kuchukua hatua kama hizi kama wananchi ni kuhakikisha kwamba kama mtu anachukuliwa na polisi basi ijulikane rasmi na wananchi kwamba amechukuliwa na polisi. Kuna utaratibu unaokubalika Poilisi wanapotakiwa ku-arest mtu, na sio huu wa utekaji. Polisi wanaofanya hivyo nia yao ni mbaya tu mara zote, ndio maana hawaji na uniform au gari zenye nembo ya Polisi, na wanatumia namba feki za gari.
Kama abiria ndani ya basi alimokuwemo Mzee Ali Kibao wote wangekataa asishushwe hadi waje Polisi wanaojulikana, huyu mzee angekuwapo hadi leo.
Na kuna minong'ono kwamba wafuasi wa CCM baada ya kujua wanaotekwa mara nyingi ni wa vyama vya upinzani, hawataki kutoa msaada wakiona mtu anatekwa. Siamini kama hili ni la kweli, na kama ni kweli wafuasi wa CCM waelewe kwamba kuna ndugu zao, rafiki zao nk wako upinzani na wao wanaweza kutekwa na kuuawa pia!
Tunasaidia watu wanapoibiwa simu zao za China, tutaachaje kusaidia watu wanapokuwa kwenye hatari ya kunyang'anywa uhai wao? Tusiangalie tu kama nyumbu wanavyoangalia mwenzao akikamatwa na kuliwa na simba. Tuwe kama nyati jasiri, tuwafuate watekaji katika umoja wetu, vichwa na pembe zetu mbele kupambana na umafia huu!