Msanii ambaye ni rapper mkongwe wa muziki wa bongo fleva Witness, amefunguka kuhusu picha yake iliyoleta utata kwenye mitandao, na kusema hakuwa na nia mbaya alipoipost.
Witness ameyasema hayo katika kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa alipost picha hiyo akiwa na lengo la kuwaonyesha watu ni jinsi gani amepungua na kuwaelimisha nini cha kufanya, lakini watu wameichukulia tofauti.
Pia msanii huyo amesema hawezi kumzuia mtu kuwa na mtazamo tofauti kwa kupost picha hiyo, kwani binadamu wanatofautiana kimawazo.
“Ni kwamba sisi binadamu tuko tofauti hauwezi ukamridhisha kila mtu, mimi nimeweka kwa lengo la kuelimisha kuhusiana na masuala ya kupungua, mwengine anaona kwa lengo lake yeye mwenyewe tofauti, kwa hiyo malengo yanatofautiana, unaweza ukafanya kitu ukaona hiki kitu kizuri, mwengine akaona kitu kibaya, so now nimeweka hiyo picha kila mtu anasema kivyake, I dont real understand”, alisema Witness.
Pia Witness amewataka watu watambue kuwa pamoja na wao kuwa wasanii lakini wana maisha yao mengine, na kuwataka wamuache aishi maisha yake. “Unatakiwa ufike wakati ambao watu wajue kabisa kwamba sometimes nina vitu ambavyo nnaweza nikaamua kuvifanya, so can they just leave me alone.”, alisema Witness.
Hiyo kufuli ni maalum kwa akili ya kwenda haja ndogo amesimama. Tofauti na nyie wote, mimi nampongeza kwa kazi nzuri japo sijui hata nyimbo yake yoyote.